Je Ungependa Kuyajua Maeneo Kumi Ambayo Fedha Imejificha...?
Habari yako rafiki yangu! Ni matumaini yangu u mzima wa afya! Karibu kwenye mwendelezo wa somo letu linaloangazia kuhusu maeneo kumi ambayo fedha Imejificha!
Kama unakumbuka vizuri makala iliyopita ilidokeza maeneo matatu, makala hii ni mwendelezo wa makala iliyopita!
Sasa unaweza kusonga nayo kwa kuyapitia maeneo mengine matatu kati ya kumi ambayo fedha imejificha kama ifuatavyo:-
4. Fedha imejificha kwenye fursa
Tatizo la mtu moja ni fursa ya mtu mwingine kutengeneza fedha, na ndiyo maana ikitokea mtu amekuja kwangu kuuliza jambo kuhusu tatizo fulani, huwa nalichukulia tatizo lake kama fursa ya kutengeneza fedha.
Kutokana na hilo huwa nasimama kama mtu wa kutatua tatizo lake, na kama itashindikana huwa nasimama kama dalali wa kumuunganisha na mtu mwingine atakayemtatulia tatizo lake kwa kamisheni! Kumbuka awali tuliona kwamba matatizo ya watu ni fursa za kutengeneza fedha!
Hata hivyo wapo watu ambao hudhani kufanikiwa kifedha ni bahati, kitu ambacho siyo sahihi. Ukweli ni kwamba bahati hutokea pale ambapo maandalizi yamekutana na fursa.
Kwa kusema hivyo kama utakuwa umejiandaa ni rahisi sana kukutana na fursa itayokufanya utengeneze fedha.
Unatakiwa kujua kwamba fursa ikija haitakusubiri kwa madai ya kusema ukajiandae kwanza, bali itaenda kwa yule ambaye alikuwa amejiandaa kwa ajili ya fursa hiyo!
Unachotakiwa kufanya ni kujiwekeza kwa ajili yako kwanza, mpaka pale utakapojujua wewe ni nani na unaweza ukafanya nini! Ukiweza kufanya hivyo utajua ni aina gani ya tatizo ambalo unaweza ukalitatua.
Baada ya hapo anza kutatua tatizo lako kidogo kidogo, ipo siku utashangaa fursa kubwa sana inakuja mbele yako ambayo itakutengenezea fedha nyingi sana!
Rafiki, unatakiwa ukae ukiwa umejiandaa kwa maana muda wowote ule na wakati wowote ule lolote lile linaweza likatokea.
Kama una uwezo wa kufanya jambo Fulani anza kulifanya, tena unatakiwa ulifanye kwa mwendelezo ipo siku moja inakuja itakayobadili historia ya maisha yako!
5. Fedha imejificha kwenye mbegu
Kila jambo lolote lile lililo kubwa lilianza kama mbegu iliyofukiwa, baada ya hapo ikamea na matokeo yake ikazaa matunda mengi sana.
Kwa kusema hivyo hata fedha imejificha kwenye mbegu. Hii ni sawa na kusema, pato lako unalotengeneza sasa ni mbegu unayotakiwa uipande ili uje uvune fedha nyingi zaidi miaka kadhaa ijayo huko mbeleni!
Na, ndiyo maana hesabu ya mti mmoja haifanyi msitu lakini kila msitu huanza na mti mmoja. Hata hivyo unaweza ukahesabia mbegu zilizopo ndani ya chungwa moja, lakini huwezi ukahesabia machungwa yaliyobebwa ndani ya mbegu moja.
Hii ni sawa na kusema unaweza ukahesabu fedha ulizonazo sasa kuwa ni kiasi kadhaa, lakini huwezi kuhesabu kiasi cha fedha kitakachotengenezwa pindi utakapozipanda na kuzifukia fedha zako kama mbegu.
Je, unafanya nini na fedha zako unazotengeneza sasa? Je, unafanya nini na wazo lako ulilo nalo? Je, unafanya nini na hicho ulicho nacho mkononi mwako?
Rafiki unatakiwa kujua kwamba hata mwanaume alianza kama mbegu kwanza kabla hajawa mwanaume, ndipo akawa mwanaume. Vilevile hata mwanamke naye alianza kama mbegu kwanza kabla hajawa mwanamke, ndipo akawa mwanamke.
Hata hivyo, kutoka kwenye shahawa ambayo ipo katika hali ya kiminika hupatikana mtoto ambaye siyo kimininika kama mbegu yake ilivyokuwa.
Hii ni sawa kusema kuwa, mbegu ikipandwa huleta matokeo tofauti kabisa na vile ilivyokuwa kabla haijapandwa na kufukiwa. kwa kusema hivyo unatakiwa ujue kwamba fedha yako ya leo ndiyo mbegu unayotakiwa uipande kwa ajili ya kesho yako.
Hivyo basi hutakiwi kumaliza fedha zako zote leo, kwa sababu kesho yako bado yaja na hakuna aijuaye kesho! Rafiki usile mbegu halafu utegemee utavuna.
Fedha ni mbegu kwa kusema hivyo, huna budi kutumia pato lako la sasa kama mbegu unayoipanda kwa ajili kesho yako!
6. Fedha imejificha kwenye bidhaa na huduma
Je, ni kiasi gani cha fedha ulichotumia miezi sita iliyopita? Je, ulitumia kufanyia nini?
Friend unatakiwa kujua kwamba, umeweza kutumia kama asilimia 75% hadi 100% ya fedha zako kwa ajili ya kununua bidhaa mbalimbali au kufanya malipo kwa ajili ya huduma Fulani!
Unachotakiwa kujifunza hapa ni kwamba fedha yako imeweza kutoka kwako na Kwenda kwa wengine kwa sababu, watu hao kuna huduma wanatoa au kuna bidha wanauza!
Mbali na hilo umeweza kutumia fedha zako kwa kulipia huduma/bidhaa ambazo zina nembo ya watu wengine. Hii ni sawa na kusema watu wanaotoa huduma hizo au bidhaa hizo ndiyo wanakuchukulia pesa yako.
Je, huwa haulipii kwa ajili ya chakula? Je, huwa hulipii kwa ajili ya usafiri? Je huwa hulipii kwa ajili ya nguo? Je, huwa hulipii kwa ajili ya kodi?
Kama umeweza kutumia fedha zako kulipia hayo yote, maana yake hata wewe unaweza ukawatimizia watu wengine mahitaji kwa kuwauzia bidhaa Fulani au kwa kutoa huduma Fulani!
Je, leo hii una bidha gani/huduma gani unayoitoa ambayo watu watakuwa tayari kuilipia?
Ndugu fedha imejificha kwenye huduma na bidhaa, tengeneza bidhaa zako kwa maana dunia inakusubiri!
Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri!
Mwendelezo Wa SoMo Hili Utaendelea Kwa Siku Ya Kesho!
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!
Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 07 44284329/0673184329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com
Comments
Post a Comment