Usimtendee Mwenzako Yale Usiyependa Utendewe Na Wewe "The Golden Rule"...
Hivi unafahamu kwamba Moja ya sababu kubwa ya magumu ambayo wanadamu tunakutana nayo ni kwa sababu ya kukosekana kwa upendo baina yetu? Ukweli ni kwamba, tungekuwa tunawatendea wenzetu yale ambayo tungependa sisi wenyewe tutendewe, basi kusingekuwa na chuki, hasira, vinyongo pamoja na visirani. Lakini haya yote yametapakaa katika kizazi hiki cha leo, kwa sababu tunawatendea wenzetu yale ambayo sisi wenyewe hatupo tayari tutendewe, na endapo itatokea tumetendewa basi tunaanza kuchukia na kujenga hasira kali vifuani mwetu! Mhubiri 7:9 Neno la Mungu linasema; “Usifanye haraka kukasirika rohoni mwako, kwa maana hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu” Rafiki unatakiwa kujua kwamba, hasira huwa haimletei madhara yule anayechukiwa bali humuumiza zaidi yule anayechukia. Hii ni sawa na kusema, ukiwa na hasira maana yake una fikra hasi kichwani mwako, na hiyo fikra hasi ndiyo inakufanya uwachukie wenzako pamoja na kuwatendea yale ambayo wewe mwenyewe hupendi kutendewa! Hebu j...