Posts

Showing posts from December, 2025

USIISHI KWA SABABU ZA WENGINE KAMA HUJAZIELEWA SABABU ZAKO

Image
Anayekusukuma ufanye jambo fulani mara nyingi huwa hakuambii kwa upendo, bali kwa kutaka kukuona ukifanana na wengine. Anajisitiri nyuma ya neno ushauri, ili siku ukiharibikiwa, akae pembeni akucheke kimya kimya. Utasikia wakisema:  “Umri umeenda, oa/olewa—unasubiri nini?” “Wenzako wa umri wako wamejenga, wana familia, wana maisha—na wewe je?” Wanaposema hivyo, hawajui jambo moja muhimu sana:  kila MTU ana sababu zake za kuishi, na sababu hizo hazifanani. Tofauti hizo si kasoro— ndizo zinazokamilisha uhai wa sisi Watu. Sababu za UWEPO wangu si sawa na zako. Ninachokifanya mimi hapa si kila MTU anaweza kufanya. Na hilo lina maana moja tu: zipo sababu maalumu zinazonizunguka zinazonilazimisha nifanye ninachofanya. Nimesoma na wenzangu shule ya msingi, hawafanyi ninachokifanya. Sekondari—hawafanyi. Advance—hawafanyi. Chuo—hawafanyi. Wafanyakazi wenzangu—hawafanyi. Hata tunaokaa nao—hawafanyi. Kiufupi, wananishangaa. Wamebaki midomo wazi. Wananiona si MTU wa kawaida. K...

AFRIKA: KABLA YA AKILI PANDIKIZI, KABLA YA IMANI YA NGUVU, NA KUPOTEA KWA UTAMBULISHO...

Image
Walikuja wakavikuta vya kwetu vikiwa timamu. Wakavivuruga. Wakaleta vya kwao. Vikatutoa kwenye mfumo wetu. ...Na leo—hatujijui! Haya si maneno ya hisia. Ni mwanzo wa kukuleta kwenye ukweli. Historia ipo wazi kabisa: bara la Afrika halijawahi kwenda kuharibu, kutawala, au kusababisha migogoro katika mabara mengine.  Afrika halikuwahi kuwa bara la uvamizi; lilikuwa - na bado ni—bara la uhai. Lilijua mema ya kuishi. Lilijua ukweli wa kuishi. Lilijua umoja wa watu, upendo, undugu na uwiano kati ya watu, asili na Uungu. Kwa maana hiyo, katika kuishi kwako leo, kama hujawahi kuyaelewa mema ya wazazi na mababu zako, na ukahisi walikuwa wapotevu au waliishi gizani, basi ujue fikra zako zilipinduliwa kabla hujazaliwa. Mema ya wazee wetu hayakupotea yenyewe - yalipinduliwa kwa makusudi. Yakavunjwa. Yakadharauliwa. Kisha yakapandikizwa akili nyingine na imani nyingine. Hili halikufanyika kwa bahati mbaya. Lilifanyika kwa mkakati. Mkakati ulikuwa mmoja: mkate mizizi, mabadilike kia...

Aliyekuahidi Connection Ameondolewa Kwenye Mfumo, Jiinue Ustahili Kuunganishwa Na Wengine...

Image
Leo nimechukua muda wangu kuandika jambo ambalo limekuwa likiwatesa wengi kimya kimya: Connection.  Nafasi.  Fursa.  Milango ya kupanda ngazi. Ni ukweli ulio thabiti, kila siku tunasikia malalamiko: “Nimehangaika lakini sifanikiwi,” “Nimeahidiwa connection lakini imegoma,” “Hakuna anayeniona.” Kwa BAHATI Mbaya hata wale  watu waliokuahidi connection, nafasi, msaada au mlango fulani wa mafanikio, leo hawapo tena kwenye mfumo. Hiyo haitakiwi kukukatisha tamaa; inapaswa kukutia akili. Kwa sababu connection ya kweli haitegemei mtu, mfumo au huruma.  Connection ya kweli inategemea thamani yako. Kwa mantiki hiyo kabla ya kuuliza “nani atanisaidia?” Jiulize kwa uaminifu:  Nimekuwa mtu wa aina ipi kiasi cha mtu kuniona na kusema -“huyu namchukua”? Hii si hoja ya kujilaumu. Ni hoja ya kujiamsha. Kwa sababu hakuna connection ya kudumu inayojengwa juu ya mtu asiyejiinua. Hebu tazama maisha yako kwa jicho la mtu mzima: Fikra zako zinajenga au zinabomoa? Mti...

Kabla Hujaipa Dunia Lawama, Kagua Ridhio Zako...

Image
Utasikia mtu akilalamika: “Maisha yangu yameharibiwa kwa sababu ya fulani…” Lakini mara nyingi husahau kuwa, katika kile anachokiita kuharibiwa, yeye mwenyewe alichangia—kwa sababu aliweka ridhio yake. Ni muhimu ieleweke: viumbe huishi kwa ridhio. Kila ridhio hukubalika pale pande mbili zinapokubali kufanya jambo fulani.  Ridhio hiyo ndiyo inayotoa kibali cha tukio kutokea.  Hili si suala la kijamii tu; hata kimungu ni fasaha. Kufanya jambo kwa kulazimisha, bila ridhio ya upande wa pili, ni kukengeuka katika haki—na hata kimungu, hauko sawa. Ukikubali kumkopesha mtu fedha, halafu akakudhulumu, kabla hujalaumu tafakari: ridhio yako ndiyo iliyomfungulia mlango huo. Ukikopa fedha kwa mtu, ukaweka ahadi ya kurudisha, kisha ukaanza kuleta kona nyingi wakati wa kulipa—hujaikiuka sheria ya mtu mwingine; umeenda kinyume na ridhio yako mwenyewe. Ukikubali kuingia kwenye mahusiano na mtu, mkashiriki safari moja ya kihisia na kijamii, kisha mkaishia kuachana, usianzishe lawam...

“Kifo: Mlango wa Uhai, Sio Hukumu...”

Image
Leo ninazungumza nanyi kuhusu jambo ambalo limekuwa likitawala maisha ya viumbe vyote tangu mwanzo wa uumbaji: KIFO. Na kabla sijaanza kwenda mbali zaidi, hebu tuanze kwa swali rahisi lakini zito: Kama kifo ni matokeo ya dhambi, kwa nini ndiyo kinachotumika kama njia ya kuingia Ufalme wa Mbinguni?  Je, huo Ufalme ni wa wema au waovu? Kama ni wa wema, iweje waingie kupitia njia inayodaiwa kuwa ovu?  Na kama ni ufalme wa waovu, basi kwa mantiki hiyo, kifo kingekuwa njia sahihi, ijapokuwa kifo chenyewe si matokeo ya dhambi. Haya maswali ya msingi yamewafanya wengi wafikiri juu juu, bila kuingia kwenye uhalisia wa maisha na kiini cha uumbaji. Kwanza, tuweke wazi: kifo ni sehemu ya mfumo wa uishi. Ni mlolongo wa asili, sheria ya uumbaji ambayo kila kiumbe hupitia.  Hata kabla ya simulizi za “tunda kuliwa,” viumbe waliishi na walikufa.  Taratibu za JADI zinaonyesha wazi kwamba MTU wa kwanza, alikufa zaidi ya miaka milioni 11 iliyopita.  Lakini simulizi la ...

“Waonjaji Wamepoteza Ladha, Sasa Ni Wakati Wetu Wa Kuamka...”

Image
Siku hizi mambo yamebadilika sana, kwani hata matunda nayo yamekuwa tayari kuonjwa na waonjaji kabla ya kuhifadhiwa kabatini.  Inashangaza sana. Sijui tunaenda wapi kama hata matunda yanataka kuliwa kwanza ndipo yahifadhiwe… Mimi mwenyewe nipo nashangaa TU naona ule usemi wetu unaosema; “mbuzi kafia kwa muuza supu, ukitimia... ... hahaha waone wanywa supu wanavyocheka.” Ni ujinga tu, lakini ndiyo hali halisi ya leo. Eti matunda yanadai na yenyewe yanataka kuonjwa kwa sababu walaji nao siku hizi midomo yao haifanyi kazi, kana kwamba midomo ipo kwa ajili ya kuzungumza tu.  Haya mambo hayatakaa  sawa. Zamani waonjaji walikuwa wanahofia kuuziwa mbuzi kwenye gunia. Ulikuwa unaweza ukanunua mbuzi, kumbe ule mfuko wa kuhifadhi upepo umetoboka au umeharibika.  Sio kwamba waliumbwa hivyo na Mungu, hapana ni makosa ya mahesabu wakati wa kuonjwa.  Upepo ulipojaa, puto likavimba, aliyesababisha puto akasema siwezi kulea, aliyebeba puto akasema; "wakati ulikuwa b...

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Image
Aliyetupa Uhuru, Ndiye Aliyerudi Kuuchukua... Afrika tulipewa uhuru, lakini hatukuachiwa uhuru wa kuwa huru. Tulipatiwa uhuru wa kupeperusha bendera, lakini hatukupatiwa uhuru wa kujitegemea kiakili. Tulipewa serikali, lakini hatukuachiwa mamlaka ya maamuzi huru. Tulipewa katiba, lakini hatukuachiwa utambulisho. Kwa hiyo leo tunaposherehekea uhuru, tunasherehekea nini hasa? Je, tunasherehekea kile tulichodhani tumepata, au tunasherehekea kivuli cha kile tulichonyang’anywa? Je, Ni nani aliyewanyang’anya uhuru wenu? Uhuru wenu ulikuwa upi? Ulichukuliwaje? Ulikuwa wapi? Na mliporudishiwa, mlipatiwa nini hasa? Kwa sababu uhuru wa kweli hauishi kwenye vitabu, wala kwenye hotuba, wala kwenye kumbukumbu za historia, unaishi katika akili aa WATU. Maana ya uhuru ni hali ya kiakili. Lakini kama fikra zako bado zinamilikiwa na mifumo ile ile iliyokuja kukuteka, unaweza kweli kusema kuwa wewe ni huru? Leo hii watu bado hawaamini kilichotokea. Wamebaki wakishangaa, midomo wazi, kwa saba...

“Wewe Ni Nani Katika Mnyororo wa Tumaini la Maisha?”

Image
Maisha yamejengwa juu ya kanuni moja kubwa: kusaidiana. Hakuna kiumbe kinachoweza kuishi peke yake. Hakuna aliyejitosheleza.  Kila nafsi, kila uhai, kila pumzi, vyote vimefungamanishwa ili kuendeleza muendelezo wa uhai. Na ifahamike kuwa, Mungu huwa haingilii maisha ya kiumbe moja kwa Moja, lakini mambo aliyoyaumba ndiyo yanashikamana kuendeleza maisha. Huo ndiyo muujiza wake mkuu, muujiza wa mfumo, si muujiza wa upendeleo. Muujiza unaohakikisha kwamba chochote kilicho hai kina nafasi katika dunia hii. Kama mambo ya Mungu yanatupa msaada wa kuishi, maumbile yake, sheria zake, pumzi, ardhi, mvua na uhai, basi sisi watu tunapaswa kuwa mwendelezo wa msaada huo. Mungu anatoa chanzo cha uhai, lakini wanadamu wanatoa muunganiko wa safari ya uhai. Yeye hatushiki mkono moja kwa moja, lakini ametupa uwezo wa kushikana sisi kwa sisi. Hivyo msaada wa Mungu hutupa uhai; msaada wa watu hutupa matumaini. Mambo ya Mungu hutuwezesha kuishi, lakini watu ndio hutusaidia kuishi kwa maana....

“Tajo 12 za Uwepo Usioishi: Safari ya Kuibua Hekima ya Mungu...”

Image
Nikisema “Amani ya ya Mungu idumu kwetu,” nawe huna budi kuitikia kimoyomoyo kwa kusema; “Idumu - na kwa wengine wote pia,” Nimeanza kwa kulitaja Jina lake Mungu, Muumba wa viumbe vyote.  Yeye aliyefanya maisha kwa amani na wema, ingawa watu mara nyingi wamemvisha hadithi za uongo, na kumfanya awe mwandishi wa kila baya na kila maumivu yanayotokea duniani. Kwa kuona jinsi jina lake linavyopotoshwa, nimeona nitoe hili somo, si kwa madai ya kutumwa, maana Mungu hana watumwa, bali kwa sababu Ukuu wake hausimami kwa imani zetu, bali kwa uhalisia wake usiotetereka. Yeye alifanya maisha bila mashauriano yetu; akaandaa Mfumo ulioanzisha maisha na kutenda kazi Kubwa bila hitaji la ibada, maneno au sifa.  Tulizaliwa tukaukuta huo Mfumo. Tutakufa tukiwa bado ndani ya huo Mfumo. Na hata waliotupotosha wao wenyewe waliukuta mfumo, waliishi ndanimo na watauacha ukiendelea hadi mwisho wa uumbaji. Tuliukuta. Tutaondoka. Lakini Mfumo huo utaendelea hadi ukomo wa dunia na pumzi ya ...

Uwezo Wa Ndani Unaotengeneza Matokeo Ya Nje

Image
Leo kijana wenu niko hapa na jambo zito, jambo linalohitaji utulivu wa kiwango cha juu. Kwa hiyo, tafadhali… vuta kiti, kaa kwa kutulia, halafu pumua polepole. Na kama una popcorn, endelea tu kutafuna; unaweza hata kushushia soda baridi bila haraka. Nataka tuzungumze kama marafiki wawili waliokutana kwenye chemchemi ya ukweli. Kwa sababu jambo la leo linaingia moja kwa moja kwenye kiini cha mafanikio ya ya kiumbe MTU, kile ambacho wengi wanakitamani, lakini wachache wanakitafakari kwa undani. Wacha nikuulize swali moja rahisi lakini zito: Kwa nini kila mtu anatamani mafanikio, lakini si kila mtu anayafikia? Ndiyo msingi wa mazungumzo yetu ya leo. Kila mtu anatamani kufika hatua fulani maishani. Kila mtu anatamani siku moja historia yake itajwe mahali kwa adabu kubwa.  Hii si hulka ya watu pekee, hata viumbe vingine vimeumbwa na hamu ya kupanda juu. Lakini leo nataka kuzungumza na wewe, mtu ambaye ndani yaki kuna kiu ya kupata matokeo makubwa kuliko unayoishi sasa. Kitu ...

USIKUBALI MADENI YAONGOZE MAISHA YAKO...

Image
Kwa muda mrefu sana tumezoea kusikia msemo huu: “Usiogope kukopa, hata serikali inadaiwa… wewe ni nani usidaiwe?” Ni msemo maarufu, wa kishujaa kwa kusikika -lakini kwa ndani unaumiza, hasa pale mtu anapozongwa na madeni na hana tena mwelekeo wa kifedha. Ukweli mchungu ni huu: Wengi wamefikia hatua ya kukopa ili kulipa deni jingine, yaani mzunguko hatari unaowafanya waishi kama mateka wa madeni. Unakuta umemuahidi mdeni wako kuwa kesho utamlipa. Lakini unajua wazi huna pesa.  Presha inakuja, usingizi unapotea, na unachokifanya mwisho wa siku ni kukopa kwa mtu mwingine ili kufunika shimo moja na kufungua jingine. Hii ni hatua mbaya sana katika maisha. Inakugeuza kuwa mtumwa wa madeni, unafanya kazi si kwa ajili ya kujenga maisha yako, bali kulisha madeni.  Ndipo ndoto zako zinakuwa mbali na ukuaji wa kiuchumi unadumaa. Ukianza kufanya kazi ili kulipa madeni badala ya kujenga mustakabali, unakuwa umeingia kwenye aina fulani ya utumwa wa kisasa. Kipato chako kinachosh...

“Thamani Haipimwi na Dunia, Inajengwa Ndani Yako...”

Image
Watu wamekuwa wakisema maneno yanayoumiza kama vile, “Usioe mwanamke wa kabila fulani kwa sababu ni chawote,” au “Usiwe na mwanamke mzuri sana sababu hao hawatuli,” na wengine hata kusema, “Usihusiane na asiyeokoka, si mwaminifu.”  Lakini kabla hatujakubaliana na misemo hiyo, ni muhimu kurudi nyuma kidogo... Kabla dini hazijaja, kabla miiko ya leo haijatungwa, watu walikutwa wanaishi, wakipendana, wakiishi kwa adabu na makubaliano yao.  Je, tuseme bibi zetu na mama zetu waliotupatia uzao huu walikuwa “chawote”? Hapana.  Kwa sababu mtu si kabila lake, mtu si sura yake, mtu si uzuri wake, wala mtu si imani yake.  Maadili ya mtu hubebwa na mtu mwenyewe. Tabia ya mtu ni zao la malezi, mazingira, historia za ndani, imani anayoishi nayo, maumivu aliyoyapitia, mitazamo yake na hata maendeleo yake ya kiakili na kiroho - si kabila lake. Sasa unatoa wapi ujasiri wa kumhukumu mtu kupitia kabila lake, sura yake, au imani yake, ilihali kila mmoja ametengenezwa na safa...

ONYO! Usijaribu Kubadili Maisha Yako Kabla Hujasoma Huu Ujumbe Mpaka Mwisho…

Image
Rafiki yangu mpendwa… Kabla hata sijakuambia chochote, kuna jambo moja nataka nikuulize. Usiogope… si mtihani. Sihitaji jibu lako kwa sauti. Jijibu moyoni mwako tu. Ulishawahi kukaa peke yako ukahisi kwamba kuna nguvu kubwa sana ndani yako… nguvu ambayo unajua kabisa ipo, lakini maisha, presha, majukumu, na mfumo wa dunia imeikandamiza kimya kimya? Ulishawahi kuhisi kama kuna “wewe mwingine” ndani yako mwenye uwezo zaidi, ujasiri zaidi, maono zaidi, lakini kila ukitaka kumtoa nje, kuna kitu kinakuzuia? Kama jibu lako ni NDIO, basi fahamu hili kwa uhakika: Hauko peke yako. Na wala hujachelewa. Na wala hujaharibikiwa. Na wala hauko nyuma kama unavyohisi… Tafiti nyingi zinaonesha kuwa zaidi ya 80% ya watu duniani kote wanaishi chini ya kiwango chao cha utambuzi. Na, wanatembea, wanafanya kazi, wanacheka… lakini ndani hawako huru. Wanaamka kila siku wakiwa na roho nzito. Maisha yanakuwa magumu kuliko kawaida. Kipato hakikui licha ya juhudi nyingi. Furaha inapungua taratibu kama...