Posts

Showing posts from April, 2024

jinsi Ambavyo Kazi Za Fasihi Na Baadhi Ya Mafundisho Ya Dini Hupelekea Watu Wajifunze Vitu Visivyo Sahihi...

Image
Pasi na shaka una uelewa Fulani hivi kuhusu kazi za fasihi. Hata hivyo miongoni mwa tafsiri nzuri sana ninayoipenda ya fasihi ni ile inayosema; “fasihi ni kazi ya Sanaa inayotumia lugha ili kufikisha ujumbe kwa jamii iliyokusudiwa” Ukweli ni kwamba kwa kipindi cha muda mrefu, fasihi imekuwa ikitumika kama nyenzo ya kufikisha ujumbe kwa jamii hususani kuhusu masuala Fulani Fulani hivi yanayoendelea kwenye jamii inayohusika!  Habari mbaya na za kuhuzunisha zaidi ni kwamba, fasihi ya leo imeacha desturi yake ya muda wote! Yaani kutoka kwenye kuikomboa jamii kifkira kwa kuionya, kuielimisha na kuiasa hadi kufikia hatua ya kuanza kuipotosha jamii!  Na hii ndiyo sababu kubwa jamii imeweza kupotezwa na kuanza kushangilia uozo na uovu! Na ndiyo maana siku hizi nyimbo zisizo na maudhui yanayojenga zimekuwa zikikubalika zaidi ukilinganisha na zile nyimbo zenye maudhui yanayojenga na kumkomboa mtu Kifikra! Hebu jaribu kuvuta picha mambo yanayooneshwa kwenye video mbalimbali z...

Je, Unajua ni Sababu Gani ambazo huwafanya watu wengi wajifunze Mambo yasiyofaa maishani mwao? Kama Jibu Lako Ni Hapana, Soma Hii...

Image
Kwa mujibu wa kanuni ya matokeo na kichocheo inasema; “kila kitu hutokea kutokana na sababu”. Hii ni sawa na kusema kuwa, kuna kila sababu ambayo imepelekea watu wengi wajifunze vitu visivyo sahihi.  Na ifahamike kwamba kujifunza ni jambo ambalo linafanyika muda wote pasipo hiari. Hata sasa ubongo wako unaendelea kujifunza vitu vipya nikiwa naandika makala hii! Kwa kusema hivyo hapo ulipo na vitu vyote vinavyokuzunguka mahali hapo ni vyanzo vinavyotoa taarifa mbalimbali zinazoingia ubongoni mwako!  Na taarifa hizo zikishaingia ubongoni mwako ndizo zitapima kile kitakachoendelea kwenye fahamu zako, yaani kuanzia: hulka, tabia, Imani, matendo pamoja na mitizamo yako, ile hali ya kuona mambo katika maisha! Hata hivyo hakuna ambaye anaweza akauzuia ubongo wake usichukue taarifa kutoka kwenye vyanzo mbalimbali vinavyomzunguka, kwa maana ni jambo ambalo haliwezekani! Lakini kuna yupo mtu mmoja hivi mdadisi ambaye hataamini kila taarifa, huyu ndiye unayepaswa uwe na hiki ...

Hii Ni Kwa Watu Wanaotaka Kujifunza Vitu Sahihi Lakini Hawajaanza Bado....

Image
Kwa mujibu wa nadharia ya blank slate (tabura lasa) iliyoasisiwa na mwanafalsafa David hume inasema; “hakuna mwanadamu ambaye huzaliwa akiwa ana uelewa wa jambo lolote lile, kwa kusema hivyo vile mwanadamu atakuwa ni jumla ya mambo yote aliyojifunza na kuhifadhiwa kwenye ubongo wake”  Ukweli ni kwamba umekuwa hivyo ulivyo kwa sababu ya vitu ulivyojifunza tokea udogoni mwako. Unatakiwa kujua kwamba, kuna vitu umejifunza kutoka kwa wazazi wako na huenda havikusaidii, kuna vitu umejifunza kwenye mazingira yako lakini havijakusaidia, kuna vitu umejifunza kwenye jamii yako lakini havijakusaidia na kuna vitu umejifunza shuleni na pengine labda havijakusaidia. Hata hivyo huna budi kufahamu kuwa, kila mtu ni zao la kile alichojifunza, kwa kusema hivyo kama hutajifunza kitu sahihi huwezi ukawa mtu sahihi atakayeleta matokeo muafaka kwa sababu kilicho ndani ya ubongo wako hakijakufanya uwe mtu sahihi. Fahamu Kuhusu Aina Za Watu Kwa Mujibu Wa Kile Walichojifunza! Watu waliohitimu...

Tahadhari Huwezi Kuelewa Kujifunza Ni Nini Mpaka Usome Kwanza Hii...

Image
Bila shaka ushawahi kusikia neno kujifunza, na huenda hata wewe umeshajifunza vitu kadhaa maishani mwako. Kwa kusema hivyo endapo utaulizwa ufafanue maana ya neno kujifunza, pasi na shaka hutakosa cha kusemea.  Kwa tafsiri nyepesi neno kujifunza linaweza kufafanuliwa kama; kitendo cha kuchukua ujuzi, taarifa, maarifa au wazo kutoka chanzo fulani na kisha kupeleka ubongoni.  Na mara baada ya ubongo kupokea funzo hilo kuna mabadiliko ya haraka sana ambayo hutokea kwenye maisha ya yule aliyejifunza. Hii ni kwa sababu, kilichoingia kama funzo hubadilisha kile kitakachotoka kama matokeo. Kwa mantiki hiyo, mtu huyo atajikuta akibadilisha hata matokeo anayoweza kuyaleta kwa kutumia maarifa ya kile alichojifunza!  Na ndiyo maana watu wengi hubadili maisha yao mara baada ya kujifunza. Kwa kusema hivyo mtu huyo hujikuta akianza kuratibu matendo yake yalandane na kile alichojifunza. Kitu unachotakiwa kuzingatia hapa ni kile unachojifunza! Kama utakuwa umejifunza yale yas...

Je, Wewe Ni Mjifunzaji Mzuri Lakini Umeishia Kujifunza Vitu Visivyo Sahihi? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...

Image
Hivi unafahamu kwamba Zaidi ya asilimia 80 ya watu wametumia muda wao mwingi kujifunza lakini wameishia kujifunza vitu visivyo sahihi?  Ukweli ni kwamba watu wengi chini ya mwamvuli wa elimu na mafunzo wameishia kujifunza vitu visivyo na msaada, na ndiyo maana mwisho wao umekuwa ni: mateso, shida, taabu, magumu na mapambano kwa sababu kile walichojifunza hakijaweza kuwarahishia maisha! Lengo kuu la kujifunza ni kutumia kile ulichojifunza ili kurahisisha maisha yako, kwa hiyo inapotokea umejifunza lakini bado hujaweza kuyarahishisha maisha yako kupitia kile ulichojifunza, maana yake huenda kile ulichojifunza hakijakusaidia katika lolote lile. Unachopaswa kujua ni kwamba, siyo kila kinachofundishwa kinafaa kulishwa kwenye ubongo wako. Hata hivyo, huna budi kufahamu kuwa, kama vile unavyokuwa kimwili kutokana na kile unachokula, vilevile unakuwa kimaisha kulingana na kile unachoulisha ubongo wako. Ukweli ni kwamba siyo kila funzo linafaa na siye kila anayefundisha anafaa. ...

Je, Unataka KUJUA Kwanini Mahusiano Mengi Huvunjika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...

Image
Wadau walisema “kila kitu hutokea kutokana na sababu”. Hii ni sawa na kusema kuna kila sababu zinazopelekea kuvunjika kwa mahusiano mengi yanayoanzishwa. Na, ukweli mchungu hakuna kitu ambacho huuma kama kuvunjika kwa mahusiano yanayohusisha wenzi wawili ambao walipendana kwa dhati, na walikuwa na ndoto za kufika mbali Zaidi!  Hata hivyo katika zama hizi kuvunjika kwa mahusiano halijawa jambo la kushangaza tena, bali limeonekana kama jambo la kawaida tu na watu wanalifurahia na kulishangilia! Je, kipi hasa ni chanzo cha mahusiano mengi kuvunjika? Fuatana Pamoja nami: 1. Kupuuza Unganiko La Kiroho Kabla Ya Kuanzisha Mahusiano... Mwanadamu ni roho, nafsi na mwili. Mwili ni kama nyumba tu lakini mwanadamu halisi ni roho. Ukweli ni kwamba watu wengi wanahusiana kimwili na si kiroho, na ndiyo maana mahusiano hayo yamekuwa yakivunjika kwa sababu hayana unganiko la kiroho. Hata hivyo watu hawa hata wanapoanzisha mahusiano huwa hawaanzi na Mungu, badala yake huanza kwanza na ku...

Je, Unataka Kujenga Mahusiano Sahihi Yatakayodumu? Kama jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...

Image
Bila shaka ulishawahi kupenda/kupendwa mpaka ukaona dunia imekuwa ndogo kiasi kwamba ukatamani kama kungekuwa na uwezekano, mngeongezewa nafasi nyingine ya dunia, au mngepewa dunia yenu ambayo mngeishi ninyi mkiwa wawili tu!  Na, huenda ulishaweka mpaka ahadi ya kumpenda mwenzi wako maisha yako yote.  Au, huenda mwenzi wako naye aliweka ahadi ya kukupenda maisha yake yote! Lakini mwisho wa siku upendo wenu haupo tena na ahadi zenu zote mlizoweka ziliishia njiani! Hivi ushawahi kujiuliza ni kipi kilichopelekea safari yenu iishie njiani mbali na kuwa ilianza kwa mbwembwe kama zote?  Unatakiwa kujua kuwa, mahusiano mengi hufa kwa sababu wanaoyaanzisha wanakuwa hawajui wanakoyapeleka ni wapi, na kwa vile huwezi ukajua kama umefika ikiwa huijui hatima unayotaka kuifikia, basi hiki ndicho hutokea kwenye mahusiano ya wapenzi hao!  Hii ni sawa na kusema kwa vile hawajui hatima kamili ya mahusiano waliyoyaanzisha basi hujikuta wakishindwa Kwenda nayo mbali, matoke...