Ukiachwa Achika: Siri Kali ya Kuacha Kung’ang’ania Mtu Asiyekutaka...
“Yaani mimi maisha yangu bila Fulani haiwezekani… Yeye ndiye alikuwa kila kitu kwangu.” Hayo ni maneno yanayotoka kwa watu ambao mapenzi yamewachanganya kiasi cha kusahau kwamba hata kabla ya mahusiano hayo, maisha yao yaliendelea vizuri tu. Kwa sababu , kabla ya huyo mtu kuingia kwenye maisha yako, uliishi, ulipumua, ulifanya kazi, ulijipanga - na uliendelea tu bila kupasuka. Lakini leo hii, mtu akikuacha unasingizia dunia yote imekugeuka. Unajifanya huna uhai. Unajifanya huna thamani. Unajifanya huwezi tena. Tatizo ni kwamba wengi wamejigeuza kuwa vipenzi ving’ang’anizi. Hawataki kuachika, hawataki kukubali, na mbaya zaidi – mahusiano wanayong’ang’ania hayana mizizi. Waliingia kwa kukurupuka kama vitenzi vikurupushi, halafu mwisho wa siku mwenzako kageuka na kuwa kitenzi kikwamizi, wakati wewe umebaki kuwa kitenzi king’ang’anizi. Matokeo? Unageuka kipenzi king’ang’anizi. Wewe kubembeleza; mwenzako anakukomesha. Wewe kutuma SMS; yeye kuzifuta bila kuzisoma. Wewe...