Posts

Showing posts from December, 2023

Je, Unataka Kujenga Tabia Mpya Zitakazobadilisha Maisha Yako? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...

Image
Habari yako rafiki yangu? Ni matumaini yangu u mzima wa afya. Karibu kwenye mwendelezo wa somo letu linaloangazia kuhusu jinsi ya kuharibu na kujenga tabia mpya. Ikumbukwe m akala iliyopita ilidokeza ni namna gani unaweza ukaharibu tabia yoyote ile kwa kutumia kanuni kuu tatu za kubadili tabia. Makala yetu ya leo itaenda kukuonesha jinsi ya kujenga tabia mpya zitakakusaidia ubadili maisha yako kwa kutumia kwa kanuni kuu tatu za kubadili tabia! Je, nifanye nini ili niweze kujenga tabia mpya ambazo awali sikuwa nazo? Usijalii fuatana nami... 1. Vichocheo Vya Tabia (cues) ➡️Fanya Vichocheo Vya Tabia Unazozitaka Viwepo Mazingira Uliyopo Ili Vikuvutie Zaidi.  Unatakiwa utengeneze mazingira yako ya sasa ili kitendo cha baadae kifanyike kwa urahisi! Kumbuka usipoandaa mazingira yatakayokusaidia ufanye tabia unazozitaka hakuna atakayekuandalia, badala yake sasa mazingira uliyopo ndiyo yatakayokuamlia aina gani ya tabia uzifanye. Rafiki, unatakiwa kujua kwamba kila tabia unayoif...

Namna Ya Kuharibu Tabia Yoyote ILe Kwa Kutumia Kanuni Kuu Tatu Za Kubadili Tabia ...

Image
Habari yako rafiki yangu, ni matumaini yangu u mzima wa afya! Karibu kwenye mwendelezo wa somo letu linaloangazia kuhusu namna ya kuharibu na kujenga tabia mpya na zenye tija! Makala iliyopita ilidokeza kanuni kuu tatu zinazoonesha jinsi zambavyo tabia yoyote ile hupitia hadi kujengwa kwake. Kwa leo utaoneshwa jinsi ya kutumia kanuni hiyo katika kuharibu tabia yoyote ile. Songa nayo... 1. Vichocheo Vya Tabia Hiyo (Cues) ➡️Ondoa Vichocheo Vyote Kwa Kuvifanya  Visionekane Kabisa Katika Mazingira Uliyopo… Hakuna tabia ambayo haiendeshwi na kichocheo Fulani. Kila tabia unayoifanya tambua kwamba kuna vichocheo vinavyokusukuma ili uifanye na endapo pasingekuwepo na vichocheo hivyo kusingekuwa na sababu ya wewe kufanya tabia hiyo.  Kwa mfano unatumia muda wako vibaya kwa sababu kuna cues zinazochukua sehemu ya muda wako. Cues hizo zaweza kuwa: simu, tv, marafiki pamoja na mazingira ya starehe. Sasa basi kanuni hii inakutaka utoe vichocheo vyote vinavyokusukuma ufanye baad...

Fahamu Hatua Tatu Ambazo Kila Tabia Iliyokomaa Hupitia Kabla Haijatengenezwa...

Image
Hivi unafahamu kwamba kila tabia iliyokomaa ni lazima hupitia kwenye hatua kuu tatu ambazo hutumika katika kujenga tabia?  Huenda hata wewe umekuwa ni yule mtu ambaye, umejaribu kujenga tabia fulani lakini umeishia njiani! Usijue shida ni nini, kumbe shida ni kutokujua hatua hizi kuu tatu ambazo kila tabia iliyokomaa hupitia! Bila shaka unataka kujua hatua hizo muhimu, nami nakutoa hofu juu ya hilo kwani makala hii imedadavua suala hili kwa undani wake! Unatakiwa kujua kwamba,  endapo tabia haitapitia kwenye hatua hizi tatu katika kujengwa kwake basi tabia hiyo haitajengwa bali itakufa! Ukweli ni kwamba hatua hizi tatu hutegemeana na na hukamilishana! Hata hivyo ukomavu wa tabia hutegemea na kiwango cha ufanywaji na urudiwaji wa tabia hiyo!  Kwa ujumla zifuatazo ni hatua tatu ambazo hukamilishana katika kupelekea kutokea kwa tabia Fulani.  1. Kuwepo Kwa Vichochezi (Cues) Hivi ni vitu mbalimbali vilivyopo kwenye mazingira halisi ambavyo huuchochea ubongo u...

Fahamu Jinsi Ambavyo Tabia Hutengenezwa Kwenye Mfumo Wa Ubongo..

Image
Katika ulimwengu wa saikolojia inaaminika kwamba hakuna binadamu hata mmoja ambaye huzaliwa akiwa na tabia!  Dai hili ni kwa mujibu wa nadharia kongwe iliyoanzishwa na mwanafalsafa maarufu sana kuwahi kutokea duniani akifahamika kwa jina la David hume. Nadharia hiyo ilipewa jina la “blank slate/tabularasa”.         Kwa mujibu wa nadharia hii ni kwamba hakuna binadamu ambaye huzaliwa akiwa na tabia, ufahamu au uelewa wa jambo lolote lile.  Kutokana na ukweli huo madai ya nadharia hiyo kongwe yakahitimishwa kwa kuona kwamba vile mtu atakuwa kitabia, kimtizamo pamoja na kimienendo ni kumbukumbu za mambo yote yaliyoingia ubongoni mwake mara baada ya kuzaliwa kwake na kuanza kuishi hapa duniani. Unachopaswa kuchukua hapa ni kwamba kila tabia yoyote ile uliyonayo imetengenezwa na wewe mwenyewe. Yaani mbali na ukweli kuwa uliumbwa huna budi kukubali kwamba umejitengeneza mpaka ukawa hivyo ulivyo.  Kitu kingine cha kuongezea hapa unatakiwa kuj...

Huwezi Ukaelewa Tabia Ni Nini Mpaka Usome Kwanza Hii...

Image
Neno tabia huenda likawa siyo geni sana machoni pakao ewe mpenzi msomaji na sina shaka endapo utaulizwa ulitolee ufafanuzi utashindwa kulifafanua. Ni Imani yangu kuwa, maana yako haitakuwa mbali na ile isemayo; tabia ni jumla ya matendo yote pamoja na vitendo mbalimbali avifanyavyo binadamu katika maisha yake ya kila siku pasipo hata kutumia ridhaa/hiari yake. Hii ni sawa na kusema kuwa, mtu huyo hujikuta akiitikia kufanya baadhi ya vitendo na matendo mbalimbali automatiki pasipo hata kujua kuwa anafanya, kwa sababu siyo yeye anayetaka kufanya hivyo bali ubongo wake ndiyo unamchochea afanye hivyo.  Rafiki, unatakiwa kujua kwamba ubongo  humchochea mtu huyo, afanye tabia hizo kwa sababu anakuwa amezifanya kwa muda mrefu, kiasi kwamba tabia hizo zinakuwa zimepokelewa kwenye mfumo wake wa ubongo, matokeo yake ubongo huo huishia kumtengenezea mtu huyo mfumo wa kuratibu ufanywaji wa tabia hizo kila muda! Kutokana na hilo mtu huyo hujikuta akiitikia kufanya tabia hizo au...

Huwezi Kubadili Kilichotokea Pasipo Kwanza Kubadili Tabia Zilizopokelekea Kutokea Kwake…

Image
Hivi unafahamu kuwa hivyo ulivyo, hali unazopitia pamoja na hapo ulipo kimaisha ni matokeo ya tabia zako mwenyewe? Ukweli ni kwamba kuna watu wako leo hii wanalaumu kuhusu hali wanazopitia kimaisha, huku wengine wakiwa wanapambana kubadili matokeo yanayotokana na hali hizo, wasijue kwamba huwezi ukabadili kilichotokea kama hutaanza kwanza kubadili chanzo kilichopelekea kutokea kwake! Rafiki, unatakiwa kujua kwamba: umaskini, kutengeneza kipato cha chini, mateso, shida, taabu pamoja na maradhi mbalimbali yanayowakumba watu wengi ni matokeo ya tabia zao wenyewe. Ukweli ni kwamba tabia ni kama panga lenye makali pande zote mbili, ambalo hukata kotekote. Kwa mantiki hiyo tabia zako zinaweza kukupaisha mpaka juu mawinguni na kukufanya ufikie mafanikio ya kiwango cha juu, hata hivyo tabia zako zinaweza kukudimiza na kukushusha katika viwango vya chini na ukaonekana si kitu!  Kwa mfano tabia ya kuishi bila bajeti inaweza kukuingiza kwenye madeni pamoja na kukuletea umaskini, t...

Akipandacho Mtu Ndicho Akivunacho...

Image
Hivi unafahamu kwamba hivyo ulivyo pamoja na hapo ulipo ni mavuno uliyoyapata kutokana ya kile ulichokipanda katika maisha yako? Huenda hata wewe umekuwa ni miongoni mwa wale watu ambao wamekuwa wakilaumu kuhusu hali ngumu wanazokumbana nazo kila leo, wasijue chanzo ni nini, kumbe chanzo ni wao wenyewe! Unatakiwa kujua kwamba kile unachokifanya (kupanda) ndicho kinapima matokeo (mavuno) unayoyapata! Kwa mantiki hiyo kama utapanda upepo utavuna upepo, kwa maana katika hali ya kawaida huwezi ukapanda mchele halafu ukavuna mahindi! Ukweli ni kwamba kila mtu ana hulka ya kuwa na mafanikio pamoja na kuishi maisha yaliyojaa furaha, lakini ni watu wachache sana ambao huwa na utaratibu wa kupanda mbegu ambazo hupelekea mafanikio hayo! Kutokana na hilo, ni watu wachache tu ndiyo hupata mafanikio, kwa sababu walipanda mbegu zilizopelekea mafanikio hayo, huku wanaosalia wakibaki kulalama na wengine wakijisemea ipo siku mambo yatakuwa sawa. Wasijue kwamba Mambo hayawezi kuwa sawa bila ...