“Yule Unayemuona Ndani Ndiye Unayekuwa Nje..."
Hakuna mtu yeyote duniani mwenye mamlaka ya kupanga kiwango cha kujiona kwako isipokuwa wewe mwenyewe. Na hakuna MTU atakayekufanya ujione dhaifu bila wewe kumpa ruhusa hiyo ndani ya fikra zako. Ukweli mkubwa wa maisha ni huu: vile unavyojiona ndivyo unavyokuwa — na kwa kiwango fulani tayari umeshakuwa hivyo. Maisha hufuata picha iliyopo ndani ya akili yako. Kama ambavyo huwezi kukipata kitu ambacho hujakiona, vivyo hivyo huwezi kuwa mtu ambaye hujamuona ndani yako. Maono ya ndani ndiyo yanayochora uhalisia wa nje. Mtu haendi mbali zaidi ya pale alipoishia kujiona, kwa sababu hapo ndipo hujenga ukomo wake wa kufikiri. Mara nyingi huo ukomo si halisi bali ni taswira iliyojengwa na mitazamo, mazingira au maneno aliyoyakubali kuyahifadhi akilini. Kiwango cha kujiona ni kama ramani ya safari ya maisha. Inakuongoza kutoka ulipo sasa hadi pale unapojiona ukifika. Ndiyo maana kanuni ya msawazo wa akili husema kuwa uhalisia wa maisha yako ni kivuli cha picha iliyop...