Posts

Showing posts from August, 2024

Hii Ni kwa Wanaume Tu, Kama Una Nia Ya Dhati Ya Kuishinda Ngono ili utimize Kwanza Ndoto Zako Soma Hii...

Image
Wanaume wengi wameichoka tabia ya kutumikia ngono na pengine labda wanatamani kuiacha lakini hawajui wafanye kipi.  Kutokana na hilo, wengi hujikuta wakijizuia kwa muda mfupi tu baada ya hapo hujikuta wakiteleza tena na kuyarudia makosa yale yale. Huenda hata wewe ukawa umechoshwa kabisa na tabia hii, na kila ukijaribu kuacha, unaacha kwa muda tu. Baada ya hapo unajikuta ukitumikia tena  ngono.  Unatakiwa kujua kwamba, kosa siyo wewe bali kosa ni kutumia mbinu zisizo sahihi katika kuacha  huu utumwa  usio na faida!  Ukweli ni kwamba, watu wengi wanajua wanachokitaka lakini ni wachache tu ndiyo wanaojua wafanye nini ili wakipate kile wanachokitaka.  Hii inamaanisha kwamba wanaume wengi wanatamani kuachana na utumwa wa ngono lakini ni wanaume wachache tu wanaojua wafanye nini ili waache utumwa huo. Na hakuna kitu kizuri kama kufanya jambo kwa kutumia mbinu sahihi, kwa maana mwisho wake huwa ni kupata matokeo sahihi! Hiki ndicho ambacho makala...

Hizi Ndizo Baraka Zilizobebwa Na Maisha Yako Ukiwa Unaadhimisha Siku Yako Ya Kuzaliwa...

Image
Hbd to me, nawashukuru wazazi Wangu pamoja na Mungu mwenye vyote kwa Neema na rehema kwa maana hadi kufikia hapa nilipo haikuwa kazi rahisi!  Ninapoadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa Kwangu nachelea kukufahamisha kuwa, maisha ni kuishi na siyo kufanya majaribio! Kwa hiyo hutakiwi tu kuishi kwa sababu umepewa uhai bure, bali unatakiwa uishi kwa sababu kuna maono na kusudi ulilolibeba linalofanya maisha yako yawe ya thamani! Mnamo tar 23/08/199... Alizaliwa kijana mmoja hivi aitwaye Emmanuel Samuel! Kuzaliwa kwake ulikuwa ni ushindi mkubwa sana kwa sababu kila mtu hushinda kwanza ili apate kuzaliwa, na hakuna mtu ambaye huzaliwa huku akiwa hakushinda!  Kijana huyu hakuishia kushinda mara moja tu, hata sasa ni mshindi kwa sababu ameushinda ulimwengu kwa kuzaliwa upya kutokana na mbegu ya Mungu isiyoharibika! 1 Yohana 5:4 " Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu" Ukweli ni kwamba tunaishi kwenye ulimwe...

Kama Una Kiu Ya Kufanikiwa Na Kufika Mbali Kimaisha Huna Budi Kuepuka Falsafa Ovu Zifuatazo..

Image
Jambo moja la msingi unalopaswa kujua ni kwamba falsafa ni somo ambalo huchambua ukweli uhusuo maisha ya binadamu. Hivyo basi endapo ukweli huo utatumika vibaya au ukweli huo ukawa hauna kweli ndani yake, inamaanisha kwamba watu watautumia ukweli usio kweli kuongoza maisha yao, hali itakayosababisha wapate matokeo yaliyo kinyume na matarajio yao!  Hii ndiyo sababu kubwa utakuta mtu anafanya vitu vingi, anapambana sana, ana matumaini makubwa kuhusu maisha yake na anaamini kwamba ipo siku atafanikiwa, lakini hapigi hatua kimaisha!  Kumbe shida siyo mapambano anayoyafanya bali shida ni aina ya falsafa alizozichagua na kuziamini katika mapambano yake! Ukweli ni kwamba, katika kuishi kwetu wengi wetu tumejikuta tukiongozwa na falsafa za uongo, hali ambayo inakwamisha maendeleo yetu na kusababisha tushindwe kuzifikia hatima nzuri za kesho zetu!  Ili kubadili maisha yako ya kesho pamoja na kufanikiwa maishani, kuna baadhi ya falsafa na imani unatakiwa uziondoe na kuz...

Fahamu Kuhusu Hatua Kuu Tatu Za Ukuaji Wa Maisha Ya Binadamu Pamoja Na Yale Unayopaswa Uyajue Katika Kila Hatua...

Image
Hatua za ukuaji wa maisha ya mwanadamu zinaweza kugawanywa katika makundi makuu matatu.  Na katika makundi haya matatu mwanadamu huyo hana budi kuwa na ufahamu kulingana na kundi la hatua alilopo! Hii inamaanisha kwamba ni lazima kuwe na upatanifu kati ya ufahamu wake pamoja na hatua aliyoifikia!  Kwa mfano unapokuwa kijana kiwango chako cha uelewa hakipaswi kuwa sawa na kile kiwango cha uelewa ulichokuwa nacho ulipokuwa mtoto.  Hata hivyo unapokuwa mzee kiwango chako cha uelewa hakipaswi kuwa sawa na kile kiwango cha uelewa ulichokuwa nacho ulipokuwa kijana!  Sasa shida huwa inakuja pale unapojikuta wewe ni kijana na una uelewa wa mtoto mdogo au wewe ni mzee na una uelewa kijana mdogo.  Endapo itakuwa hivyo, unatakiwa kujua kwamba huwezi kufika mbali kimaisha! Watafiti wamebaini kwamba kuna hatua tatu za ukuaji katika maisha ya mwanadamu, na katika kila hatua mwanadamu anatakiwa awe na maarifa na taarifa sahihi hasa ukihusisha na hatua aliyopo. Na ...