Posts

Showing posts from February, 2024

Je, Siku Kuu Ya Krismasi Inatambuliwa Kwa Mujibu Wa Maandiko Matakatifu?...

Image
Bila shaka ulishawahi kujiuliza kwanini tarehe 25 disemba ilitengwa iwe ndiyo sikukuu ya krismasi, yaani iwe siku maalumu kwa ajili ya kusheherekea kumbukizi la kuzaliwa kwake Yesu, na huenda mbali na kujiuliza hivyo hukupata jibu. Na kama hujawahi kujiuliza basi leo tuuangalie uhalali wa maadhimisho ya siku kuu hii!  Angalizo: Sipingani na Imani ya mtu na wala sitaki mtu aachane na imani yake, hata hivyo sikulazimishi uamini kile ninachokiamini mimi. Lengo langu ni kuleta mjadala utakaoibua mtizamo mpya kuhusu mahusiano ya tarehe 25 disemba na kuzaliwa kwake Yesu!  Ukweli ni kwamba hakuna andiko lolote lililotuamuru tufanye kumbukizi ya kuzaliwa kwa Yesu tarehe 25 Disemba kila mwaka! Na kama hakuna andiko maana yake siku hii iliamriwa tu na mwanadamu mwenyewe.  Na ikiwa mwanadamu ndiye aliyeitenga tarehe hii, maana yake Mungu hayatambui maadhimisho haya. Ninasema Mungu hayatambui maadhimisho haya kwa sababu hakuna sehemu kwenye maandiko yake ambayo katuamuru ...

Pokea Salamu Za Mwaka Mpya 2024 kutoka kwa Emmanuel Samuel…

Image
Awali yeyote natanguliza shukrani kwa Mungu kwa kutulinda, kutusimamia na kutuongoza sote pamoja na kutuvusha kutoka 2023 hadi 2024. Rafiki, tumia sehemu ya muda wako kumshukuru Mungu haijalishi mwaka uliopita umepitia mangapi, unatakiwa kujua kuwa, ni neema kubwa sana kuweza kuuona na kuufikia mwaka mpya ukiwa hai.  Hebu rudisha sifa na utakufu kwa Mungu wako kwa maana haikuwa rahisi. Natambua kuwa umepitia mengi lakini nipo hapa kukusihi kuwa umshukuru Mungu haijalishi umepitia magumu mangapi! 2 Wathesalonike 5:18 “shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu”. Pili, natanguliza shukrani zangu za dhati kwako wewe ambaye umekuwa ukiguswa na masomo yangu, ikiwa ni pamoja na kuniunganisha na baadhi ya watu, kunipa fursa za kuwafundisha watu kwenye groups, kufanya mahojiano na mimi kuhusu vipengele kadhaa, kuwa tayari kulipia ili upate huduma zangu, kuthamini huduma yangu ya ushauri pamoja na kukubali kufanyiwa usimamizi na mimi chini ...

JINSI YA KUTUMIA KANUNI YA VISACO KUFANIKISHA MALENGO YAKO YA KIFEDHA!

Kila kitu hapa duniani huendeshwa na kanuni! Na ili mafanikio yapatikane kuhusu kitu hicho utatakiwa kufanya kama vile kanuni inavyokutaka! Uzuri ni kwamba kanuni hufanya kazi kwa mtu yeyote yule na akiwa mahali popote pale! Habari njema nyingine ni kwamba kanuni hazina upendeleo bali humpa kila mtu matokeo sawa sawa na alivyotumia kanuni hiyo! Hio ni sawa na kusema endapo utafanya kile kanuni inakutaka ufanye, utapata matokeo Mazuri, na endapo utafanya kinyume na kanuni yako utapata matokeo mabaya! Hivyo basi ili ufanikiwe katika kuweka malengo ya kifedha, unatakiwa utumie kanuni ifuatayo:- Kanuni ya VISACO ni kifupisho cha maneno matatu ambayo ni: vision, sacrifice na consistence. VI= VISION SA= SACRIFICE CO= CONSISTENCE. wengi wetu huwa tunashindwa kufanikiwa katika mambo yetu kutokana na kushindwa kutumia kanuni hii! Unatakiwa kujua kwamba kuna uwezekano wa kufanikiwa katika jambo lolote lile endapo utatumia kanuni hii! Mambo MATATU kuhusu kanuni hii ya visaco... 1. Vision Maono ni...

Je Ushawahi Kujiuliza Juu Ya Haya?

Kwanini mtu mmoja ana furaha ilihali mwingine ana huzuni?  Kwanini mtu mmoja anapona ugonjwa ambao unasadikika hauwezi kuponywa ilihali mwingine haponi?  Kwanini mtu mmoja ana hofu, wasiwasi, hana amani, hana tumaini ilihali mtu mwingine ana furaha, amani na matumaini? Kwanini mtu mmoja anafanikiwa katika jambo Fulani ilihali mtu mwingine anashindwa kufanikiwa katika jambo hilo? Kwanini mtu mmoja anafanikiwa kujibiwa katika sala juu ya jambo Fulani ilihali mwingine anashindwa kujibiwa katika jambo hilo? Kwanini watu wengi wanaosali sana hupitia mitihani, mateso magumu akilini mwao na maishani mwao mwote? Je, kuna majibu yoyote juu ya haya? …muda siyo mrefu utaenda kuujua ukweli.  Yohana 8:32 “tena mtaifahamu kweli, na hiyo kweli itawaweka huru”. Huenda ukawa unapitia nyakati ngumu sana kiasi kwamba umeshakata tamaa na huna tumaini lolote lile… Na, huenda unapitia hali ngumu kama alivyopitia mwandishi wa  Zaburi 6:6, ambapo Neno la Mungu linasema; “Nimechoka kwa kuugu...

JINSI YA KUTENGENEZA UTAJIRI... HATUA YA 2,3,&4

2. Gundua soko lako... Ukishagundua uwezo wako lazima ujue soko linalohitaji kile ulichinacho. Unatakiwa kujua kwamba kipaji chako ni kwa ajili ya watu wengine. Ukweli ni kwamba tunaishi kwa ajili ya watu wengine. Mbali na hilo unatakiwa kujua kwamba siyo kila mtu atahitaji kipaji chako au uwezo wako! Kuna wengine hawatahitaji kabisa chochote kile kutoka kwako, hata usiumie kwa maana hata wao nao wanahitaji kitu kutoka kwa watu wengine. Kutokana na hilo unahitaji kugundua soko lako liko wapi ili uweze kuuza huduma yako au bidhaa zako. Kugundua soko lako lilipo kunahusisha vitu kama vile: kuwadokeza wateja wako ni wepi? Jinsia yao ni ipi, umri wao ni upi, hadhi ya maisha yao ni ipi, ikiwa ni pamoja nae neo wanalopatikana. Ndugu siyo kila mtu anahitaji kipaji chako au uwezo wako, kwa hiyo kugundua uwezo wako siyo kigezo cha kufanikiwa kutengeneza utajiri huo bali lazima uandae orodha ya watu watakaonufaika na uwezo wako. Kumbuka mtandao wa watu ulionao ndiyo unapima utajiri wako. Kwa kus...

You can't get something for nothing...

Image
Hi there my friend! Emmanuel Samuel here! I have the abundance of exciting news for you.. What I am asking from you is your undivided attention... And I'm pleasing you to pack your property wherever you are, then travel with me through reading this wonderful publication ever published! First of all you have to know that, you can't be a goal getter unless you becomes a goal setter... You may be asking your self what does it mean by the way?  The answer is very simple, what I meant is this; if you want to achieve any goal in your life, the first thing that you have to do, is for you to set some goals concerning what you really want to accomplish in your life... My friend you need to set goals in your life so as to be successful, the naked Truth is that, success is not an accident... Dear reader all successful people have achieved great accomplishments in their life because they started setting goals first!  You too if you want success in your life, you have to seat d...

Jinsi Ya kutengeneza Utajiri

Image
“Yule ambaye hamfundishi mtoto wake jinsi ya kufanya biashara ni sawa na anamfundisha kuwa mwizi” “Hakuna mtu atakayekufanya ushindwe pasipo ruhusa yako mwenyewe” Wadau walikuja na msemo usemi usemao; “Kushindwa kupanga ni sawa na kupanga kushindwa”. Hii ni kwa sababu kufeli huja kama matokeo ya moja kwa moja kwa mtu asiye na mipango maishani.  Ukweli ni kwamba hakuna mtu ambaye hupanga kushindwa, bali kuna mtu ambaye hupanga kwanza ili afanikiwe! Hata hivyo, katika dunia hii tuliyonayo sasa kila mtu ana ndoto za kuwa Tajiri na ndoto za kuufikia uhuru wa kifedha, lakini ni watu wachache tu kati ya hao wengi ambao wanajua jinsi ya kutengeneza utajiri ili wafikie hatua ya uhuru wa kifedha. Hata hivyo, katika uumbaji wa kitu chochote hapa duniani, huhitajika kwanza malighafi zitakazohitajika kwenye uumbaji huo pamoja na michakato kadha wa kadha itakayopelekea uumbwaji huo uwe halisi. Kwa kusema hivyo, hata utajiri ni sawa na uumbaji mpya. Hii ni kwa sababu mtu unatakiwa uu...

SIFA KUU ZA MALENGO YA KIFEDHA...

Image
Siyo kila jambo linalowekwa, linaloazimiwa au linalopangwa kufanyika hapo baadae linafaa kuitwa lengo! Ili Lengo lolote lile liweze kuitwa lengo lazima liweze kuwa na sifa hizi zifuatazo! NB: haijalishi litakuwa ni lengo la kifedha, kiafya, kimaisha au lengo lolote lile endapo litakosa sifa hisi basi hilo halitakuwa lengo bali litakuwa ni tamanio tu!    1. Malengo ya kifedha lazima yawe mahususi... Ili lengo la kifedha lihesabike kama lengo lazima liwe mahususi! Hii inamaanisha kuwa kile kiasi cha fedha kinachoazimiwa lazima kielezwe kwa uwazi! Epuka kusema nataka kufanikiwa tu kifedha, sema unataka kufanikiwa kwa Kiasi gani. Unatakiwa kujua kwamba sababu kubwa wengi huwa hatufanikiwi katika maisha ni kwamba hatujaweka wazi kile tunachotaka tukikamilishe! Ndugu Unapaswa uepuke matarajio yenye ujumla bali kuwa na matarajio yenye ubayana. Kwa mfano ninaazimia kufikia mwezi wa 12 mwaka huu 2024 niweze kuweka akiba ya shilingi 1,000,000/= NB hii siyo motivation bali ni...

HATUA KUU ZA KUPANGA NA KUTIMIZA MALENGO YA KIFEDHA...

Image
Hakuna jambo ambalo hutokea pasipo kuanza ngazi fulani hadi kufikia ngazi fulani! Na ndiyo maana hata ukuaji wa mtoto huanza hatua ndogo zaidi na kwenda hatua ya juu zaidi! Na, endapo itatokea kuna hatua imerukwa basi kutakuwa kuna shida ya ukuaji wa mtoto husika! Kwa kusema hivyo ili ufanikiwe katika kuazimia na kufanikisha malengo ya kifedha unahitaji kuyapanga malengo yako hatua kwa hatua! Unatakiwa kujua kwamba, hakuna jambo ambalo huwa halitokei pasipo kupitishwa kwenye hatua fulani! Hii inamaanisha kwamba ili upate matokeo mazuri ya mipango yako ya kifedha ni lazima uzingatie hatua zifuatazo:- 1. Andika Kiasi cha Fedha Unachokitaka Kukipata. Wengi wanajua wanachokitaka lakini ni wachache tu ndio wanaojua kiasi wanachokitaka kutoka kwenye kile wanachokitaka!  Ukweli ni kwamba moja ya sababu kubwa ambayo imetufanya watu wengi tushindwe kufanikiwa kifedha ni kwa sababu hakuna kiasi cha fedha ambacho tumelenga kukipata.. Unatakiwa kujua kwamba, kwenye maisha usipojua ...

JINSI YA KUFANIKISHA LENGO LA KIFEDHA KWA AJILI YA JAMBO FULANI ILI KUEPUKA MADENI...

Image
Siyo kila njia unayotumia kufanya jambo fulani ni njia sahihi! Na endapo hutatumia njia sahihi huwezi huwezi ukapata matokeo sahihi vilevile! Kwa kusema hivyo unatakiwa utumie kanuni hizi mbili ili kuepuka kuingia kwenye madeni pamoja na kufanikiwa kifedha! 1. Angalia kiasi cha fedha kinachohitajika. Ni lazima ujue ni kiasi gani cha fedha kinachohitajika kwa ajili ya kufanikisha lengo lako! Mara baada ya kujua ni kiasi gani kinachohitajika, angalia pato lako huku ukihusisha na muda uliobaki ili kiasi hicho kikamilike! Baada ya hapo amua kutenga kiasi fulani cha pesa kila baada ya muda Fulani au kila siku. Mpaka muda uliopanga kufanikisha lengo lako kufika utakuwa tayari una kiasi hicho mkononi mwako!  Kwa mfano tuchukulie umepanga kufikia mwezi wa 12 mwaka huu 2024 uwe umefanikiwa kuweka angalau 100, 0000,000/= kwa ajili ya mtaji wa kufungua biashara yako! Unachotakiwa kujiuliza ni hiki; je, umebaki muda gani ufike mwezi wa 12? Ukishapataa jibu sasa amua kutenga kiasi f...

FAIDA KUU ZA KUWA NA MALENGO YA KIFEDHA...

Image
Hivi unafahamu kwamba huwezi ukafanikiwa katika jambo fulani kama hujaazimia kulifanikisha jambo hilo? Hata hivyo kabla hujafanya kitu chochote tafakari mambo haya haya: 1. Faida za kufanya kitu hicho 2. Hasara za kutokufanya kitu hicho. Zifuatazo ni faida kadhaa za kuwa na malengo ya kifedha! 1. Malengo ya kifedha yanakufanya usiangalie muda uliotumia kufanya kazi bali matokeo uliyoyapata ndani ndani ya muda uliofanywa kazi! Hii inamaanisha kwamba ukiwa na lengo hutokuwa bize kuangalia muda unaotumia bali utakuwa unaangalia umefikia wapi kwenye lengo lako... Pia unatakiwa kujua kwamba watu waliofanikiwa sana kifedha siyo watumwa wa muda bali ni watumwa wa malengo. 2. Malengo ya kifedha yatakufanya uwe na nidhamu ya fedha. Huwezi ukatumia pesa hovyo wakati umelenga kutengeneza milioni 100 mwaka huu. Kwa mantiki hiyo malengo ya kifedha yatakufanya uwe na nidhamu ya fedha.  Kutokana na hilo, utajikuta ukiheshimu kila kiasi cha fedha utakachoingiza haijalishi ni kiasi gani...

Kama Unahitaji Fedha Nitakuonesha Mahali Fedha ilipo....

Image
Habari yako mpenzi msomaji, karibu kwenye mwendelezo wa somo letu linaloangazia kuhusu maeneo kumi ambayo fedha Imejificha... Mpaka sasa tumeangalia maeneo sita!  Kwa leo utaenda kuoneshwa maeneo mengine ambayo fedha Imejificha kama ifuatavyo:- 7. Fedha imejificha kwenye maono Maono ni kuwa na picha kamili juu ya jambo Fulani lijalo.  Kwa kusema hivyo linapokuja suala la fedha kila palipo na maono makubwa kuhusu fedha pana mafanikio ya kifedha, na pale ambapo hapana maono kuhusu fedha hapatakuwa na mafanikio ya kifedha. Unatakiwa kujua kwamba maono huweza kuvuta matukio mazuri katika maisha, na hii ni kwa sababu yale mambo ambayo mtu anakuwa kaona akilini mwake ndiyo anayoyavuta na kuyafanya yawe sehemu ya maisha yake.  Kumbuka unapata kwenye maisha kile unachokitengeneza na kukiona akilini mwako.  Na ndiyo maana kanuni ya msawazo wa akili inasema; “kile unachokipata kwenye maisha ni uakisi wa kile unachokiona kwenye akili zako” Bila shaka hapo ulipo una ...