Jinsi Ambavyo Mtizamo Wa Kijamii Hupelekea Wanaume Waendekeze Ngono....
Vile jamii inavyomuona na kumchukulia mwanaume ndivyo inavyomfanya awe hivyo. Unatakiwa kujua kwamba huwa hauoni kitu kama kilivyo, bali huwa unakiona kitu kutokana na wewe ulivyo na jinsi ulivyoaminishwa kuhusu kitu hicho. Na ifahamikie kuwa, utaonesha mwitikio fulani kuhusu kitu hicho kutokana na fikra ulizonazo pamoja na Imani uliyonayo kuhusu kitu hicho. Na hii ndiyo sababu kubwa inawafanya wanawake wengi wa leo wasiwaamini kabisa wanaume kuwa wanaweza kutulia na mwanamke mmoja. Kwa sababu hiki ni kitu kilichomo ndani ya fahamu zao, na siyo rahisi kuweza kukitoa kwa sababu hicho ndicho wanachokijua na ndicho wanachokiamini! Kwa mfano jamii inamuona mwanaume kama mtu anayetakiwa; atunukiwe ngono kila anapohitaji haijalishi anahitaji kwa nani, mtu ambaye hawezi akakaa miezi mitatu bila kukutana na mwanamke, (na endapo itatokea hivyo anaweza kuwa chizi). Mtu ambaye huwa hatosheki kimapenzi, mtu ambaye ni kawaida kuwa na wanawake wengi, na mengine mengi kama hayo...