Posts

Showing posts from August, 2025

Maumivu ni Sehemu ya Safari ya Maisha

Image
Maisha ni safari yenye milima na mabonde. Kuna nyakati za furaha na nyakati za maumivu makali ambayo kila mmoja wetu hupitia. Maumivu yapo kwenye maisha ili kukupa funzo, ili siku moja uthamini kile ambacho kiliwahi kukuumiza mara baada ya kukipata.  Kwa maana fupi tunaweza kusema: kuumizwa kunaweza kuwa ufunguo wa kukupeleka kwenye furaha, kama utaruhusu maumivu yakufundishe. Lakini ieleweke vyema kwamba si kila maumivu yanakupeleka kwenye furaha. Unapaswa kujua: si kila kinachokuumiza kina thamani ya baadaye. Usijidanganye kuyatukuza yote, kwa sababu siyo yote ni ya kujenga. Kila mmoja wetu hubeba maumivu ya ndani—ya kifamilia, kikazi, kimapenzi, kifedha, kielimu, au hata ya kitaifa.  Mimi ninayeandika haya pia hupitia maumivu makali nyakati fulani. Lakini ukweli ni huu: *tatizo siyo maumivu yenyewe, bali ni namna unavyoitikia.* Ukiwa kwenye kipindi kigumu, jiulize maswali haya muhimu: 1. *Chanzo chake ni nini?* – Je, ni wewe mwenyewe, mzazi, ndugu, mwenzi, au ha...

Dunia ni Halisi; Ila Kuna Watu Waliovuruga Mfumo wa Dunia Kwa Lengo la Kuwatawala Wengine...

Image
Hapo Kale kabla Mimi na wewe hatujazaliwa. Wapo watu wachache sana duniani waliokuja na lengo moja kali: kuvuruga mfumo wa dunia ili kutawala watu! Sihofii kuhusu ukubwa wa mtu, wala mabavu yake, lakini si kila mtu mkubwa anajitambua kweli. Kuna wakubwa waliopotea, akili zao zimefungwa, na hawajui hata nafsi zao! Kujielewa ni msingi wa kuishi kwa utu. Kutokujielewa ni chanzo kikubwa cha mivurugano, migogoro, na maafa yanayotukumba leo hii! Mwafrika wa leo anajivunia sana elimu ya Magharibi, lakini elimu hii ni ya kinyonge, ni kifungo cha akili kinachomfanya mtu awe mfanyakazi tu wa mfumo, si mbunifu wala mkombozi wa jamii. Elimu hii imemfunga mtu kwa kumsahaulisha rasilimali zake za aina yake na kumfanya awe sehemu ya mfumo unaoharibu maisha ya wengi kwa kufanya mambo yasiyo sahihi huku akiwacha wafuasi wake kwenye taabu. Mwafrika wa leo anakumbatia imani potofu na mitazamo inayojenga chuki na uadui kwa sababu anaamini ni njia pekee ya kumlinda mwenye mali au mamlaka, hata ...

Kadri Unavyoongezeka Thamani, Ndivyo Fedha Zinavyokufuata — Je, Umejiwekea Thamani Yoyote?

Image
Siku zinavyozidi kwenda mbele, kila mtu anakaribia uzee. Hakuna anayerudi kuwa mtoto tena. Kifo kinakuja polepole, bila tahadhari — lakini kinakuja!  Swali ni, thamani yako inaendelea kupanda au kushuka? Je, wewe  wa jana ulikuwa na thamani gani? Na wewe wa leo, uko wapi kithamani?  Je, watu wanaokutegemea wanaongezeka au wanapungua? Je, watu wanakuzungumziaje? Je, katika kuishi KWAKO unavuta watu wa thamani au unapoteza nafasi zao?  Fedha inafuata thamani — ni sheria isiyoandikwa ya maisha. Je, una thamani ya kutosha kuvuta fedha kwako? Nakumbuka mwaka 2022, nilipokuwepo kwenye hali ngumu. Sikuwa mtu wa thamani, sikuweza kutengeneza fedha, na maisha yalikuwa ya kawaida tu—hakuna mwangaza wala matumaini. Lakini siku moja, nikajitazama kwenye kioo na kusema, "Hili hali haitatokea bila sababu kubwa." Lazima nifanye jambo. Niliamua kuchukua hatua.  Nikaanza kujifunza, kuwekeza muda, nguvu, na akili zangu kwenye kujenga thamani yangu binafsi. Siku za mwa...