Jinsi Ya Kupata Matokeo Unayoyataka... Mbinu Ya 2&3
2. Tafuta Njia Zitakazokusaidia Ili Ufanikiwe Kupata Kile Unachokitaka... Kujua unachokitaka siyo kigezo cha kukipata, bali ni lazima uweke wazi njia zitakazokusaidia ili upate hicho unachokitaka. Rafiki, hakuna matokeo ambayo hujitengeneza yenyewe pasipo njia zitakazochochea matokeo hayo… Na, ndiyo maana hata katika hesabu huwezi kupata jibu pasipo kutumia formula/njia fulani. Hebu jaribu tu kuvuta picha utapateje jibu (matokeo) pasipo kutumia njia fulani itakayokuletea jibu hilo (matokeo hayo)? Hii ni sawa na kusema, katika kila utakachokitaka kuna njia utakayopsawa uitumie ili ikusaidie uweze kukipata kitu hicho! Na, ndiyo maana niko hapa kukukumbusha kuwa ukishajua unachotaka lazima udokeze mbinu utakayopasawa uitumie ili ukipate! Kwa mfano katika hoja ya kwanza nilisema kwamba ninachokitaka ni “kuongeza pato langu la mwezi lifikie 300,000/=” kwa mantiki hiyo itabidi niweze kuja na njia ambazo zitanisaidia ili niweze kuyapata matokeo hayo ninayoyataka. ...