Kama Unataka Kujua Ni Kipi Unapaswa Ufanye Mara Baada Ya Kugundua Uwezo Wako Soma Hii...
Watu wengi wanaujua vyema uwezo wao lakini hawajui jinsi gani wanaweza wakatumia uwezo huo ili uwanufaishe! Kujua uwezo wako ni kitu kingine na kutumia uwezo wako ili ukunufaishe ni kitu kingine vilevile! Ukweli ni kwamba, ukishagundua uwezo wako jambo la kwanza unalopaswa kufanya ni kuandaa huduma au bidhaa Inayotokana na uwezo huo! Unatakiwa kujua kwamba, moja ya eneo ambalo fedha nyingi imejificha ni eneo la bidhaa au huduma. Kwa kusema hivyo ni wale tu watakaokuwa wanatoa huduma Fulani au watakaokuwa wanauza bidhaa Fulani ndiyo watakaokuwa wanatengeneza fedha! Wewe mwenyewe unaweza kufanya tathmini binafsi ni kwa namna gani umekuwa ukitumia fedha zako kwa ajili ya kupata huduma au bidhaa Fulani zinazozalishwa na kutengenezwa na watu wengine! Na umetumia fedha zako ili kupata huduma au bidhaa Fulani kwa sababu kuna thamani Fulani ambazo zimebebwa kwenye bidhaa hizo au huduma hizo! Kwa kusema hivyo hata wewe huna budi uandae bidhaa au huduma yenye thamani...