Posts

Showing posts from November, 2024

jinsi Ya Kuwa Mtu Usiyesimamishwa Na Chochote Kile

Image
Mbinu Ya Sita Yapuuzie Maoni Hasi... Kila mahali ulipo fahamu kwamba, umezungukwa vyanzo mbalimbali vinavyotoa maoni na mapendekezo kuhusu maisha yako.  Kwa hiyo basi endapo maoni hayo yatakuwa ni maoni hasi utajikuta ukisimamishwa na kushindwa kukamilisha harakati zako.  Kwa kusema hivyo kama unataka kuwa aina ya yule mtu ambaye hawezi kusimamishwa huna budi kupuuzia mapendekezo hasi. Unatakiwa kujua kwamba maoni hasi yapo kila mahali kuanzia: nyumbani, ofisini, shuleni, mtaani, makanisani pamoja na misikitini.  Hata hivyo, ikiwa hautakuwa na uwezo wa kuyakataa na kuyapuuzia, utajikuta ukisimamishwa hali itakayosababisha anguko lako.  Ili kuepuka kusimamishwa, ni muhimu kujifunza jinsi ya kuyakataa mapendekezo hasi na kuunda mtazamo chanya wa maisha. Hii itakusaidia kuongeza kiwango chako cha bidii na juhudi katika mambo yako!   Mbali na hilo endapo utachunguza kwa undani, utagundua kwamba watu wa karibu ambao tunawaamini ndio wamekuwa wakituam...

Jinsi Ya Kuwa Mtu Usiyesimamishwa Na Chochote Kile..

Image
Mbinu Ya Tano Jifunze Kuamua Vyema... Umefika hapo ulipo, umekuwa hivyo ulivyo, unatengeneza hicho kipato unachotengeneza, unafanya hiyo kazi unayoifanya, unaishi hapo unapoishi, unaishi maisha ya hadhi hiyo unayoishi, umekuwa na mwenzi huyo uliyonaye na kila kila unachokifanya katika maisha yako unakifanya kwa sababu umeamua kukifanya. Ukweli ni kwamba, huwa unafanya maamuzi ukiwa huru, lakini mara baada ya kuamua unageuka na kuwa mfungwa na mtumwa wa maamuzi yako.   Kwa hivi huna budi kufanya maamuzi ambayo hayatakufanya usimame bali fanya yale maamuzi ambayo yatakufanya uwe mtu wa kusonga mbele tu. Unatakiwa ufanye maamuzi ambayo kesho yako itakuja kukushukuru kwa kile ulichokiamua jana. Unapokuwa ni mtu wa kufanya maamuzi sahihi maana yake utakuwa ni yule ambaye huwezi ukasimamishwa kwa sababu ya usahihi wa maamuzi yako kunyoosha mapito yako.  Kwa mfano mara baada ya kuamini kuwa ninaweza kuwa yoyote yule na nikachagua yule ninayetaka niwe.  Niliamua kutok...

jinsi Ya Kuwa Mtu Usiyesimamishwa Na Chochote Kile!

Image
Mbinu Ya Nne   Amini Kuwa Unaweza Kuwa Yeyote Yule .. Dunia ni wewe unachotaka kuwa. Na Dunia huwa haimfungi mtu yeyote yule, badala yake sasa mawazo ya mtu huyo ndiyo humfunga na kumsababishia  ajiwekee ukomo juu ya pale anapoweza kufika kimaisha. Unatakiwa kujua kwamba duniani hakuna vikwazo halisi zaidi ya vile vikwazo unavyojiwekea mwenyewe kutokana na mtindo wako wa kufikiri.  Kwa hiyo umekuwa hivyo ulivyo kwa sababu umeamua uwe hivyo, au kuna mifumo Fulani hivi ambayo imekutengeneza na kusababisha uwe hivyo ulivyo na wewe hukuwa na chaguo jingine.  Na unaweza ukawa huyu ama yule kesho yako endapo utaamua kuwa mtu mwingine kabisa ambaye hujawahi kuwa. Habari njema ni kwamba hakuna wa kukusimamisha zaidi ya wewe mwenye unayeweza ukajisimamisha kutokana na mtindo wako wa kufikiri. Yamkini umechoshwa na utambulisho bandia unaotokana na kozi uliyosomea au kazi unayoifanya na pengine labda unataka ukate minyororo inayokuunganisha huko ili uwe mtu mwingine...

Jinsi Ya Kuwa Mtu Usiyesimamishwa Na Chochote Kile...

Image
Mbinu Ya Tatu   Jiboreshe Kila Leo  Kwa mujibu wa tafiti zilizofanyika zimeonesha kuwa, karibu kila ujuzi huw eza kupitwa na wakati kila baada ya miaka miwili na nusu hadi miaka mitatu.  Kwa hivi kujua kitu Fulani siyo kigezo cha kufanikiwa kimaisha, bali kuendelea kujiboresha ndiyo mbinu itakayokusaidia uwe mtu usiyesimamishwa katika kufanya kitu Hicho. Kwa sababu hata kama mabadiliko yatatokea wewe pia utabadilika kuendena na mabadiliko hayo, na hakuna kitu ambacho hubadilika haraka kama mabadiliko yenyewe. Rafiki unapojiboresha kila leo inamaanisha kwamba, utakuwa unapata mbinu mpya za kufanya mambo yako. Kwa hiyo basi utakuwa mtu muafaka muda wote! Kwa mfano sikuweza kujua kwamba kuna kitu kinaitwa online coaching, lakini mara baada ya kujifunza nimeweza kutoa huduma hii na mpaka sasa huwa nasimamia watu waliopo nje na eneo nililopo! Na kuna baadhi ya wanafunzi wangu ambao huwa tunamaliza nao huduma nzima ya coaching bila kuonana kabisa!  Nakumbuka ma...

Jinsi Ya Kuwa Mtu Usiyesimamishwa Na Chochote Kile... Mbinu Ya Pili

Image
2. Daima Fikiri Kuhusu Malengo Yako Unapokuwa umeweka lengo kwa uwazi maana yake unakuwa unajua kile unachokitaka.  Unapojua kile unachokitaka maana yake hutaweza kuvipa nafasi vile usivyovitaka vikusimamishe katika mapambano yako utakayokuwa unayafanya ili kufanikisha malengo yako.  Unatakiwa uweke lengo lako kwa uwazi ili upate hamasa na shauku ya kulifikia. Kwa sababu wakati mwingine si kwamba watu wanakosa hamasa kuhusu maisha yao, bali wamekosa kuweka wazi kile wanachokitaka maishani mwao.  Kwa hiyo hakikisha unaazimia lengo lako katika hali ya uwazi! Kwa tafsiri nyepesi lengo ni; mpango, tarajio, dhamira, nia au kusudio la mtu ndani ya kipindi fulani cha muda.  Ili tupate picha kamili kuhusu lengo lazima tufafanue masuala yafuatayo.  Lengo Ni Nini? Ni kile unachokusudia kufanikisha ndani ya muda fulani, hii inamaanisha hicho kitu kiwe dhahiri kikiwa kina viashiria ambavyo vitajidhihirisha ili tujue kuwa lengo hilo limetimia. Kwa mfano ninaweza ...

Jinsi Ya Kuwa Mtu Usiyesimamishwa Na Chochote Kile...

Image
Bila shaka ulishawahi kukutana na wale watu ambao hufanya baadhi ya mambo halafu wanaishia njiani kutokana na sababu mbalimbali.  Ukweli ni kwamba mbali na watu hawa kuthubutu kuchukua hatua maishani mwao, matokeo yake wamejikuta wakishindwa kuzifikia hatima zao nzuri!  Unatakiwa kujua kwamba baadhi yao wameishia njiani siyo kwamba wanatakiwa kuishia njiani, bali ni kwa sababu nyuma ya pazia kuna sababu ambazo zimesabababisha washindwe kukamilisha safari zao walizozianzisha!  Na endapo itatokea hivyo watu hawa hujikuta wakishindwa kufanikiwa maishani mwao, kwa hivi badala ya kwenda mbele hujikuta wakirudi nyuma. Mara nyingi hushindwa kuzifikia hatima zao kwa sababu ya kukosa hamasa, shauku, nguvu na kiu ya kufika huko. Ukweli ni kwamba, hali hii husababishwa na watu hao kutokuweka kwa uwazi kile wanachokitaka kukikamilisha katika maisha yao.  Huenda hata wewe ni miongoni mwa wale watu ambao wamekuwa wakianzisha vitu vipya na kutokuvikamilisha, na pangine ...