KUNA WATU WANACHAMBUA… NA KUNA WATU WANACHANGANUA
Mara nyingi nimekuwa nikisema: Kuna watu wanajua wanavyosema… na kuna watu hawajui. Na kuna watu wanachambua, na kuna watu wanachanganua. Mchambuzi ataelezea jambo kama lilivyo. Lakini mchanganuzi… atalipa jambo MAANA. Na ukweli ni huu: 👉 Wengi wanaishia kuchambua. Chukulia mfano wa neno “Mungu”. Wengi wanachambua tu—wanajua kulitamka, kulijadili, hata kulitetea. Lakini hawafiki kwenye kina. Mchanganuzi atakuambia: 👉 Jina “Mungu” halipo kugawa watu—lipo kuwaunganisha kwa sababu ndiyo hoja kubwa zaidi kuliko zote. Lakini kwa sababu ya kuchambua bila kuchanganua… kile kilichotakiwa kuunganisha, kimekuwa sababu ya kugawanyika. Unaona? Leo nikiwa mahali, mtu akaniuliza: “Wachumba wapo huko uliko?” Nikasema: “Wapo.” Akasema: “Mimi wananikataa kwa sababu nimeokoka, wao ni madhehebu mengine.” Nikamwambia: 👉 “Mimi Biblia nimesoma yote. Niambie dhehebu lililoandikwa mule.” Akakosa jibu. Sikumwambia aache imani. Nilimwambia ukweli mmoja tu: 👉 Endelea kuchambua… lakini ujue bado h...