Huwezi Kuishinda Hofu Mpaka Usome Kwanza Hii...
Habari yako rafiki? Ni matumaini yangu u mzima wa afya! Ashukuriwe Mungu kwa neema zake nyingi! Hatimaye leo hii somo letu la Mbinu tisa za kuikabili hofu linaenda kutamatika kwa kuangazia hoja tatu zizokuwa zimebaki! Karibu uweze kupata mbinu hizi tatu za mwisho zikusaidie katika Kuikabili Hofu... 7. Badilisha Mitizamo Yako… Siyo kila anayeona, anaona, na siye kila anayesikia, anasikia. Kuna wengine wanaona lakini ni vipofu, na kuna wengine wanasikia lakini ni viziwi. Ninasema hivi kwa sababu watu wengi huwa hatuoni vitu kwa namna ile inavyopaswa iwe, bali tunaona vitu kutegemeana na sisi tulivyo… Ukweli ni kwamba tupo watu wengi ambao tunaona mambo kwa kulinganisha na jinsi sisi wenyewe tulivyo, kutokana na hilo tutajikuta tukijitengnezea milima na mwisho wa siku tunaanza kuhofia mambo hayo! Mwanzo 1:26 Neno la Mungu linasema; Mungu akasema, “Na tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu”… Chukua neno “kwa mfano wetu”, halafu weka akilini mwako! Iko ...