Usimtendee Mwenzio Yale Ambayo Haupo Tayari Kutendewa... The Golden rule
Hivi unafahamu kwamba Moja ya sababu kubwa ambayo imesababisha magumu mengi tunayopitia wanadamu wengi katika nyakati hizi ni kukosekana kwa upendo baina yetu? Laiti kama kila mtu kwa kadri ya jinsia yake angekuwa anamtendea mwenzake yale ambayo hata yeye mwenyewe yupo tayari kutendewa basi hapa duniani ingekuwa ni sehemu salama sana wala kusingekuwa na chuki, hasira, vinyongo pamoja na visirani. Lakini kutokana na kukosena kwa utu na upendo baina yetu ndiyo maana chuki, vinyongo, visirani vimetapakaa sana katika kizazi hiki cha leo. Ukichimba kwa undani utagundua kuwa leo hii wapo majirani ambao hawazungumzi kutokana na chuki, wapo wamafamilia ambao hawana upendo baina yao kutokana na chuki, wapo wanandoa ambao chuki ndiyo imechukua nafasi kubwa zaidi katika maisha yao kana kwamba walioana ili wachukiane na siyo wapendane... Ukweli ni kwamba, haya yote yanatokea kwa sababu tunawatendea wenzetu yale ambayo sisi wenyewe hatupo tayari kutendewa. Hebu jaribu kuvuta picha, unam...