Mambo Matano Unayopaswa Kuyafahamu Kuhusu Muda...
Hivi umewahi kufikiri kwamba muda ni rasilimali unayoweza kuiwekeza kama fedha au mali? Wengi hawalijui hilo. Wamekuwa waumini wa kutumia muda hovyo, bila kutambua kwamba sehemu kubwa ya maisha yao inapotea kupitia muda wanaouharibu. Leo, ngoja nikuoneshe mambo matano ya msingi unayopaswa kuyafahamu kuhusu muda, mambo ambayo yakieleweka vizuri, yanaweza kubadili kabisa namna unavyoishi na kupanga maisha yako. 1. Muda ni Maisha Muda ndicho kipimo halisi cha hadhi ya maisha ya kila MTU. Kutoka siku ulipozaliwa hadi sasa, maisha yako yote ni mkusanyiko wa vipindi vya muda vilivyopita. Hadhi ya maisha yako inahusiana moja kwa moja na namna ulivyotumia muda wako. Wapo watu wenye umri mdogo lakini wamepiga hatua kubwa kimaisha; na wapo wazee ambao miaka imepita bila mafanikio makubwa. Tofauti yao haipo kwenye umri - ipo kwenye *lmatumizi ya muda. Jiulize leo: Kwa muda wote niliouishi, nimefanya nini cha kujivunia? Hadhi ya maisha yangu inaakisi matumizi bora ya muda wangu kw...