Posts

Showing posts from October, 2024

Fahamu Tafsiri KUU MBILI Za Fedha...

Image
Hivi unafahamu kuwa watu wengi wametingwa muda wote kutafuta fedha Lakini hawajui fedha ni nini? Kwa mujibu wa tafiti binafsi nilizozifanya nimebaini kwamba, baadhi ya watu hawafahamu fedha ni nini, hali ambayo imesababisha wakutane na masumbufu mengi katika kuipata na hata kama wakiipata waishie kuipoteza! Ukweli ni kwamba watu wengi wanajua jinsi ya kupata fedha, lakini hawajui jinsi ya kuidhibiti fedha yao isipotee! Hii ni sawa na kusema tunatengeneza fedha kwa kile tunachokijua, na tunapoteza fedha kwa kile tusichokijua! Unatakiwa kujua kwamba jambo hili hutokea likichangiwa na ukosefu wa maana halisi ya fedha miongoni mwa watu wengi! Ikiwa hata wewe, ulikuwa unaamini ya kwamba fedha ni karatasi au sarafu, nataka nikuulize hili; huwa unafanya nini mpaka upate hilo karatasi (noti) au hiyo sarafu unayoiita fedha? Unachopaswa kujua ni kwamba kile ambacho unafanya kabla hujapokea malipo ya noti au ya sarafu basi hicho ndicho fedha yenyewe... Kwa Sababu kile ulichokifanya ki...

Je Na Wewe Ulikuwa Ukifanya Kosa Hili Kwenye Ndoa Yako?

Image
Katika ulimwengu huu mpana na ulio mkubwa sana, wapo watu wengi sana ambao huteseka kwenye eneo la ndoa! Takwimu zimeonesha kwamba, wanaume wengi wamekuwa wakinyimwa haki ya tendo la ndoa na wake zao! Ninaandika hivi kwa sababu huko nyuma nilishawahi kukutana na kesi kama hizi, ijapokuwa nilifanikiwa kuzitatua! Nilijiuliza sana kwanini wanawake hao huamua kuwatesa wanaume zao kiasi hicho?  Ndipo nikagundua kuwa hali hii inachangiwa na ujinga wa kutokujua kile ambacho Mungu kaamuuru kwenye neno lake kuhusu ndoa!  Na ifahamike kwamba ndoa ni taasisi iliyoasisiwa na Mungu mwenyewe! Katika Maisha haya nimegundua kwamba, ili ufanikiwe katika kitu fulani unatakiwa ujue Mungu kasema nini kuhusu hicho kitu, baada ya kujua ndipo sasa unatakiwa ufanye kama vile ambavyo ameamuru! Hata katika haki ya kupeana tendo la ndoa Mungu kashatoa mwongozo unaotakiwa uzingatiwe! Ngoja tuangalie andiko linasemaje, kuhusu hilo... 1 Wakorintho 7:3 “Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hiv...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...

Image
Siku Moja Nilikuwa Nikitafakari Kwa Kina Ni Kipi Hasa Chanzo Halisi Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika?  Na Kwa Vile Unaweza Ukaituma Akili Yako Irudi Miaka Ya Nyuma Huko Ikatalii Ili Ione Baadhi Ya Mambo Yaliyotokea Miaka Hiyo, Basi Nilifanya Hivyo Hatimaye Nikagundua Kuwa Matatizo Mengi Tunayokumbana Nayo Ni Ya Kutengenezwa! Unaweza Ukawa Unajiuliza Tatizo La Kutengenezwa Ni Nini Na Lipoje Hilo? Hili Ni Tatizo Ambalo Mtu Anakumbana Nalo Sasa Lakini Huko Nyuma Kuna Kundi La Watu Ambalo Lilihusika Katika Kulitengeneza Aidha Kwa Kujua Ama Kutokujua. Na Kwa Vile Tatizo Hili Huwa Limetengenezwa Basi Hurithishwa Kutoka Kizazi Kimoja Hadi Kingine Bila Ya Kupatiwa Ufumbuzi. Na Wengi Hulichukulia Kikawaida Sana, Matokeo Yake Hujikuta Wakiishia Kuhalalisha Kwa Kusema; "Tuishi Nalo Tu, Huenda Ndivyo Ambavyo Maisha Yetu Yalipaswa Yawe" Kwa Mfano Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika, Yalitengenezwa Kipindi Cha Miaka Ya Nyuma Sana! Na M...

Je, Unataka Kufahamu kufahamu Tatizo ni Nini, Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...

Image
Tatizo Ni  Hali Yoyote Ile Iliyo Kinyume Na Matarajio.  Kwa Mfano tufanye Ulitarajia upate Furaha Maishani yako yote Lakini ikatokea Ukajikuta Ukikumbana Na Huzuni Zaidi kuliko furaha!  Hii Inamaanisha kwamba Huzuni Ni Tatizo Kwako Kwa Sababu ni Hali ambayo ipo kinyume na kile ulichokitarajia yaani furaha! Ina Maana Kwamba, Badala Ya Kukutana Na Furaha (Matarajio Yako) Umejikuta Ukikutana Na Huzuni Tu (Tatizo)… Hata hivyo Kwa asilimia kubwa wengi wetu huwa tunatamani tuishi maisha mazuri kwa kutengeneza kip ato kikubwa cha fedha (matarajio yetu), Lakini inapotokea tukawa  tunaishi maisha magumu huku t ukitengeneza kipato cha chini linakuwa ni tatizo kwa sababu ni hali iliyo kinyume na matarajio yetu. Na hii ndiyo sababu ambayo imesababisha umaskini uonekane kana kwamba ni tatizo! Au Neno Tatizo linaweza kufafanuliwa kama kitu chochote kile ambacho huibuka kama kikwazo, ambacho husababisha kitu kingine kisitokee au kama kitafanyika kisifanikiwe!  Kwa ...