Hii Ni Kwa Wale Watu Wanaotaka Kubadili Maisha Yao Lakini Hawajaanza Bado…
Hivi unajua kwamba zaidi ya asilimia 80 ya watanzania wanapambana sana katika kubadili maisha yao lakini jitihada zao zinagonga mwamba na kujikuta wakishindwa kupiga hatua kimaisha? Hili ndilo tatizo unalokumbana nalo, kwa maana mbali na kupambana sana huoni matunda yanayotokana na juhudi zako unazozifanya… Yamkini umeajiriwa aidha kwenye taasisi binafsi au serikalini lakini kila ukipokea mshahara wako unaishia kutumika wote. Matokeo yake unabakia kapuku na madeni juu, na huna chanzo kingine cha kukutengenezea mapato, na hata ukijaribu kuweka akiba kidogo kidogo inashindikana kwa sababu kipato chako ni cha chini… Na pengine labda unatamani sana ungebadilisha hata kazi au ungeongezewa mshahara, lakini kila kunapokucha ni afadhali ya jana. Na ndiyo kwanza mambo yanazidi kuwa magumu… Yamkini umefungua hadi biashara yako ili ujikwamue kiuchumi cha ajabu huoni maendeleo yoyote yale mbali na kuwa unafanya mauzo! Huenda ukawa unapitia manyanyaso, dhara...