Je, Unataka Kufahamu Athari Za Mifumo Ya Kutengenezwa Dhidi Ya Maisha Yako? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...
“Usipojijua wewe ni nani na unaweza ukafanya nini mtu mwingine atatumia udhaifu wako kujinufaisha.”-emmanuel king’ung’e Habari yako champion wangu wa nguvu? Bila shaka umeshinda salama kabisa na umekuwa na siku njema na yenye kupendeza! Kwa Siku Ya Leo King Mentorship Program imekuandalia somo linalohusu; "Athari Za Mifumo Ya Kutengenezwa Dhidi Ya Maisha Yako." Ikiwa bado umefungwa kwenye mifumo kandamizi basi soma ujumbe huu ili Ubadili maisha yako! Kumbuka hakuna kuteseka bila taabu, kwa maana hiyo katika makala hii utagundua kwamba, moja ya sababu kubwa ya magumu ambayo watu wengi wanakutana nayo maishani mwao yanatokana na mifumo ya kutengenezwa. Mbali na hilo huenda umeona hapo ulipofikia ndiyo mwisho wako, na huna chaguo lingine zaidi ya kuendelea kuteseka... Hata hivyo sina maana ni wewe msomaji lakini huenda ukawa unafanya juhudi sana, unapambana sana lakini hakuna kizuri unachokipata maishani mwako. Swali unalotakiwa ujiulize ni hili, je malipo mazuri ya ...