Jinsi Ya Kupanga Na Kufanikisha Malengo Yako…
Kitu unachopaswa kujua ni kwamba kuazimia malengo ni kitu kingine na kufanikisha lengo ni kitu kingine. Lengo likiazimiwa haimaanishi kwamba ndiyo limetimia. Hivyo basi ili kufanikisha lango lako hatua zifuatazo ni lazima zizingatiwe kwanza:- ➡️Andika Malengo Yako… Ili kutimiza malengo uliyoyaazimia ni lazima uyaandike kwanza. Unachopaswa kujua ni kwamba ili lengo liitwe lengo sharti ni lazima liandikwe… hii ni kwa sababu lengo ambalo halijaandikwa huwa ni tamanio tu ambalo haliwezi kutimizwa. Unatakiwa uandike kwa sababu akili yako huwa inaingiza taarifa nyingi, kwa mantiki hiyo lengo lisilioandikwa ni rahisi kusahaulika. Hivyo basi ili kutimiza lengo lako ni lazima uliandike na kulisoma kila siku kabla ya kulala na ukishaamka. Mbali na hilo unahitaji kuandika malengo yako kwa sababu kuandika kunakufanya utengeneze kitu Fulani unachoweza kukishika na kukisoma kila unapohitaji kukisoma. Kadhalika unapoamua kuandika lengo lako utajikuta ukiunganishwa na kanu...