Fahamu Jinsi Maendeleo Ya Sayansi Na Teknolojia Yalivyoathiri Namna Watu Wengi Wavyojiona...
Hivi unafahamu kwamba maendeleo ya sayansi na teknolojia yameleta athari nyingi zaidi kuliko faida miongoni mwa watu wengi hasa linapokuja suala la namna wanavyojiona? Unachopaswa kujua ni kwamba kila kilicho na faida hakikosi hasara! Kutokana na ukweli huo huna budi kukubaliana na mimi kwamba maendeleo ya sayansi na teknolojia yamekuja kuathiri sana watu kimtizamo pamoja na hata namna wanavyojiona! kwanini nasema maendeleo haya yamebadilisha watu kimtizamo? Sababu kubwa inayonisukuma niseme hili ni kwa sababu watu wengi wamejikuta wakitumia sayansi na teknolojia kama kioo cha kujitizamia! Ambapo mwisho wa siku wanaishia kujiona wao ni wabaya kimuonekano, (hasa wakihusisha na rangi zao pamoja na muonekano wa maumbile yao) Kutokana na hilo wanaanza kujishushia thamani na kujiona wao kama siyo kitu, pasipo kujua kwamba kioo walichotumia kujitizamia siyo kioo halisi! Kwa mfano maendeleo ya sayansi na teknolojia yamekuja na ugunduzi wa baadhi ya viungo bandia (vinavyopandi...