Jinsi Ambavyo Walimu Wa uongo Hupelekea Watu Wajifunze Yasiyofaa...
Kitaaluma mimi ni mwalimu mtaalamu. Nikiwa kazini kuna wakati wanafunzi huwa wananiita mwalimu! Mwalimu! Nami huwa naitika kwa kusema; “mwalimu wa pekee na wa kweli alikuwa Yesu Kristo” Simaanishi kwamba walimu wengine hawafai lahasha! Tafadhali usinielewe vibaya, walimu wazuri wapo. Hata hivyo uzuri wa mwalimu unapimwa kupitia maarifa anayoyatoa kama yanajenga au yanabomoa. Endapo itatokea mwalimu akawa anatoa mafundisho yanayoharibu, kudidimiza na kubomoa badala ya kujenga basi mwalimu huyo hafai, bali anachokifanya ni uharibifu. Mwalimu huyu anastahili kupewa jina la mwalimu mharibifu na si jina la mwalimu mjenzi kwa sababu anachokifanya ni kuharibu akili za watu! Hawa ndiyo walimu tulionao karne hii, kwa sababu ukichunguza kwa ukaribu utagundua kwamba karibu kila sekta tumezungukwa na walimu, lakini ujinga bado ni mwingi kumbe tatizo siyo ujinga, bali tatizo ni walimu wenyewe kutokana na mafundisho wanayoyatoa! Mtu anapobaki kuwa mjing...