Je Umekuwa Ukikumbwa Na Hofu Maishani Mwako? Hizi hapa Ni Sababu Ambazo Hupelekea Hofu...
Kwa mujibu wa kanuni ya kichocheo na matokeo inadai kwamba, "kila kitu hutokea kutokana na sababu" Hii inamaanisha kwamba, kama hakuna sababu basi hakuna matokeo. Na, hii ni kwa sababu kila matokeo / hali hutokana na kisababishi fulani. .. Hii ni sawa na kusema hauhofii tu kwa sababu unatakiwa uhofu, ila unahofia kwa sababu kuna visababishi vilivyopelekea uweze kuhofu... Ukweli ni kwamba hofu ni kama ugonjwa ambao humfanya mtu awe mahututi, na endapo mtu huyo hatazinduka anaweza akafa katika hali ya unyonge na asifurahie kabisa maisha yake hapa duniani. Zifuatazo ni sababu ambazo hufanya watu wengi wawe na hofu maishani mwao... 5. Kukisa maarifa/Taarifa Sahihi… Hosea 6:4 “…kwa kuwa umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe…" Kama unakuwa kimwili kutokana na kile unachokula, vilevile utakuwa kiakili kutokana na kile unachoulisha ubongo wako. Kukosekana kwa mwamko wa kujifunza kumefanya watu wengi wazidi kuwa na hofu kwa sababu ya kukosa, maarifa pamoja ...