Je Ungependa Kuyajua Maeneo Kumi Ambayo Fedha Imejificha...?
Habari yako rafiki yangu! Ni matumaini yangu u mzima wa afya! Karibu kwenye mwendelezo wa somo letu linaloangazia kuhusu maeneo kumi ambayo fedha Imejificha! Kama unakumbuka vizuri makala iliyopita ilidokeza maeneo matatu, makala hii ni mwendelezo wa makala iliyopita! Sasa unaweza kusonga nayo kwa kuyapitia maeneo mengine matatu kati ya kumi ambayo fedha imejificha kama ifuatavyo:- 4. Fedha imejificha kwenye fursa Tatizo la mtu moja ni fursa ya mtu mwingine kutengeneza fedha, na ndiyo maana ikitokea mtu amekuja kwangu kuuliza jambo kuhusu tatizo fulani, huwa nalichukulia tatizo lake kama fursa ya kutengeneza fedha. Kutokana na hilo huwa nasimama kama mtu wa kutatua tatizo lake, na kama itashindikana huwa nasimama kama dalali wa kumuunganisha na mtu mwingine atakayemtatulia tatizo lake kwa kamisheni! Kumbuka awali tuliona kwamba matatizo ya watu ni fursa za kutengeneza fedha! Hata hivyo wapo watu ambao hudhani kufanikiwa kifedha ni bahati, kitu ambacho siyo ...