Ni Kweli Unatafuta Mwenzi, Wenzi Wako Wengi, Je Umeandaa Vigezo Gani Ili Umpate Mwenzi Sahihi?
Habari yako champion wangu wa nguvu? Ni matumaini yangu u mzima wa afya, kwa upande wangu namshukuru Mungu niko salama usalimini! Kwa Siku ya leo King Mentorship Program imekuandalia somo linalohusu; "Jinsi Ya Kumpata Mwenzi Sahihi Kwa Kutumia Vigezo Ulivyoviandaa." Kama Unataka umpate mwenzi atakayekufaa kwa kadri ya mahitaji yako, basi tumia MBINU hii, na kama unaye tayari huna budi kusoma Makala hii mpaka mwisho kuna kitu kipya utajifunza! Hivi unafahamu kwamba, watu wengi hushindwa kupata wenzi sahihi katika mahusiano yao kwa kutokuandaa vigezo vya wenzi wanaowataka? Hata katika maisha yetu ya kawaida, huwezi ukakipata kitu ambacho hujaandaa mazingira ya upatikanaji wake... Na ndiyo maana hata kwenye tangazo linalomhitaji mfanyakazi fulani, huwekwa sifa na vigezo vya mtu anayestahili kufanya maombi kwa ajili ya kazi hiyo! Rafiki, unatakiwa kujua kwamba vigezo Pamoja na sifa hizo, huwa haviwekwi ili kurefusha au kuremba tangazo, bali huwekwa ili kuisaidia ofi...