Posts

Showing posts from September, 2023

Njia 4 Tahisi Za Kupanga Bajeti Yako Ili Ufanikiwe Kifedha...

Image
Hivi unajua asilimia kubwa ya watu hawana utaratibu wa kupangilia matumizi ya fedha zao hali ambayo huwafanya washindwe kufanikiwa kifedha huku wakilia hali ngumu muda wote?  Huenda hata wewe umekuwa ni yule mtu ambaye unatengeneza fedha kila leo lakini huna matumizi yanayoeleweka hali ambayo inapelekea upotevu  wa fedha zako!  Rafiki unatakiwa kujua kwamba, usipojua namna ya kupangilia matumizi ya fedha zako, basi fedha zako zitakupangia uzitumiaje!  Na ndiyo maana kuna watu wakishapata fedha, huwa wanapatwa na hali ya mchecheto (fedha zinawawasha), hali ambayo huwafanya washindwe kutawala matumizi mazuri ya fedha zao, matokeo yake hujikuta wakifanya manunuzi kwa shinikizo linalotokana na fedha walizozitengeneza na siyo vile wao wanavyotaka kutumia fedha zao! Ubaya huja pale ambapo unakuta mtu uliingiza kipato kikubwa tu cha fedha, lakini mwisho wa siku unajiona hujabakiwa na kitu na ukijaribu kuwaza umefanyia nini cha maana hauna. Matokeo yake unajikuta...

Fahamu Kuhusu Tabia/Sifa Za Fedha...

Image
Habari rafiki! Ni matumaini yangu u mzima wa afya! Kwa upande wangu namshukuru Mungu, niko mzima wa afya na ninaendelea vyema kabisa! Karibu sana kwenye mwendelezo wa somo linaloangazia kuhusu elimu ya fedha! Kama unakumbuka makala iliyopita ilishia kudokeza sifa kuu mbili za fedha!  Makala hii ni mwendelezo wa makala iliyopita, kwa leo utaenda kuoneshwa sifa nyingine bainifu za fedha kama zinavyodokezwa hapa chini:- 3. Fedha Huwafuata Watu Wenye Imani Nayo... Kuamini ni kupokea kuwa jambo fulani ni kweli hata kama jambo hilo siyo kweli!! Hii ni sawa na kusema il i ufanikiwe kifedha unatakiwa upokee kuwa ni kweli unamiliki fedha nyingi hata kama mfukoni mwako hauna fedha kabisa! Unatakiwa kujua kwamba, imani halisi haiji katika kuona uhalisia wa tukio lenyewe, bali inakuja kwa kuweka tumaini thabiti juu ya kile kilichoaminiwa kuwa kitatokea! Na ndiyo maana kanuni ya kuamini inasema, "chochote kile utakachokiamini kuhusu wewe na dunia yako kitafanyika kwako pamoja na d...

Onyo! Hata Usifikirie Kubadli Hali Yako Ya Kifedha Mpaka Usome Kwanza Hii...

Image
Habari rafiki! Ni matumaini yangu u mzima wa afya!  Kwa upande wangu namshukuru Mungu, niko mzima wa afya na ninaendelea vyema kabisa! Karibu sana kwenye mwendelezo wa somo linaloangazia kuhusu elimu ya fedha!  Kama unakumbuka makala iliyopita ilishia kudokeza tafsiri kuu mbili za fedha! Makala hii ni mwendelezo wa makala iliyopita, kwa leo utaenda kuoneshwa sifa za fedha. Je ni zipi sifa bainifu za fedha? Usijalii ndani ya muda unaenda kuoneshwa sifa za fedha kama zifuatazo: 1. 𝐅𝐞𝐝𝐡𝐚 I𝐧𝐚𝐨𝐧𝐠𝐨𝐳𝐰𝐚 N𝐚 𝐊𝐮𝐭𝐞𝐧𝐠𝐞𝐧𝐞𝐳𝐚 K𝐰𝐚 𝐊𝐚𝐧𝐮𝐧𝐢. Kila eneo linalohusu maisha ya binadamu hutawaliwa na kanuni fulani mahususi, na ifahamike kwamba  kanuni hizo ndizo hupima na kupelekea matokeo fulani katika eneo hilo! Ukweli ni kwamba kanuni huwa hazidanganyi, lakini endapo itatokea ukafanya kinyume na matakwa ya kanuni hizo basi utaishia kupata matokeo mabaya. Unatakiwa kujua kwamba kuna kanuni zaidi ya 20 za fedha. Hii ni sawa na kusema utafanikiwa kifed...

Huwezi Kujua Fedha Ni Nini Mpaka Usome Kwanza Hii...

Image
Hivi unafahamu kuwa watu wengi hawajui fedha ni nini, hali ambayo huwafanya wakutane na masumbufu mengi katika kuipata na hata kama wakiipata hujikuta wakiishia kuipoteza? Ukweli ni kwamba watu wengi wanajua jinsi ya kupata fedha, lakini hawajui jinsi ya kuidhibiti fedha yao isipotee! Hii ni sawa na kusema tunatengeneza fedha kwa kile tunachokijua, na tunapoteza fedha kwa kile tusichokijua! Hata hivyo, katika dunia tuliyonayo sasa watu wengi wako bize muda wote kutafuta fedha lakini hawajui fedha ni nini... Watu wengi wako bize kuweka hata malengo ya kifedha lakini wanashindwa kufikia malengo hayo kwa vile hawajui fedha ni nini... Hata hivyo wapo wanaochanganya fedha na karatasi, yaani wao wanajua kwamba fedha ni noti au sarafu kitu ambacho siyo sahihi! Na kama, na wewe ulikuwa unaamini fedha ni karatasi, nataka nikupe challenge hii: huwa unafanya nini mpaka upate hilo karatasi (noti) au hiyo sarafu unayoiita fedha? Unachopaswa kujua ni kwamba kile ambacho unafanya kabla hu...

Sababu Kuu Tatu Kwanini Unatakiwa Usome Ujumbe Huu...

Image
  Habari yako rafiki! Ni matumaini yangu u mzima wa afya! Kwa upande wangu namshukuru Mungu niko vizuri na ninaendelea vyema kabisa! Karibu kwenye mwendelezo wa somo letu linaloangazia uwezo wa maeneo kumi ambayo kila binadamu huzaliwa nao!  Kama unakumbuka vizuri, makala iliyopita ilidokeza hoja tatu za maeneo uwezo! Hii ni sawa na kusema, makala hii ni mwendelezo wa makala iliyopita! Kwa leo utaenda kuoneshwa uwezo mwingine wa maeneo matatu ambayo kila binadamu huzaliwa nao! Na huu ndiyo utakuwa mwisho wa maeneo yote kumi! Karibu sasa kwenye uchambuzi wa uwezo wa maeneo matatu ya mwisho kabisa:-  8. Uwezo wa ushawishi (interpersonal Intelligence)... Huu ni uwezo wa kushawishi, kuwasiliana, kusihi, kutuliza migogoro pamoja na kuunganisha watu. Kuna watu ambao wao wana uwezo mkubwa sana wa kushawishi watu na popote wanapopata kupita huwa wanakubalika sana kutokana na ushawishi wao.. SIFA ZAO. ➡️Wanapenda sana kuzungumza... ➡️Wanatengeneza marafiki kirahisi san...

Fahamu Kuhusu Maeneo Matatu Ya Uwezo Ambao Kila Binadamu Huzaliwa Nao....

Image
Habari yako rafiki! Ni matumaini yangu u mzima wa afya! Kwa upande wangu namshukuru Mungu niko vizuri na ninaendelea vyema kabisa! Karibu kwenye mwendelezo wa somo letu linaloangazia uwezo wa maeneo kumi ambayo kila binadamu huzaliwa nao!  Kama unakumbuka vizuri, makala iliyopita ilidokeza hoja tatu za maeneo uwezo! Hii ni sawa na kusema, makala hii ni mwendelezo wa makala iliyopita! Kwa leo utaenda kuoneshwa uwezo mwingine wa maeneo matatu ambayo kila binadamu huzaliwa nao! Angalizo: unaposoma maeneo haya ya uwezo, uwe unahusisha na maisha yako ili utambue unamiliki uwezo gani! Ukishatambua eneo la uwezo wako kwa msaada zaidi nitafute nami nitakupa mawili matatu juu ya kipi unatakiwa ufanye! Karibu sasa kwenye uchambuzi wa maeneo mengine matatu:-  5. Uwezo Wa  Uchoraji (Spatial Intelligence) Hawa ni wataalamu katika kuona matukio fulani na kisha kwenda kuyatengenezea picha kwa kuyachora na kuyawasilisha kupitia michoro mbalimbali... Wana uwezo mzuri sana wa k...

Huwezi Kugundua Uwezo Uliozaliwa Nao Mpaka Usome Kwanza Hii....

Image
Habari yako rafiki! Ni matumaini yangu u mzima wa afya!  Kwa upande wangu namshukuru Mungu niko vizuri na ninaendelea vyema kabisa! Karibu kwenye mwendelezo wa somo letu linaloangazia uwezo wa maeneo kumi ambayo kila binadamu huzaliwa nao!  Kama unakumbuka vizuri, makala iliyopita ilidokeza hoja moja ya eneo la uwezo!  Hii ni sawa na kusema, makala hii ni mwendelezo wa makala iliyopita! Kwa leo utaenda kuoneshwa uwezo mwingine wa maeneo matatu ambayo kila binadamu huzaliwa nao! Angalizo: unaposoma maeneo haya ya uwezo, uwe unahusisha na maisha yako ili utambue unamiliki uwezo gani! Ukishatambua eneo la uwezo wako kwa msaada zaidi nitafute nami nitakupa mawili matatu juu ya kipi unatakiwa ufanye! Karibu sasa kwenye uchambuzi wa maeneo mengine matatu:- 2. Uwezo Wa Kuchezesha Viungo Vya Mwili (Bodly kinetisthetic)/ (body smart) Hawa ni watu ambao wana uwezo wa kutumia viungo vya mwili pamoja na mijongeo ya kimadaha... Bila shaka katika kuishi kwako, umekutana na ...

Huwezi Kufahamu Uwezo Uliozaliwa Nao Mpaka Usome Kwanza Hii..

Image
Hivi unafahamu kuwa kila mwanadamu ndani yake anamiliki uwezo mkubwa sana aliozaliwa nao, ili umsaidie katika kuishi kwake hapa duniani?  Kwa mujibu wa tafiti za kisaikolojia kuwahi kufanyika zimeonesha kwamba, hakuna binadamu anayezaliwa akiwa hana uwezo fulani ndani yake (hazina), bali k ila binadamu huzaliwa na uwezo asilia ambao Mungu alimuumbia ili umsaidie katika kuishi kwake hapa duniani... Hata hivyo, kinachosikitisha na kushangaza zaidi ni pale unakuta watu wengi ambao wanamiliki uwezo huo ndani yao hawajui kabisa kuhusu hili, huku wengine wakiwa hawajui kabisa kuwa ndani yao kuna hazina kubwa sana ambayo, endapo ingetumika basi ingebadili kabisa hali za maisha yao. (Yaani hali za kiuchumi, kijamii pamoja na kitaifa kwa ujumla wake )  Ukiachilia hilo, moja ya sababu ambayo huwafanya watu hawa washindwe kugundua uwezo wao ni kutokana na mifumo iliyowatengeneza! Hata hivyo, ukichimba ndani zaidi katika ulimwengu wa saikolojia, mifumo hii hufamika kama archet...

Huwezi Kujua Kusudi La Kuumbwa Kwako Mpaka Usome Kwanza Hii...

Image
Hivi unafahamu kwamba zaidi ya asilimia 80 ya watu duniani kote hawaliishi kusudi la kuumbwa kwao, bali wanaishi huku wakitimiza kusudi ambalo hawakuumbiwa huku wengine wakikosa kabisa kitu cha kufanya?  Huenda hata wewe umekuwa ni mtu ambaye mpaka sasa hujajua kwanini uliumbwa, upo hapa duniani kwa kusudi gani na unatakiwa ufanye nini ili uweze kutimiza kusudi la kuumbwa kwako! Rafiki unatakiwa kujua kwamba maisha pasipo kusudi si kitu, kwa sababu maana halisi ya maisha imebebwa na kusudi.  Hii ni sawa na kusema kama haujui kusudi la kuumbwa kwako maana yake umeshapoteza maana halisi ya maisha yako!   Na, ikiwa ushapoteza maana halisi ya maisha yako maana yake hakuna ulazima wa wewe kuendelea kuishi tena… Kwa sababu hata kama utaendelea kuishi hakuna kitu chochote cha maana ambacho unaweza ukakifanya kwa ajili ya maisha yako, dunia yako, jamii yako pamoja na maisha ya watu wengine. Sijui kwanini unasoma makala hii, lakini uamuzi ulioufanya wa kusoma maka...