Kwanini Huwa Unapata Kinyume Na Kile Unachokiomba...
Na Emmanuel Samuel King'ung'e Hivi unafahamu kwamba zaidi ya asilimia 90 ya sala zinazoombwa na watu wengi huishia kuwaletea matokeo yaliyo kinyume na matarajio yao? Kwa mujibu wa tafiti binafsi nilizofanya nimebaini kwamba, hili limekuwa ni tatizo linalowakumba watu wengi sana! Huenda hata wewe umekuwa ukikumbana na tatizo hili, usijisikie mpweke kwani wapo watu wengi sana wanaokumbwa na changamoto kama yako! Habari njema ni kwamba makala hii inaenda kutatua kabisa tatizo hili ambalo huenda limekutesa kwa muda mrefu, na umekuwa ukijiuliza maswali mengi pasipo kupata majibu muafaka! Kwa mfano huenda ukawa u memuomba Mungu akujaalie utele katika jambo fulani, halafu ukaishia kupata ukomo! Na kinachokuvunja Moyo zaidi ni pale unapotambua fika kabisa kwamba, Mungu wetu ni tajiri na vitu vyote ni mali yake! Sasa inakuwaje Wewe unakuwa siyo sehemu ya utajiri huo? Je ni kweli kwamba Mungu anakuwa amekutenga? Je ni kweli kwamba Mungu anakuwa hakujali? Je ni kweli kwamba...