KUNA WATU WANACHAMBUA… NA KUNA WATU WANACHANGANUA
Mara nyingi nimekuwa nikisema:
Kuna watu wanajua wanavyosema…
na kuna watu hawajui.
Na kuna watu wanachambua,
na kuna watu wanachanganua.
Mchambuzi ataelezea jambo kama lilivyo.
Lakini mchanganuzi… atalipa jambo MAANA.
Na ukweli ni huu:
👉 Wengi wanaishia kuchambua.
Chukulia mfano wa neno “Mungu”.
Wengi wanachambua tu—wanajua kulitamka, kulijadili, hata kulitetea.
Lakini hawafiki kwenye kina.
Mchanganuzi atakuambia:
👉 Jina “Mungu” halipo kugawa watu—lipo kuwaunganisha kwa sababu ndiyo hoja kubwa zaidi kuliko zote.
Lakini kwa sababu ya kuchambua bila kuchanganua…
kile kilichotakiwa kuunganisha, kimekuwa sababu ya kugawanyika. Unaona?
Leo nikiwa mahali, mtu akaniuliza:
“Wachumba wapo huko uliko?”
Nikasema: “Wapo.”
Akasema: “Mimi wananikataa kwa sababu nimeokoka, wao ni madhehebu mengine.”
Nikamwambia:
👉 “Mimi Biblia nimesoma yote. Niambie dhehebu lililoandikwa mule.”
Akakosa jibu.
Sikumwambia aache imani.
Nilimwambia ukweli mmoja tu:
👉 Endelea kuchambua… lakini ujue bado hujafika kwenye MAANA.
Kwa sababu kabla ya dhehebu—
wewe ni MTU.
Tukaingia kwenye suala la KAZI.
Nikasema hivi:
Wachambuzi watakwambia:
“Kila kitu ni kazi.”
Lakini mchanganuzi atasema:
👉 Kuna wanaofanya kazi
👉 Na kuna wanaotumia matokeo ya kazi za wengine
Na hapa ndipo wengi wetu tunapojidanganya.
Ndiyo, tunafanya kazi.
Lakini swali siyo tu unafanya kazi gani.
👉 Swali ni: UNAUNDA NINI?
Ukweli mchungu ni kwamba:
Tumekuwa watu wa kutumia vitu vilivyoundwa na wengine, kuliko kuunda vyetu.
>> Tunajua kutumia computer… lakini hatujui kuiunda
>> Tunatumia mitaala… lakini hatuibuni
>> Tunatumia dawa… lakini hatutengenezi
>> Tunatumia mifumo… lakini si yetu
Hii haimaanishi hatufanyi kazi.
Inamaanisha bado hatujafika hatua ya kuunda.
Nakumbuka hata tarehe 9 December 2025 niliwahi kuwahoji:
👉 “Mnasemaje mnasheherekea uhuru, wakati bado mnakumbatia mifumo iliyowaondolea uhuru?”
Elimu si yetu. Siasa si yetu. Dini tumepewa tafsiri
Sio lawama. Ni swali.
Kwa sababu uhuru wa kweli unaanza kwenye fikra—sio kwenye sherehe.
Sasa nauliza tena:
👉 Wewe ni mfanyakazi halisi…
au ni mtumiaji wa kazi za wengine?
Kabla hujajibu, anza hapa:
>> Usijifunze kutumia tu—jifunze kuunda
>> Usikubali kila kitu kilivyo—uliza “kwa nini?”
>> Elewa vitu kwa kina, si juu juu
>> Ongeza kitu, hata kidogo, kwenye kile unachofanya
Kesho ukiamka, una maamuzi mawili:
👉 Kuendelea kutumia vilivyoundwa na wengine
AU
👉 Kuanza kuwa sehemu ya wanaoleta MAANA
Mimi siyo mpinzani.
Mimi siyo mchambuzi wa juu juu.
Mimi ni mchanganuzi.
✍️ Naitwa Mbulwa King’ung’e
📞 0744284329
Mara zote huwa nafikiri TOFAUTI.
Comments
Post a Comment