Huwezi Kubadili Kesho Yako Mpaka Usome Kwanza Hii..
Hivi unajua kwamba kesho yako inatabirika kulingana na hali yako uliyonayo leo pamoja na kile unachokifanya?
Unatakiwa kujua kwamba, kama vile mama mjamzito anavyokadiriwa kuwa atazaa baada ya miezi tisa. Vivyo hivyo ndivyo ilivyo kwa kesho yako.
Hii ni sawa na kusema kuwa, kesho yako inatabirika kulingana na hali yako ya leo!
Mbali na hilo kanuni ya makadirio inasema kwamba; “kwa kila tukio linalotokea kuna uwezekano kuwa tukio hilo hutokea kutokana na hali fulani.”
Tukihusisha kanuni hii na kesho yako, tutasema kesho yako inatabarika kupitia hali uliyonayo leo pamoja na kile unachokifanya.
Kwa minajiri hiyo kile unachokifanya leo, ndicho kimebeba thamani ya kesho yako!
Hata hivyo kabla sijaenda mbali zaidi unatakiwa ujiulize swali hili, "vipi kama hali niliyonayo leo itaendelea kuwa hivihivi pamoja na hiki ninachikofanya leo kikaendelea kunipa matokeo haya haya?"
Je, maisha yangu baada ya miaka kumi yatakuwaje?
Sijajua upo katika hali gani. Lakini jibu ulilolipata hapa lifanyie tathmini. Kumbuka huwezi kubadili kesho yako kama hutaanza kubadili leo yako kwanza!
Sijajua kwanini unasoma makala hii, lakini uamuzi uliofanya kusoma makala hii ni uamuzi mzuri sana kuwahi kuufanya!
Hii ni kwa Sababu makala hii inaenda kukupa nuru mpya, mtizamo mpya pamoja na mbinu mpya zitakazokusaidia uweze kubadili kesho yako!
Nifanye Nini Ili Nibadili Kesho Yangu…? Alisikika mtu mmoja akiniuliza, wakati nilipokuwa nikitoa mafunzo. Nami sikuwa na majibu mengi sana, nikampa jibu moja tu lililomshangaza sana, nahisi na wewe litakushangaza kidogo…
Nilimjibu hivi; “njia rahisi ya kubadili kesho yako ni kuanza na mwisho wa kesho yako” nikaongezea kwa kusema kwamba, “ukishauona mwisho wa kesho yako utapata utayari wa kuufikia mwisho huo”.
Na, utaufikia huo mwisho kwa sababu umeshapata nguvu ya kwanini unatakiwa ufike huko!
Nakuja kwako mpendwa wangu, vipi unaona nini kuhusu kesho?
Je, una picha gani kichwani mwako kuhusu kesho yako?
Rafiki, kama ulikuwa hujui basi leo nakupasha na habari motomoto, unatakiwa kujua kwamba kile unachopata katika maisha yako, ni uakisi wa kile unachokitegeneza pamoja na kile unachokiona akilini mwako.
Kwa mantiki hiyo endapo utakuwa umeuona mwisho mbaya lazima utaufikia, kwa sababu ni wewe mwenyewe ndiye umehusika katika kuutengeneza akilini mwako pamoja na kuuona!
Rafiki, unatakiwa kujua kwamba, hakuna kitu chenye nguvu kama picha. Hivyo basi zoezi la kubadili kesho yako linatakiwa lianze kwako, kwa kufuta picha zote mbaya unazoziona kuhusu wewe na kesho yako.
Pia, unatakiwa ufute kauli zote mbaya ulizoambiwa au ulizojiambia wewe mwenyewe kuhusu kesho yako.
Mara baada ya kufanya hivyo, huu utakuwa ni wakati muafaka wa wewe kuanza kuipamba kesho yako kupitia akili zako kwa kujiona: umeshafanikiwa, unaishi maisha ya ndoto yako, unafanya kile unachopenda kukifanya pamoja na kupata kila utakachokihitaji maishani mwako!
Kama zoezi la kufuta picha mbaya kuhusu kesho yako limekamilika basi, katika sehemu hii utajifunza hatua muhimu za kuchukua ili ubadili kesho yako.
Hata hivyo ili kubadili kesho yako huna budi kufanyia kazi mikakati ifuatayo. Na, huwa nawaambia watu siku zote kwamba maisha yetu ni kama mti ulioota sehemu fulani.
Sote tunafahamu kuwa mti huwa hautembei. Hii ni sawa kabisa na maisha yako, kwa sababu maisha yako hayawezi kujongea mpaka pale wewe utakapoamua kuanza kujongea nayo.
Kwa mantiki hiyo wewe ndiye una wajibu wa kutoa msukumo kwenye maisha yako, ili ubadili kesho yako kwa kufanya yafuatayo:-
1. Weka Malengo Mbalimbali Kuhusu Kesho Yako…
Hauwezi kufikia lengo kama hutaazimia lengo lolote lile. Hii ni sawa na kusema, huwezi kupata kesho nzuri kama hutaweza kuazimia malengo mbalimbali kuhusu kesho hiyo.
Unachopaswa kujua ni kwamba unahitaji kuazimia lengo ili kufikia lengo.
Jambo lingine unalopaswa kujua ni kwamba, kuweka lengo ni mchakato wa kukufanya wewe uibuke mshindi katika eneo uliloliazimia.
Hata hivyo maishani huwezi kupata kitu ambacho hukitafuti hata kama kitakuwa mazingira uliyopo.
Sikia hii tena rafiki yangu, maisha bila malengo ni sawa na mtumbwi unaosukumwa na upepo usijue unaenda wapi, ijapokuwa unakuwa upo kwenye mwendo tayari.
Hivyo basi ili uweze kupata picha kamili juu ya uelekeo wa maisha yako unatakiwa ujihoji hili; ni wapi ninayapeleka maisha yangu kwa siku zijazo?
Rafiki hutakiwi kabisa kuyafanya maisha yako yawe kama mtumbwi, unaolea juu ya maji huku ukisukumwa na upepo usijue unakoelekea!
Hata hivyo katika historia kuna kisa kinamuelezea Christopher coulumbus aliyegundua bara la Amerika.
Cha kushangaza ni kwamba mwanajiografia huyu aligundua bara la Amerika, lakini yeye alikuwa anatafuta route ya kwenda India! Wewe hupaswi kuwa kama yeye.
Bali unatakiwa kujua, kule unakoipeleka kesho yako kwa kuiwekea malengo mbalimbali.
Ndugu unahitaji kuazimia malengo kuhusu kesho yako kwa kuyaandika.
Je,unataka utimize nini kuhusu maisha yako?
Je, unataka kuifanyia nini kesho yako?
Je, unataka dunia ikutambue wewe kama nani baada ya miaka mitano ijayo?
Unapaswa ujibu maswali hayo kwa ufasaha.
Lengo likiwa ni kupima uelekeo wa kesho yako unayoitaka na yule unayetaka uwe. Kumbuka hakuna atakayekupangia kuhusu kesho yako pasipo uhusika wako, hata hivyo kutokupanga ni sawa na kupanga kushindwa.
Jinsi Ya Kupanga Na Kufanikisha Malengo Yako…
Kitu unachopaswa kujua ni kwamba kuazimia malengo ni kitu kingine na kufanikisha lengo ni kitu kingine.
Lengo likiazimiwa haimaanishi kwamba ndiyo limetimia. Hivyo basi ili kufanikisha lango lako hatua zifuatazo ni lazima zizingatiwe kwanza:-
Mwendelezo Wa Somo Hili Utaendelea Kwa Siku Ya Kesho!
Ahsante Sana Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri!
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Mwl, Mwandishi Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!
Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 0673184329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com
Comments
Post a Comment