Dunia ni Halisi; Ila Kuna Watu Waliovuruga Mfumo wa Dunia Kwa Lengo la Kuwatawala Wengine...
Hapo Kale kabla Mimi na wewe hatujazaliwa. Wapo watu wachache sana duniani waliokuja na lengo moja kali: kuvuruga mfumo wa dunia ili kutawala watu!
Sihofii kuhusu ukubwa wa mtu, wala mabavu yake, lakini si kila mtu mkubwa anajitambua kweli. Kuna wakubwa waliopotea, akili zao zimefungwa, na hawajui hata nafsi zao!
Kujielewa ni msingi wa kuishi kwa utu.
Kutokujielewa ni chanzo kikubwa cha mivurugano, migogoro, na maafa yanayotukumba leo hii!
Mwafrika wa leo anajivunia sana elimu ya Magharibi, lakini elimu hii ni ya kinyonge, ni kifungo cha akili kinachomfanya mtu awe mfanyakazi tu wa mfumo, si mbunifu wala mkombozi wa jamii.
Elimu hii imemfunga mtu kwa kumsahaulisha rasilimali zake za aina yake na kumfanya awe sehemu ya mfumo unaoharibu maisha ya wengi kwa kufanya mambo yasiyo sahihi huku akiwacha wafuasi wake kwenye taabu.
Mwafrika wa leo anakumbatia imani potofu na mitazamo inayojenga chuki na uadui kwa sababu anaamini ni njia pekee ya kumlinda mwenye mali au mamlaka, hata akijua anavunja umoja wa watu wake, huku yeye akiwa hanufaiki na lolote lile!
Yupo tayari kuzungumza ujinga na kudanganya, akitaka tu kupata fedha, bila kujali athari kwa jamii na vizazi vijavyo.
Tunazalisha kizazi kisichojielewa kwa sababu sisi tunaoleta watoto duniani hatujielewi!
Tunaridhika na kazi na mshahara, lakini hatufikirii urithi wa kiakili tunaoutaacha kwa watoto wetu.
Tunakumbatia mambo ambayo yaliwaatabisha babu zetu kwa mateso makubwa — kuuawa, kutumikishwa, hatimaye walipigana na kuyashinda lakini sisi tumeyageuza na kuyafanya kuwa mtindo wetu wa maisha ya sasa!
Hakuna anayethubutu kuuliza “Ilikuwaje hivi?” kwa sababu kila anayetoa hoja anazimwa na kuonywa kwa laana ya "kukufuru."
Lakini mimi, M’bulwa King’ung’e, nakuambia wazi:
HAKUNA mtu anayepaswa kukukandamiza kwa sababu haukujua uovu uliokufikia!
Fikiria mtu aliyekatishwa tamaa na mfumo huu, aliyeishishwa hapa duniani, hajatafuta asili yake halisi, amekubali hali, hana ndoto wala matumaini.
Je, mtu kama huyu anapaswa kulaumiwa? Hapana! Ana haki ya kuchoshwa, ana haki ya msaada!
Ndio maana niko hapa, kuchochea akili zilizofungwa, kuanzisha mchakato wa kufungua macho ya wengi!
Akili zetu zinahitaji kurekebishwa, kufikirikishwa upya!
Msikubali kila kilichokuja kutoka ulaya na kuamininika na wazazi wetu kuwa ni KWELI, vingine vipo kama mfumo wa kulemaza na kufubaisha akili.
Nimekutana na watu wazima wengi waliopotea, wanaishi wakiwa kwenye kitanzi kikubwa!
Kitanzi hiki hakionekani kwa kila mtu, ila kwa wachache kama mimi ni wazi: tumepotea, tumefungwa, tumekuwa watumwa wa akili zetu wenyewe.
Huu ni wakati wa kuamka, kujiwekea viungo upya, na kurudi kwenye asili yetu ya kweli!
Mapendekezo Makubwa Kwa Ajili ya Mabadiliko ya Afrika:
1. Kumjua Mungu wa kweli kwa namna moja - si miungu ya ukoloni na viabudiwa vilivyoletwa na wakoloni!
Mungu wa kweli ni msingi wa umoja, utu na haki halisi, si chanzo cha ubaguzi au uadui!
2. Kuboresha mfumo wa elimu kwa mwelekeo wa utambuzi binafsi, sio tu upimaji wa ufaulu wa mitihani!
Mfumo huu mpya lazima ubadilishe mtazamo wa walimu na wanafunzi, ili mabadiliko ya kweli yafikie matokeo!
Kwa kufanikisha haya mawili, tutaanza kujielewa, kuungana, na kujenga jamii yenye amani, salama na mafanikio halisi!
Ndimi M’bulwa King’ung’e, nawaambia: Afrika imeharibika kwa sababu tumekubali mfumo potofu! Wakati umefika wa kupindua mfumo huu, kurejesha hadhi yetu na utu wa kweli!
Ni wakati wetu wa kuamka, kujiuliza, na kuishi kwa uhalisia!
Kuhusu Mwandishi
Emmanuel Samuel King’ung’e, maarufu kama M’bulwa King’ung’e, ni mtaalam wa utambuzi binafsi, mshauri wa maendeleo ya binafsi na kijamii, na mwanzilishi wa King Mentorship Program.
Kwa miaka mingi, amekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha Wafrika kuamka kiakili na kiroho, kuondoa fikra potofu, na kujijengea uwezo wa kuongoza maisha yao kwa hekima na ujasiri.
Kupitia King Mentorship Program, Emmanuel anawasaidia watu mbalimbali kujitambua, kuvunja minyororo ya ukandamizaji wa akili, na kufanikisha malengo yao ya kweli kwa kutumia mbinu za kisasa za utambuzi binafsi na maarifa ya asili.
Kwa matumaini na moyo wa mabadiliko, M’bulwa King’ung’e anatoa mwito mkali kwa kila mtu mwenye kiu ya kubadilisha maisha yake na jamii kujiunga na King Mentorship Program - sehemu ambapo utaweza kupata mafunzo, ushauri, na uongozi wa moja kwa moja wa kukusaidia kufikia mafanikio halisi na uhuru wa kweli.
Jiunge Na King Mentorship Program Leo!
Usikose nafasi hii ya aina yake ya kuanza safari ya mabadiliko yako binafsi na kijamii. Kupitia programu hii, utafundishwa mbinu za utambuzi binafsi, kuondoa vizingiti vya fikra potofu, na kujifunza jinsi ya kuishi maisha yenye tija, amani, na mafanikio.
Huu ni mwito wa kuamka, wa kujitambua, na wa kushinda minyororo ya akili zilizokufunga.
Kwa maelezo zaidi na usajili, wasiliana nasi kupitia nambari:
📞 0744284329
Hapa ndipo safari ya kweli ya mabadiliko inapoanza. Jiunge sasa, na uwe sehemu ya kizazi cha viongozi wa Afrika wa kesho!
Comments
Post a Comment