Kadri Unavyoongezeka Thamani, Ndivyo Fedha Zinavyokufuata — Je, Umejiwekea Thamani Yoyote?
Siku zinavyozidi kwenda mbele, kila mtu anakaribia uzee. Hakuna anayerudi kuwa mtoto tena. Kifo kinakuja polepole, bila tahadhari — lakini kinakuja!
Swali ni, thamani yako inaendelea kupanda au kushuka? Je, wewe wa jana ulikuwa na thamani gani? Na wewe wa leo, uko wapi kithamani?
Je, watu wanaokutegemea wanaongezeka au wanapungua? Je, watu wanakuzungumziaje? Je, katika kuishi KWAKO unavuta watu wa thamani au unapoteza nafasi zao?
Fedha inafuata thamani — ni sheria isiyoandikwa ya maisha. Je, una thamani ya kutosha kuvuta fedha kwako?
Nakumbuka mwaka 2022, nilipokuwepo kwenye hali ngumu. Sikuwa mtu wa thamani, sikuweza kutengeneza fedha, na maisha yalikuwa ya kawaida tu—hakuna mwangaza wala matumaini.
Lakini siku moja, nikajitazama kwenye kioo na kusema, "Hili hali haitatokea bila sababu kubwa." Lazima nifanye jambo. Niliamua kuchukua hatua.
Nikaanza kujifunza, kuwekeza muda, nguvu, na akili zangu kwenye kujenga thamani yangu binafsi. Siku za mwanzo zilikuwa ngumu, lakini pole pole, thamani yangu ilianza kuongezeka.
Leo, fedha zinanifuata kama kivuli! Siku hizi, watu hunitafuta, wananihitaji, na wapo tayari kunilipa kwa sababu nagusa maisha yao kwa maana.
Watu hutoa pesa kwa vitu wanavyovithamini. Je, unajitengenezea thamani ambayo watu wanaweza kugharamia?
Kama haujajenga thamani, fedha haitakufuata! Najua, maana nilipitia hapo hapo.
Leo hii thamani yangu imeongezeka Nina ELIMU ya Mungu Mwenye vyote ambayo ndi Elimu ya msingi ipitayo Elimu zote hapa duniani, nina ELIMU ya fedha, saikolojia, maendeleo binafsi, ninafanya coaching, ushauri, mentorship, na uandishi, fedha inanifuata! Hii sio bahati, ni matokeo ya kujitahidi na kujitengenezea thamani.
Usisubiri fedha ikukimbilie — jenga thamani yako! Anza leo kuwekeza kwenye akili zako, ujuzi wako, na uwezo wako wa kiroho na kiakili.
Usijifunge kwenye hali ya kawaida, jifunze kuwa mtu wa thamani — mtu anayeonekana na kuthaminiwa.
Jina langu ni Emmanuel Samuel King’ung’e. Naomba nikualike ujiunge nami kwenye King Mentorship Program — programu inayokusaidia kutambua thamani yako halisi, kukuza vipaji vyako, na kufikia mafanikio unayoyatamani.
📞 Wasiliana nami sasa: 0744 284 329
Usikubali maisha yakupite bila kujenga thamani yako! Fedha hufuata thamani — wewe jenga thamani, na mafanikio yatafuata.
Je, tayari kuanza safari yako ya mabadiliko? Jisajili sasa, na tuanze pamoja!
Comments
Post a Comment