Muda Hutufundisha Thamani Ya Maisha...
Na Emmanuel Samuel King'ung'e
Usipotumia muda wako katika kufanya mambo ya msingi, basi mambo yasiyo ya msingi ndiyo yatatawala matumizi ya muda wako!
Uelewa kuhusu muda bado upo katika kiwango cha chini sana miongoni mwa watu wengi, na hii ndiyo sababu kubwa watu wengi hutumia sehemu kubwa ya muda wao kufanya vitu visivyokuwa na thamani kabisa au vyenye thamani ndogo!
Je muda wako wote wa thamani ulionao huwa unatumia kufanya nini?
Kumbuka, ili jambo fulani liweze kutokea ni lazima lifungamane na kipindi fulani cha muda! Hii inamaanisha pasipo uwepo wa muda hakuna chochote kile kitakachotokea!
Hivyo basi endapo utakuwa hauna chochote cha maana unachokifanya kwenye matumizi ya muda wako, hakuna matokeo ya maana utakakayoyapata maishani mwako!
Unatakiwa kujua kwamba wengi wetu huwa tunaishia kuwa watu wa kawaida, pamoja na kupata matokeo ya wastani kutokana na namna tunavyotumia muda wetu!
Weka suala hili akilini mwako, daima muda huwa ndiyo kizuizi cha mwisho, kwani hauwezi kurudishwa nyuma, kusimamishwa, kusogezwa mbele wala kupunguzwa...
Mpenzi msomaji unatakiwa kujua kwamba kuna muda ndani ya muda!
Hivyo basi unaalikwa kuanza kuhesabu muda wako kuanzia sekunde moja hadi nyingine, kwani kupitia sekunde dakika hupatikana, kupitia dakika saa hupatikana, kupitia saa siku hupatikana kupitia siku wiki hupatikana, kupitia wiki miezi hupatikana, kupitia miezi mwaka, hupatikana kupitia mwaka miaka hupatikana. N.k
Hii inamaanisha kwamba kuna muda ndani ya muda hivyo basi ukipoteza hata sekunde moja tu umepoteza kitu kikubwa sana...
Hakuna aliyependelewa muda, bali sote tuna muda sawa, ila tunaishia kupata matokeo tofauti kutokana na namna tunavyotumia muda wetu!Usipochunga matumizi ya muda wako, hakuna atakayechunga kwa niaba yako!
Jifunze kukomboa wakati, ili upate matokeo makubwa maishani mwako!
Kumbuka kwa kila jambo Kuna majira yake.Hata hivyo hauwezi kuotea muda bali unaweza kuotea kufanya jambo fulani kutokana na muda uliopo!
Kesho nitakusogezea mambo matano Kuhusu Muda!
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e mwalimu mwandishi muelimishaji katika eneo la maendeleo Binafsi life coach and consultant!
Unaweza kuwasiliana nami kupitia Whatsapp no+255744284329
Ahsante sana mwalimu Kwa somo hili, maisha Kwa ujumla ni muda ndio maana Kila kitu unachokifanya ktk maisha mtu anapokuhoji atakuhoji umekifanya Kwa mda Gani, umeishi huko mda Gani, unapata mshahara kiasi Fulani Kwa mda , Gani , mtu ana umri Gani Toka kuzaliwa Kwa hiyo utaona kwamba maisha ni muda, hivyo ukiweza kucheza vizuri na muda ktk maisha utapata pesa nyingi na maisha Yako yatakuwa mepesi ndio maana wazungu husema time is money, muda mali
ReplyDeleteAhsante sana kwa ufafanuzi mzuri! Karibu sanaa!
Delete