Mambo Matano Unayopaswa Uyafahamu Kuhusu Muda...

Na Emmanuel Samuel King'ung'e

Hivi unafahamu kwamba muda ni rasilimali ambayo inaweza kuwekezwa?

Huenda ukawa hulifahamu jambo hilo, ndiyo maana umekuwa ni muumini wa kutumia muda kiupotevu pasipo hata kujua kwamba kuna sehemu ya muda wako unaipoteza!

Zifuatazo ni hoja zenye mashiko kuhusu muda!

1. Muda ni maisha!
Muda ndicho kipimo halisi  cha hadhi ya maisha ya kila binadamu.
Kwamba kutoka siku umezaliwa mpaka sasa, umeweza kuishi ndani ya kipindi cha muda fulani! 

Hivyo basi hadhi ya maisha utakayokuwa nayo itathaminishwa kwa kuhusishwa na kipindi cha muda ulichoishi. Hata hivyo hadhi utakayokuwa nayo ndicho kitakuwa kipimo halisi kinachoonesha matumizi yako ya muda yapoje!

Kwa mfano tufanye labda umeishi kutoka 1990 hadi 2030. 

unachopaswa kujua ni kwamba, utakuwa na hadhi fulani kimaisha kadri ya muda uliotumia kuishi pamoja na namna ulivyotumia muda wako!

Jaribu kufanya uchunguzi, utajua kwamba kuna baadhi ya watu wana umri mdogo lakini wamepiga hatua ndefu kimaisha, ilihali kuna watu wengine wana umri mkubwa lakini hakuna hatua yoyote ya maana waliyopiga kimaisha!

Tofauti ya kimaisha ya watu hawa haipo kwenye umri bali ipo kwenye namna wanavyotumia muda wao!

Je kwa kipindi chote ulichoishi mpaka kufikia sasa  unajivunia kufanya nini?

Je hadhi ya maisha yako ipoje mpaka sasa?
Kumbuka muda uliopotezwa ni sawa na maisha yaliyopotezwa!
Muda ni maisha! Ni wakati wa kuamka na kuwa macho Sasa!

2. Muda ni mali! 
Unatumia masaa, siku, miezi, miaka kufanya kazi zako, kutumikia ajira au kufanya biashara zako ukibadilishana na fedha! 
Mara baada ya kufanya MABADILISHANO  kati ya muda wako na shughuli zako utakachokipata ni fedha na siyo muda!

Hii inamaanisha kwamba muda uliopotezwa ni sawa na fedha iliyopotezwa!

Na, kwa wale ambao huwa mnakaa tu pasipokujishugulisha na  chochote kile, mkiamini kwamba wakati wa Mungu ndiyo mzuri mjifunze kitu hapa!
Unatakiwa kujua kwamba wakati wote ni mzuri, kikubwa kuwa na kitu unachokifanya ukibadilishana na muda wako! Kumbuka muda ni fedha!

3. Muda ni maarifa! 
Maarifa yote, ujuzi wote na akili zote ulizonazo mpaka leo hii ni mbadilishano wa muda wote uliotenga katika kujifunza! Kwa mfano kwenda shule pamoja na kujisomea vitabu!
Hii inamaanisha kwamba kadri unavyotumia muda mwingi katika kujifunza, ndivyo unavyokuwa na maarifa mengi zaidi!

Kitu kimoja sana unachopaswa kujifunza hapa ni kwamba, muda uliopotezwa ni sawa na maarifa yaliyopotezwa!
 
4. Muda ni upendo, uhusiano pamoja na familia!
Mapenzi yote unayoonesha kwa watu wote unaokutana nao, kwa mwenzi wako, kwa familia yako upo nao kwa sababu uliwekeza kipindi fulani cha muda katika kuujenga!
Upendo ni hazina kubwa sana ya kuwa nayo!
Kwani kila palipo na upendo huwa hapana uadui katikati yake!
Hata Mimi nakuandikia ujumbe huu ewe mpenzi msomaji kwa vile nakupenda!
Tudumishe upendo ili tuishi maisha yenye mafanikio!

5. Muda ni kila kitu!
Unaweza kuwa chochote kile kutokana na muda, unaweza kufanya chochote kile kutokana na muda, na unaweza kuwa yeyote yule kutokana na muda!

Hii inamaanisha kwamba muda ni kila kitu, na pasipo muda hakuna kitakachotokea katika maisha yako!
Hivyo basi endapo utakuwa na mtizamo wa kuona muda kama kila hutoweza kabisa kupoteza muda wako!

Wewe ni mtu mkuu sana! Ndani Yako unamiliki ukuu sana, lakini kama hautakuwa na utaratibu wa kutumia muda wako vizuri, hakuna chochote kile utakachokipata! 
Muda ni kipindi kinachotumika ili tukio fulani liweze kutokea!
Muda ni mzunguko wa matukio mbalimbali yamhusuyo kila binadamu!
Ni muhimu ukathamini muda wako!

Kumbuka muda hutufundisha thamani ya maisha, ikiwa maisha hutufundisha thamani ya muda!

Na huu ndiyo mwisho wa somo la leo!
Tukutane Kesho kwa ajili ya somo jingine!

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e, mwalimu, mwandishi, muelimishaji katika eneo la maendeleo Binafsi, life coach and consultant!
Unaweza kuwasiliana nami kupitia Whatsapp no +255744284329

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...