Jinsi Ya kufanya Maamuzi Sahihi Kwa Ajili Ya Kesho Yako

Na mwandishi Emmanuel Samuel King'ung'eHivi unafahamu kwamba kile unachoamua kufanya leo ndicho kinachopima vile utakavyokuwa kesho?

Unatakiwa kujua kwamba hapo ulipo na hivyo ulivyo ni kutokana na maamuzi yako mwenyewe!

Aidha uliamua mwenyewe au kuna mtu alikuamlia na wewe ukakosa chaguo mwisho wa siku ukajikuta, ukiamua pasipo kutumia dhamiri yako hali ambayo imekuletea matokeo mabaya!

Kitu kimoja cha msingi unachopaswa ufahamu ni kwamba, ili uweze kupata matokeo ambayo hukuwahi kuyapata ni lazima ukubali kufanya maamuzi ambayo hukuwahi kufanya!

Hata hivyo unatakiwa kujua kwamba siyo kila uamuzi ni uamuzi na siyo kila anayeamua anaamua kwa usahihi!

Kwani kutokuamua ni kuamua pia, maamuzi yasiyo sahihi nayo ni maamuzi pia maamuzi sahihi ni maamuzi!

Sababu kubwa ambayo imetufanya wengi tubaki kuwa watu wa kawaida, ilihali ndani yetu tunamiliki kitu kisicho cha kawaida ni aina ya maamuzi tunayoishia kuyachagua!

Unatakiwa kujua kwamba, haujaumbwa uishie kuwa mtu wa kawaida ila umebaki kuwa mtu wa kawaida kwa sababu wewe mwenyewe umeamua uwe hivyo!

Najua unajiuliza hivi huyu mwandishi anamaanisha nini, kinachomaanishwa hapa ni kitu kidogo sana. Kwamba unatakiwa ubadilishe namna unavyofanya maamuzi ili uweze kabisa kubadili historia ya maisha yako na endapo hutofanya hivyo hakuna chochote cha maana utakachokipata.. 

Huu siyo wakati wa kuendelea kuteseka Tena, huu siyo wakati wa kuendelea kujionea huruma Tena, huu ni wakati wa kuamua upya, lengo kuu likiwa ni  kubadili kabisa maisha yetu!

Je nifanye nini ili nifanye maamuzi sahihi?
Usijalii my friend fanya yafuatayo:

1. Anza Na Mungu Wako Kabla Hujaamua kufanya Jambo Lolote Lile!

Usifanye maamuzi kwa kufuata mapenzi Yako, kwani unaweza ukaharibu mpango wa Mungu aloweka maishani mwako!

Bila Mungu sisi sote si kitu! Mungu pekee ndiye aujuaye mwanzo na mwisho wa kila jambo!

Hii inamaanisha kwamba ukianza na Mungu kabla ya kufanya maamuzi yeye atakupa ishara juu ya mwisho wake!

Hivyo basi endapo mwisho utakuwa mbaya hutoweza kuamua, na endapo mwisho utakuwa mzuri, utaamua na utaishia kupata matokeo mazuri! Kwa Sababu muumba wako katika baraka!

Mbali na hilo unatakiwa kujua kwamba, endapo ukianza na Mungu, yeye atakuongoza pamoja na kukutengenezea njia ambapo mwisho wa siku utapata matokeo mazuri na yenye tija kutokana na maamuzi hayo!

Ndugu mpe Mungu nafasi kwenye maisha yako!

Kamwe usiingie kwenye mahusiano kabla hujaomba kibali kwake!

Kamwe usiingie kwenye biashara yoyote ile pasipo kuomba kibali kwa Mungu wako!

Kamwe usiingie kwenye agano na mkataba wowote ule pasipo kumshirikisha Mungu wako!

Kamwe usiamue jambo lolote lile pasipo kuomba kibali kwa Mungu!

Ndugu epuka kumuweka Mungu pembeni, Kwani ukimuweka Mungu pembeni, yeye naye atakuweka pembeni vivyo hivyo!

Kamwe usitegemee akili zako na Fahamu zako kwa maana zina ukomo!
Mshikrikishe Mungu aujuaye mwanzo wako na mwisho wako!

2. Fafanua Tatizo Unalokutana Nalo!
Ili uweze kufanya maamuzi sahihi ni lazima uweke bayana tatizo unalokumbana nalo! 

Je ni kipi kimekuwa kikisumbua kwa muda mrefu kiasi kwamba kinahitaji ukifanyie maamuzi?
Je ni mahusiano?
Je ni eneo la uchumi na fedha?
Je ni eneo la kukosa kujiamini?
Je ni ndoa uliyonayo?
Je ni kutengeneza kipato cha chini?
Je ni umaskini?
Je ni biashara uliyonayo?

Mpenzi msomaji ni tatizo lipi lililokusumbua kwa muda mrefu sana kiasi kwamba usipoamua utayaweka maishani yako rehani? 

Kumbuka usipolitaja tatizo kwa ufasaha  utaishia kufanya maamuzi yasiyo sahihi, ambapo mwisho wa siku utajikuta hakuna unachokibadili katika maisha yako!

3. Orodhesha Njia  Utakazotumia Ili Kutatua Tatizo Lako!

Ni muhimu kuja na njia nzuri zitakazokusaidia ili uweze kutatua tatizo lako!

Unatakiwa kujua kwamba kila tatizo linatatulika!
Na ukiona hakuna njia ya kutatua tatizo basi hapo hakuna tatizo!

Kila tatizo linatatulika, lakini changamoto itaibuka kutegemeana na njia utakayoamua kutumia kutatua tatizo hilo.

Kwa mfano tufanye hali yako ya kiuchumi haipo vizuri, unapitia changamoto kwenye ndoa Yako, biashara yako haifanyi vizuri n.k 

Halafu unaamua kuanza kunywa pombe, kuiba, kutafuta michepuko pamoja na kukaa tu pasipo kujishughulisha na chochote kile! Omg 😱

Kwa hiyo unataka kumaanisha Kwamba tatizo lako litaisha? 

Huenda kifikra ukaona hizo njia unazotumia ni sahihi, lakini kinachosikitisha zaidi ni pale utakapoona tatizo linabaki palepale na kwenda  katika hatua mbaya zaidi!

Ni lazima ujitafute pamoja na kuja na njia bora zaidi.  Kwa mfano kutafuta maarifa, kutafuta taarifa sahihi, kuomba ushauri, kufanya juhudi zaidi pamoja na kujiboresha kila leo!

Endapo utafanya hivyo lazima utafanya maamuzi sahihi, kutegemeana na changamoto uliyonayo!

Ndugu epuka kutafuta majibu mepesi kwenye mambo magumu!


5. Fikiri Kuhusu Njia Mbada Kabla Hujaamua Kuchukua Hatua Zaidi!

Hata kama utapata njia nyingi kadri ya uwezavyo, bado unashauriwa kufikiri juu ya njia mbadala nyingine unazoweza kutumia ili kutatua tatizo lako!

Ni muhimu kujifanyia tathmini ya kutosha ili uweze kutumia njia sahihi.

Unatakiwa kujua kwamba unaweza ukajua tatizo ni nini, lakini endapo utafanya maamuzi haraka katika kulitatua kwa kutumia njia fulani pasipo kufikiri njia mbadala unaweza ukaishia pabaya!

Kwa mfano kama biashara yako haifanyi vizuri, badala ya kuamua kuuza mzigo wote, unaweza ukaamua kwenda kutafuta maarifa juu ya ujuzi uuzaji na usokoaji!

6. Chagua Njia Mbada Ambazo Unaamini Zitakupa Tulizo La Moyo Na una Amani Nazo.

Ukishapataa njia nyingi mbadala za kutatua tatizo lako, sasa tafuta njia ambazo zinaendana na shauku yako!

Usitumie mbinu ambazo zitaondoa amani ya moyo wako utaishia kuharibu!

Kwa mfano tufanye una changamoto ya mahusiano, na una machaguo mawili tu mbele yako, aidha kuyavunja au kuendelea nayo lakini kwa tahadhari!

Hivyo basi kati ya hayo machaguo mawili uliyonayo, unapaswa ufanye maamuzi ambayo yatakupa amani na tulizo la Moyo!

Epuka kufanya maamuzi ambayo yatakufanya ujiuze kwa gharama ndogo!

7. Chukua Hatua Madhubuti!

Ndugu, hautakiwi tu kuishia kuamua Kwa usahihi, bali unatakiwa kuchukua Hatua!

Unatakiwa kujua kwamba hakuna maamuzi ambayo hujitekeleza yenyewe!

Hii inamaanisha kwamba ni lazima ujizatiti kuchukua hatua ambazo zitafanya maamuzi yako yakuletee manufaa!

Unatakiwa kujua kwamba hatua zitakuwa ni michakato ambazo zitafanya maamuzi yako yaweze kutimia!

Mbali na hilo maisha yetu ni mchakato, hivyo basi ikitokea umechukua hatua halafu hujapata matokeo sahihi, jifunze kutoka kwenye mchakato huo mchakato halafu usonge mbele!

Kumbuka......
Kutouamua ni kuamua pia!

Maamuzi yasiyo sahihi nayo ni maamuzi!

Maamuzi Sahihi ni maamuzi pia!

Nguvu ziko mikononi mwako! Unaamua! Unachagua!
  
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e, mwalimu, mwandishi muelimishaji katika eneo la maendeleo Binafsi, life coach and consultant!

Unaweza ukawasiliana nami kupitia Whatsapp no +255744284329






 

Comments

  1. Ahsante sana! Unakaribishwa sana kwa ajili ya kujifunza zaidi!

    ReplyDelete
  2. Nafrahi sana wa kidato pambana usikate tamaa ujumbe mzuri na una elimisha Jamii

    ReplyDelete
  3. Asante sana mwalimu kuamua ni maamuzi, kutoamua nayo ni maamuzi, kitakachotofautisha watu hawa wawili aliyeamua na asiyeamua ni matokeo tu.

    Pia maamuzi sahihi ni maamuzi pia na maamuzi yasiyo sahihi ni maamuzi pia matokeo ndio yatatofautisha watu hawa wawili

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...