Kile Unachokijua Ndicho Kitapima Umbali Utakaoenda Kimaisha
mwandishi Emmanuel Samuel King'ung'e
Hivi unafahamu kwamba moja ya adui tishio sana wa binadamu katika kizazi hiki tulichonacho leo ni ujinga?
Kama ulikuwa hujui basi leo leo ukweli unaenda kufahamika...
Unatakiwa kujua kwamba hata baba wa taifa hayati Mwl J. K. Nyerere aliutaja ujinga kama miongoni mwa wale maadui watatu wakubwa wa taifa letu pendwa la Tanzania...
Hii inamaanisha ujinga lilikuwa janga la taifa toka enzi hizo...
Lakini cha kushangaza zaidi ni kwamba kadri siku zinavyozidi kwenda mbele ndivyo tatizo hili linavyozidi kukua na kwenda hatua mbaya zaidi...
mategemeo yangu makubwa yalikuwa ni kuisha kwa tatizo hilo kadri siku zinavyozidi kwenda lakini hali imekuwa kinyume chake...
The situation is getting worse as long as the days moves on...
Moja ya kitu ambacho natamani hata leo kingeondoka kwenye jamii yangu ni ujinga..
Natamani ujinga ungeondolewa kwa nguvu zote kutokana na giza linalosababishwa na ujinga hasa kwenye Fahamu za watu wengi...
Unatakiwa kujua kwamba ujinga ni giza nene lililotanda Totoro kwenye Fahamu za Watu wengi.
Hata hivyo ni ukweli usio na kipingamizi kwamba, popote pale palipofunikwa na giza hakuna chochote kile cha maana kitakachotokea...
Na hii kwa sababu giza huashiria kuwa hakuna Nuru, na kama hakuna nuru manake hakuna matumaini.
Hata hivyo kama hakuna matumaini manake hakuna maisha, na kama hakuna maisha manake hakuna maendeleo...
Huenda ukawa unajiuliza huyu kijana mdogo anamaanisha nini?
Okay mimi kama kijana mdogo namaanisha kile kinachomaanishwa...
Anyway tuache masihara maana yangu ni kwamba kuna baadhi ya shida, matatizo, changamoto pamoja na hali ambazo wengi wetu tunapitia zinasababishwa na ujinga wa kutokujua.
Hii inamaanisha kwamba ukosefu wa maarifa ndiyo kimekuwa chanzo cha matatizo hayo yote...
Kuna baadhi ya mambo hayatakaa yabadilike katika maisha yetu na jamii yetu kama tutaendelea kubaki na kiwango kilekile cha ufahamu...
Hii inamaanisha kwamba tutaendelea kupitia matatizo yaleyale kizazi hadi kizazi kama hatutatokomeza ujinga katika jamii yetu...
Huenda nikawa nazungumza jambo ambalo ni geni kwako (yaani hujui maana ya ujinga)... Hata hivyo sipo hapa kuibua na kufanya mjadala uwe mkubwa, Bali nipo hapa kuweka sawa uelewa wako kuhusu neno ujinga...
Kwa mujibu wa Brian Tracy katika kitabu chake kiitwacho "change your thinking change your life", yeye anafafanua ujinga kama ile hali ya kutokujua na kutokujua Kama hujui! Tumeelewana?
Mbali na hilo siyo mbaya endapo tukafafanua maana ya neno mjinga...
Kwa tafsiri nyepesi mjinga ni yule mtu ambaye hajui na hajui kama hajui...
Imagine haujui kuhusu jambo fulani au tatizo fulani au changamoto fulani, au hali fulani unayopitia na ubaya zaidi ni kwamba haujui kama hujui😀😀
Tukirudi katika uumbaji tutaona kwamba Mwenyezi Mungu alimpa kila mtu akili na utashi!
Hivyo basi sitakosea endapo nitasema Mungu hakuumba ujinga, ila ujinga ni matokeo ya juhudi za kutokujifunza zinazofanywa na binadamu mwenyewe..
Na ndiyo maana ukisoma biblia takatifu utakutana na andiko linaosema *"watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa"*
Hii inamaanisha kwamba maarifa ulishapewa ila kutokana na ujinga umejikuta ukikosa kabisa maarifa ya kukusaidia ili uishi kweli ya maish Yako, ndiyo maana kila upande unakutana na vipingamizi na vikwazo kama vyote!
Mpenzi msomaji nakala hii fupi na ikawe kama alamu ya kuamsha fahamu zako nawe uanze kupiga vita ujinga...
Unatakiwa kujua kwamba kile Unachokijua ndicho kitapima umbali utakaoenda kimaisha!
Hii inamaanisha kwamba ukijua vingi utaweza kufika mbali kimaisha!
Ilihali ukijua vitu vichache hutafika mbali kimaisha...
Hata hivyo Unatakiwa kujua kwamba mbinu kubwa ya kupambana na ujinga ni kupitia kujifunza!
Na ndiyo maana sisi wanafalsafa tunaamini kwamba siku utakayoacha kujifunza ndiyo siku ya kifo chako, Kwani utajizika kwa kujichimbia kaburi lako mwenyewe...
Na hii ni kwa sababu ubongo wako utaanza kuzalisha mawazo yaliyokufa au yaliyopitwa na wakati!
Kutokana na ukweli huo hapa ndipo huwa tunapata aina mbili za watu!
Aina ya kwanza ya watu ni wale watu ambao wanaishi lakini wamekufa.
Na aina ya pili ya watu ni hujumuisha watu ambao wamekufa lakini bado wanaishi!
Ukitaka uishi ukiwa hai huna budi kujifunza...
Yes boss jifunze kujifunza!
Unatakiwa kujua kwamba unaweza kujifunza kupitia social medias (Facebook, Whatsapp, Instagram, Twitter n.k), kusoma vitabu, kuhudhiria semina mbalimbali, kusikiliza audio books, kujifunza kupitia podcast, CD, audios mbalimbali n.k.
Ndugu unatakiwa ufahamu kwamba kila eneo la maisha yako linahitaji uwe na maarifa fulani ili uweze kulikabili ipasavyo...
Kumbuka kadri unavyojua kuhusu jambo fulani ndivyo na hofu ya kufanya jambo hilo inavyopungua, ikiwa kadri usivyokuwa na uelewa wa jambo hilo ndivyo na hofu ya kufanya jambo hilo inavyoongezeka!
Wakati mwingine mimi na wewe hapo hatuna budi kufahamu kwamba, hatuna: umaskini, hali ngumu, maradhi, changamoto, dhiki pamoja na matatizo mengine mengi, bali tuna ujinga mwingi vichwani mwetu kuhusu mambo hayo!
Kwamba hatuna uelewa wa kutosha juu ya mambo hayo..
Ndugu huenda ukawa umeona pengine labda una mikosi, nuksi, laana, .nk.
Na huenda ukawa umehama mpaka mtaa, kijiji, wilaya mkoa, mpaka nchi unayoishi na umeona hakuna kitu kinachobalika mbali na kuwa umehama...
Hata hivyo huenda ukawa umebadili mpaka kazi na biashara na haujaona mabadiliko yoyote yale usijue shida nini!
Kumbe tatizo halisi lipo kichwani mwako!
Unahitaji uamuzi mmoja tu... Ambao ni huu hapaa...
ANZA KUJIFUNZA!
YAANI JIFUNZE KUJIFUNZA!
Kesho nitakuletea aina tano za ujinga zilizopo miongoni mwetu...
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; mwalimu, mwandishi, muelimishaji katika eneo la maendeleo Binafsi, life coach and consultant!
Unaweza kuwasiliana nami kupitia Whatsapp no +255744284329
Great I appreciate your articles sir
ReplyDeleteKaribu sana! Usisite kutembelea blog hii pendwa
ReplyDelete