Jinsi Watu Huitikia Kuhusu Matatizo...

1. Kulidharau
Hawa Ndiyo Wale Watu Huamua Kusema “Liwalo Na Liwe”, Jaribu Kufikiri Kuhusu Kitu Kinahusu Maisha Yako Halafu Unaamua Kukipuuzia Kwa Kusema Liwalo Na Liwe Vipi Kama Halitakuwa?
Na Vipi Kama Litaleta Matoke Mabaya? 
Unafikiri Hayo Matokeo Yatamkuta Nani Kama Siyo Wewe Mwenyewe? Unahitaji Kufikiri Juu Ya Hili…

2. Kulaumu
Sasa Aliyekuambia Kulaumu Hubadili Kilichotokea Ni Nani? Hakuna Kiwango Cha Lawama Ambacho Hutatua Tatizo… 
Hii Si Njia Sahihi Ya Kulikabili Tatizo Kwani, Kulaumu Ni Kitu Kingine Na Kutatua Tatizo Kingine, Acha Kulaumu Kabili Tatizo Kwa Njia Sahihi.

3. Kuwekeza Juhudi Na Nguvu Kubwa Kwenye Tatizo…
Yaani Badala Ya Kuweka Juhudi Kutafuta Chanzo Cha Tatizo Wewe Unaweka Juhudi Kwenye Kukikabili Kilichotokea.
Je Ni Kwamba Hautambui Kwamba Kila Matokeo Yana Kichocheo Ambacho Hupelekea Kutokea Kwake?
Na, Kama Unatambua Kwanini Unahangaika Na Kilichotokea Na Siyo Kuhangaika Na Kile Kilichopelekea Kutokea Kwake?

Ndugu Ili Utatue Changamoto Unatakiwa Urudi Kwenye Chanzo Kilichopelekea Kutokea Kwa Tatizo, Hilo… Rudi Kwenye Kichocheo. Kumbuka Kila Kitu Hutokea Kutokana Na Sababu…

4. Kulihofia Tatizo
Hivi Ushawahi Kusikia Mtu Katatua Tatizo Kwa Kulihofia? …Ndiyo Upo Sahihi Jibu Ni Hapana… Labda Hofu Itakuwa Ilimfanya Mtu Huyo Asipate Ule Ujasiri Na Hamasa Ya Kulikabili Tatizo Hilo. Na, Akaona Kama Ameshatatua Tatizo Kwa Kutolikabili, Asijue Kwamba Tatizo Liko Palepale…
Ndugu Hofu Huwa Haitatui Tatizo Bali Hulifanya Liende Hatua Mbaya Zaidi..

Jinsi Ya Kutatua Matatizo Hatua Kwa Hatua...

Endapo Itatokea Siku Umeulizwa Kazi Yako Kubwa Hapa Duniani Ni Ipi Sema Mimi Ni Mtatua Matatizo…
Yes, Wewe Ni Mtatua, Matatizo Kwa Sababu Matatizo Ni Sehemu Ya Maisha Yako, Na Hakuna Siku Utakuja Kujihakikishia Kwamba Hutokutana Na Matatizo Tena…
Unatakiwa Kujua Kwamba Watu Ambao Hawakutani Na Matatizo Wapo Makaburini Wamelala Tulii...

Maadam Uko Hai Matatizo Yataibuka Tu, Na Ifahamike Kwamba Matatizo Hayo Hayataibuka Kukukwaza Bali Yataibuka Ili Kutangaza Ukuu Wako Na Uwezo Wako Kama Utayatatua… 

Hata Hivyo Huna Budi Kufahamu Kwamba, Maisha Yako Yatakuwa Ni Mpokezano Wa Matatizo Tu Kadri Siku Zinavyozidi Kwenda Mbele. Yaani Hujakaa Sawa Linatokea Hili, Mara Linaibuka Lile Yaani Ili Mradi Tu Uteseke Ahahahahahahahahahahahahahaahhh…

Hata Hivyo Hijalishi Utakutana Na Yapi Wewe Jiaminishe Kwamba Utayakabili Na Utayatua Matatizo Hayo Kwani Matatizo Yote Hutatulika…
Matatizo Yapo Kutupa Ladha Ya Maisha, Utakuja Waambia Nini Watu Kuhusu Mafanikio Yako Kama Hutapitia Matatizo? Jaribu Kufikiri Tu!

Hata Hivyo Unatakiwa Kujua Hakuna Atayekuja Kutatua Matatizo Yako Pasipo Uhusika Wako…
Na, Kama Hutatatua Matatizo Yako Mtu Mwingine Atakutatulia Huku Ukitakiwa Umlipe? Sasa Kwanini Umlipe Mtu Wakati Uwezo Wa Kutatua Unao?

Ndugu, Zingatia Hatua Zifuatazo Katika Kutatua Matatizo Yako:
1. Libaini Tatizo
Ili Uweze Kutatua Tatizo Kwa Njia Sahihi Ni Lazima Uanze Kubainsha Tatizo Linalokukumba. Unapaswa Ulibainishe Kwa Ubayana. 
Kumbuka Huwezi Ukaja Na Njia Za Kutatua Kitu Ambacho Hata Wewe Mwenyewe Hukijui.
 Katika Hatua Hii Unatakiwa Ubainishe Matatizo Yote Unayokumbana Nayo Kwa Mfano: Kiafya, Kielimu, Kiuchumi, Kiuwekezaji, Kikazi, Kiroho Na Mengine Kama Hayo.

2. Lifafanue Tatizo Hilo
Ni Muhimu Ukafafanua Kwanini Unaona Hilo Ni Tatizo.
 Endapo Utalifafanua Vizuri Utapata Njia Sahihi Za Kulikabili.
Je Ni Kwa Vipi Unaona Hilo Ni Tatizo Na Je Linakuletea Athari Katika Kuishi Kwako?…

3. Jitoe Kwenye Tatizo
Ili Uweze Kutatua Tatizo Ni Lazima Ujitoe Kwanza Kwenye Tatizo. 
Ukijiweka Kuwa Sehemu Ya Tatizo Hutatatua Tatizo Bali Utasababisha Tatizo.
 Hata Kama Ni Wewe Mwenyewe Ndiye Uliyepelekea Kutokea Kwa Tatizo Basi Jiondoe Kuwa Sehemu Ya Tatizo. 
Maana Yake Ni Kwamba Ukijiondoa Kuwa Sehemu Ya Tatizo, Utakuwa Sehemu Ya Kutatua Tatizo Hivyo Hata Mtizamo Wako Kuhusu Tatizo Utabadilika, Nawe Utafanikiwa Kutatua Tatizo Hilo Kwa Vile Wewe Siyo Sehemu Ya Tatizo Tena Bali Ni Suluhu Ya Tatizo Hilo…

4. Tafuta Njia Za Kutatua Tatizo
Kila Tatizo Hutatulika… Na Ukiona Hakuna Njia Za Kutatua Tatizo Basi Hapo Hakuna Tatizo.
Unatakiwa Uje Na Orodha Ya Njia Mbalimbali Utakazotumia Ili Uweze Kutatua Tatizo Hilo. 
Tumia Njia Hii, Inaitwa Brainstorming Yaani Ujiulize Swali Moja Halafu Njoo Na Orodha Ya Majibu Kama 20 Hivi Yakayojibu Swali Hilo. 

5. Tatua Tatizo
Sasa Hapa Ndipo Uchague Njia Nzuri Na Sahihi Utakayotumia Kutatua Tatizo. 
Unatakiwa Ujue Kwamba Hatua Moja Iliyochukuliwa Ina Thamani Zaidi Ya Mipango 1000 Ambayo Haijaanza Kufanyiwa Utakelezaji.
Hata Hivyo Njia Nzuri Ya Kutatua Tatizo Ni Kuanza Kwenye Chanzo Cha Tatizo. 
Kwamba Urudi Ukadhibiti Chanzo! Ukiweza Kudhibiti Chanzo Tatizo Linakuwa Limeishia Hapo!  

6. Weka Kumbukumbu
Ni Muhimu Kuweka Kumbukumbu Kuhusu Tatizo Na Jinsi Ulivyotatua Ili Na Wenzako Kama Watakumbana Na Tatizo Kama Lako Watumie Mbinu Ileile Ambayo Wewe  Uliitumia Kutatua.
Hata Hivyo Ni Muhimu Kuweka Kumbukumbu Kwani Hii Itakusaidia Kesho Endapo Utakutana Na Tatizo Kama Hilo Uweze Kulitatua Kwa Kutumia Njia Moja.

Hitimisho: Kuna Wakati Mwingine Hatuna Matatizo Bali Tuna Ujinga.
Na Ujinga Ndicho Chanzo Kikubwa Cha Matatizo, Kwani Ujinga Ni Giza, Na Palipo Na Giza Hapana Matumaini, Na Kama Hakuna Matumaini Maana Yake Pana Matatizo Na Kama Pana Matatizo Maana Yake Hapana Maisha!
Kwa Hivi Ni Muhimu Kutafuta Maarifa Kila Iitwapo Leo...

Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya.

Ndimi Emmanuel Samuel King’ung’e; Mwl, Mwanishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!

Unaweza kuwasiliana name kupitia WhatsApp no +255744284329, au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com 

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...