Jinsi Ya Kuanza Upya Tena mbinu ya pili

2. Rudi kwenye chanzo chako
"Ee bwana umenichunguza na kunijua, Wewe wajua kuketi kwangu na kuondoka kwangu;  
Umelifahamu wazo langu tokea mbali". Zaburi 139
"Kabla sijakuumba katika tumbo la mama yako nalikujua na kabla hujatoka tumboni nalikutakasa"… “Yer 1:5”. 

Nimeanza na hiyo mistari miwili ili ujue kwamba kuna yule ambaye anakujua wewe kuliko hata wewe mwenyewe unavyojijua.
Kwamba ukirudi kwake ukajikabadihi naye atakuongoza na kukupeleka kule anakotaka akupeleke, kwani yeye ndiye aujuaye mwanzo na mwisho wako. 

Na, ndiyo maana isaya 48:17 neno la BWANA linasema “BWANA, mkombozi wako, mtakatifu wa Israel, asema hivi, Mimi ni BWANA, MUNGU wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongazaye kwa njia ikupasayo kuifuata.

Unatakiwa kujua kwamba mawazo yetu pamoja njia zetu si kitu kwani huwa na ukomo, kwamba unaweza ukazifuata na usifike popote pale kwa sababu hujaanza na Mungu.

Na, ndiyo maana, Isaya 55:8-9 inasema kwamba “maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zangu zenu si zangu; asema BWANA, kwa maana kama mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu ziko juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu”

Hata hivyo, unaweza ukajiona wewe pekee unaweza na hivyo ukaamua kufuata njia zako ukaishia mautini... 
Na ndiyo maana mithali 14:12 neno la BWANA linasema, “iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, lakini mwisho wake ni njia za mauti”.
 Unachotakiwa kujifunza hapa ni kwamba huenda ulitumainia njia zako ambazo mwisho wa siku zimekupeleka kwenye mauti na siye kule ulikopaswa uende, na ndiyo maana ninakusihi uanze upya ukiwekeza kwa Mwenyezi Mungu pamoja na kumtumainia yeye peke…

kwa kutambua umuhimu wa kuweka tumaini kwa Mungu ndiyo maana mwandishi wa kitabu cha mithali anasema, “mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, wala usitegemee akili zako mwenyewe”. mithali 3:5

Unatakiwa kujua kwamba chanzo cha maarifa yote ni Mungu! kwanini utegemee akili zako pekee ilihali zina ukomo? Jaribu kufikiri tu…

Hebu muulize Mungu wako juu ya sababu ya kuachilia uumbwaji wako, kwa maana mawazo yake na fahamu zake hazichunguzuki. 
Hebu muombe hekima na akili ikusaidie katika kuishi kweli ya maisha yako!

Na, ndiyo maana hata yakobo 1:5 neno la BWANA linasema “lakini mtu kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei, naye atapewa”

Ndugu huu ni wakati wa kurudi kule kilipo chanzo chako! Mungu pekee ndiye chanzo halisi kwani yeye ndiye anajua kwanini alikuumba! Lazima utafute sababu ya kuumbwa kwako.

Anza upya kwa kumuomba Mungu Kwanza kumbuka Hesabu 23:19
Neno la Mungu linasema "Mungu si mtu, aseme uongo; 
Wala si mwanadamu, ajute; 
Iwapo amesema, hatalitenda? 
Iwapo amenena, hatalifikiliza?"

Yakabidhi maisha yako yote kwake naye atajua akupeleke wapi. 
Huwezi ukaanza upya pasipo Mungu, kumbuka Mungu humpa kila mtu aombaye kwani Mungu siyo kiziwi kwamba hasikii..
Nitaondoka, nitakwenda kwa baba yangu… luka15:18.

Mpendwa rudi kwa baba yako kwani kule ndipo lilipo tumaini, uhuru, Amani, mafanikio na furaha ya kweli…

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; mwalimu, mwandishi muelimishaji katika eneo la maendeleo Binafsi, life coach and consultant!

Unaweza kuwasiliana nami kupitia Whatsapp no  +255744284329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...