Jinsi Ya Kuanza Upya Tena... Mbinu ya Tano


5.Tafuta Maarifa Mapya Kila Leo......
Tunaishi kwenye dunia inayobadilika kila leo hivyo sote tunatakiwa tuwe wanafunzi kwamba tujifunze kila iitwapo leo. 
Unatakiwa kujua kwamba kama hauna taarifa sahihi utapoteza uelekeo, kama haujitengenezi kuwa bora basi unazidi kuharibika.
 Kama haufanyi jitihada katika kujiboresha basi utapitwa na wakati…
Mifumo iliyotutengeneza kuna wakati imetufunza mambo ya kizamani kiasi kwamba mtu unahitimu hata shule ukiwa na taarifa za zamani! 

Hebu vuta picha umefundishwa kupitia mtaala wa zamani, old school curriculum ni kipi kipya utakifanya kwenye dunia hii ya kisasa?
Kanuni ya kitokacho na kiingiacho inasema kwamba "kitakachotokea kitakuwa sawa na kilichoingia"

Hii inamaanisha kwamba utafanya mambo fulani kutegemeana na maarifa yaliyoingizwa kichwani mwako!
Jaribu kufikiri tu, ni kipi utakifanya kwenye hii dunia ya kisasa ilihali kichwani mwako kuna mafaili ya zamani! 
Hebu vuta picha umepewa maarifa ya dunia iliyokuwepo 1800 halafu wewe upo 2023, je utatumiaje maarifa ya 1800 kwenye dunia yetu ya 2023?
Je mpaka hapo unaona kuna ulazima wa kung'ang'ania maarifa ya zamani?
Bila Shaka Jibu ni hapana, kwani dunia ya sasa siyo sawa na ya kipindi hicho!

Na, kama ni hivyo kwanini usijizatiti kutafuta maarifa ili uwe wa kisasa zaidi, kwanini uishi kama mhenga my friend?

Hebu vuta picha vile ulikubali kutumia zaidi miaka 18 kutafuta elimu ya kitaaluma, baada ya hapo ukahitimu, lakini soko likashindwa kutambua ulichosomeaa…

Kwamba mbali na kuwa umehitimu ila ulichosomea hakitajiki Tena...

Sasa kwanini usitenge hata miaka miwili utafute marifa mapya ambayo yanaendana na kile dunia ya sasa inataka? 
Kama ulikubali kutumia zaidi ya miaka 18 kwenye elimu ya kitaauma, je utakosa kutenga hata miaka miwili uanze upya kwa kutafuta maarifa muafaka? 

Ninaamini inawezekana kabisa ndiyo maana niko hapa kukusihi!
Vilevile unatakiwa kujua kwamba, endapo hutaamua kufanya hivyo hakuna kitu kitakachobadilika katika maisha yako…

Hata hivyo unatakiwa kujua kwamba unakuwa kutokana na kile unachoulisha ubongo wako. 

Mbali na hilo na ifahamike kwamba, kile unachokijua ndicho kitapima umbali utakaoenda!
Kwamba, ukitaka usifike mbali kimaisha usitafute maarifa, ikiwa ukitaka kufika mbali kimaisha tafuta maarifa mapya! 
Uamuzi ni wako kwani unaamua! Unachagua!

Sisi wanafalsafa tunaamini siku utakayoacha kutafuta maarifa ndiyo itakuwa siku ya kifo chako, kwani ubongo wako utaanza kuzalisha mawazo ambayo yatakuwa hayaishi, na kama ubongo wako utazalisha mawazo yasiyoishi utaniaminishije kwamba wewe uko hai na unaishi?

Huu si wakati wa kuendelea kushikilia ya zamani tena, huu ni wakati wa kujifunza mapya. 
Kwani huwezi ukaleta matokeo mapya kama hutojifunza mbinu mpya…

Jifunze kila leo, ulimwengu tulionao leo siyo wa kutumia nguvu tena, bali ni ulimwengu wa kutumia akili, kwamba siyo wale wenye nguvu ndiyo wafanikiwao bali ni wale wenye akili ndiyo wafanikiwao!

Akili unazipataje? Ni kupitia kujifunza.
 Na, ndiyo maana leo nimekuja hapa kukusishi ujifunze ili uweze kuanza upya ukiwa na maarifa sahihi pamoja na taarifa sahihi! 

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e, mwalimu, Mwandishi Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!

Unaweza kuwasiliana nami kupitia Whatsapp no +255744284329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...