Jinsi ya kupata matokeo unayoyataka…

Hivi unafahamu kwamba asilimia kubwa ya watu hushindwa kupata matokeo mazuri juu ya kile wanachokitaka na wengine huishia kupata matokeo yaliyo kinyume kabisa hasa ukihusisha na yale matokeo wanayoyataka?

Huenda na wewe umekuwa miongoni mwa watu hawa, ambao wameshindwa kupata matokeo ya kile wanachokitaka kwa asilimia zote, au wamepata kinyume chake.

Unatakiwa kujua kwamba watu wengi wanajua wanachokitaka lakini hawajui jinsi ya kukipata, kutokana na hilo hujikuta wakitumia mbinu zisizokuwa sahihi katika kutafuta kile wanachokitaka mwisho wa siku wanaishia kutokupata kitu chochote kile.

Mbali na hilo katika kuishi kwetu tuna lile kundi kubwa la watu ambalo lenyewe halijaweka wazi juu ya kile linachokitaka kukipata, hii inamaanisha kwamba kwa sababu hawajakusudia kitu hawawezi kupata matokeo juu ya kitu kisichokusudiwa! 

Kwani katika hali ya kawaida huwezi ukakipata kitu ambacho hukitafuti hata kama kitakuwa katika mazingira uliyopo…

Unatakiwa kujua kwamba ukiweka wazi kile unachokitaka utajikuta ukipata hamasa kubwa, ukipokea nguvu mpya, ukipata maono mapya pamoja na kuyafanya maisha yako yawe na kusudi. 

Kutokana na hilo hutaishi tu kwa sababu uko hai, bali utaishi kwa sababu kuna jambo linalokufanya uishi, nalo ni moja tu yaani lile jambo unalotaka ulitimize, kwamba utawekeza juhudi zote mpaka ulipate...

Je Nifanye Nini Ili Niweze Kupata Matokeo Ninayoyataka?...

Usijali ndani ya muda mfupi ujao unaenda kubadilisha kabisa historia ya maisha yako, kupitia  kusoma tu, Makala hii fupi iliyoandikwa kwa ustadi mkubwa…

Ili uweze kupata matokeo unayoyataka fanya yafuatayo:

1. Weka Wazi Kile Unachokitaka…
Lazima ueleze kwa uwazi kile unachokitaka! Na, endapo itatokea kitu hicho ni cha aina nyingi kielezwe aina yake, vilevile kama ni cha idadi kidokezwe idadi yake! 

Kwa mfano ninaweza kuweka wazi kile ninachokitaka kwa kusema “ninataka kukuza pato langu la mwezi lifike 300,000/=” hapa wazo langu limeelezwa kwa uwazi na akili yangu imelipokea kwa mikono miwili kile ninachokitaka…

Hii inamaanisha akili yangu kwa muda wote itakuwa inachakata kipi nifanye ili niweze kupata matokeo hayo ninayoyataka.

Kwa mantiki hiyo nitakuwa napambana kwa sababu kuna kitu ninachokitaka kwenye mapambano yangu, kwamba sitokuwa nimetingwa pasipo kukusudia kitu, bali nitakuwa nimetingwa kwa sababu kuna kitu nimeazimia kukipata kwenye juhudi zangu nizifanyazo.

Bila shaka katika kuishi kwako, ushawahi kukutana na watu ambao katika kuishi kwao huwa wanakuwa wametingwa muda wote, lakini ukiwafuatilia hakuna hatua yoyote ile waliyoipiga, watu hawa wamefanikiwa katika kufanya juhudi lakini hakuna chochote kile walichokilenga kukipata kwenye juhudi zao, na, ndiyo maana mbali na kufanya juhudi nyingi mwisho wa siku wamejikuta hakuna hatua ya maana wanayoifikia. 

Usipoweka wazi unachokitaka maana yake utaishia kutapanya kabisa nguvu zako katika kufanya mambo mbalimbali mwisho wa siku utajikuta hakuna chochote kile unachokipata mbali na kuwa unapambana…

Ndugu, weka wazi kile unachokitaka ukipate, kifanye kipokelewe akilini mwako, baada ya hapo wekeza juhudi nyingi mpaka ukipate.

Na endapo utafanya hivyo, nakuhakikishia kwa asilimia zote utapata matokeo unayoyataka.

Mbali na hilo ikitokea ukawa una orodha ya mambo mengi unayoyataka basi unapaswa uyafanyie utekelezaji kwa kuweka vipaumbele. Kwamba leo anza na jambo hili kesho maliza na jambo jingine! 

Epuka kabisa kufanya mambo yote pamoja utashindwa kupata matokeo unayoyataka.

Je ni kipi unachokitaka katika maisha yako? Kumbuka usipoweka wazi kile unachokitafuta yale usiyoyataka ndiyo yatachukua nafasi katika maisha yako!
Weka wazi kile unachokitaka ndipo sasa ukipate!

Mbinu ya pili kuhusu jinsi ya kupata matokeo unayoyataka itatumwa kesho! Usipange kukosa!

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!

Unaweza kuwasiliana nami kupitia Whatsapp no+255744285329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...