kila Mtu Kaumbwa Kwa kusudi Fulani

Na Emmanuel Samuel King'ung'eHivii unafahamu kwamba kila mtu ameumbwa kwa ajili ya kutimiza kusudi Fulani hapa duniani?
Unatakiwa kujua kwamba hujaumbwa uje uishie kuwa mzururaji au msindikizaji tu hapa duniani, bali kuna sababu iliyomfanya Mungu aachilie uumbwaji wako!
Hii inamaanisha kwamba, hiyo sababu ilikuyokuwepo nyuma ya pazia iliyopelekea kuumbwa kwako, ndiyo ilibeba kusudi halisi la wewe na maisha yako! 

Vilevile unatakiwa kujua kwamba pasipo kujua kusudi lako hutouishi ukuu wako, bali utaishia kuwa mtu wa kawaida tu, ilihali umebeba kusudi lisilo la kawaida kabisa ndani Yako! 

Hivyo basi, kutokana na ukweli huo unatakiwa kujua kwamba, hukuumbwa kwa bahati mbaya, bali uliumbwa ili uje uwe mtu mkuu na mtatua matatizo ya watu! 
Kamwe usimlaumu Mwenyezi Mungu kwa kuumba (huenda ukawa unapitia magumu na mateso mengi sana hivyo unaamua kuachilia lawama), bali jilaumu mwenyewe kwa kutokutafuta na kugundua kusudi la kuumbwa kwako!

Unatakiwa kujua kwamba hapa duniani hakuna mbadala wako, yaani hakuna mtu kama wewe, na hatatokea mtu mwingine atakayekuwa kama wewe. 

Na, kama hakuna mtu kama wewe isipokuwa wewe pekee, hii inamaanisha kwamba, hakuna mtu aliyebeba kusudi sawa na wewe!

Kutokana na hilo unatakiwa kujua kwamba hatua ya kwanza ya wewe kuwa wewe pamoja na kuonesha upekee wako ipo kwenye kugundua kusudi la kuumbwa kwako!

Mpenzi msomaji unatakiwa kujua kwamba maisha bila kusudi si kitu, bali ni utumwa na mateso yasiyokuwa na faida yoyote ile!

Sababu kubwa inayotufanya watu wengi tuteseke sana maishani mwetu, ni kwa sababu hatujaweza kutambua kusudi la kuumbwa kwetu, kutokana na hilo tunajikuta tukishindwa kufanya yale tupaswayo kuyafanya mwisho wa siku tunaishia kuteseka tu...

Ndugu huu siyo wakati wa kuendelea kuteseka Tena!  Kuteseka kwetu kumetosha Sasa, huu ni wakati wa mimi na wewe kuamua kuanza kulitafuta kusudi la kuumbwa kwetu!

Unachopaswa kujua ni kwamba, kama hutolitambua kusudi la kuumbwa kwako, hakuna atakayejishughulisha kugundua kusudi la maisha yako!
Na, endapo hutalitambua kusudi la kuumbwa kwako unatakiwa kujua kwamba, utawafanya watu wengine waishi maisha magumu!

Hii ni kwa sababu kusudi la kuumbwa kwako lipo kwa ajili ya kuwasaidia watu wengine!
Na ndiyo maana hata ng'ombe hawezi kunywa maziwa yake mwenyewe, au hata mti hauwezi kuyala matunda yake wenyewe ijapokuwa wenyewe ndiyo umeyazalisha matunda hayo!

Je, wewe umeshaanza kulifanyia kazi kusudi lako?
Je, unahisi unafanya kile ulichoumbiwa uje ukifanye?

Unatakiwa kujua kwamba usipoliishi kusudi la kuumbwa kwako, utafanya watu wengine waishi maisha magumu...
Hii ni kwa sababu huenda kuna maelfu ya watu inatakiwa waje wainuliwe kupitia kusudi la kuumbwa kwako! 

Ukiwa katika kuendelea kujipa tathmini jiulize swali hili, je ni kwa kiasi gani nimechangia watu waishi maisha magumu kutokana na kutokutambua kusudi la kuumbwa kwangu?

Bila shaka jibu umelipata.. 

Ukiachilia mbali hilo, unatakiwa kujua kwamba kuna kusudi na kuna kazi, na huenda kusudi lako lisifanane kabisa na kazi unavyofanya pamoja na kozi uliyosomea, kwani hivyo vyote vimetokana na mifumo uliyoikuta hapa duniani na siyo Mungu!

Ndugu yangu kwanini uishi kinyonge, kwa kushindwa kulitambua kusudi la kuumbwa kwako? 

Imetosha Sasa Ndugu yangu...
Huu ni wakati wako muafaka wa kugundua kusudi la kuumbwa kwako...

Ndugu msomaji unatakiwa kujua kwamba hapa duniani watu hupambana sana, lakini kama utakuwa unapambania masuala mengine na siyo kusudi lako utaishia kuteseka tu...

Nilipofanya uchunguzi kuhusu kusudi niligundua kuwa kuna watu wa aina mbili, yaani:

Watu wa kawaida, hawa ni wale watu ambao hupambana sana katika kutekeleza ndoto zao, malengo yao pamoja na matarajio yao wakiamini hivyo vitu huenda ndilo kusudi lao!

Watu wenye busara, hawa ni wale watu ambao hutumia sehemu kubwa ya muda wao katika kujitafuta mpaka kulijua kusudi la kuumbwa kwao! 
Je kati ya hayo makundi mawili wewe unadondokea kundi lipi?
Bila shaka jibu umelipata tayari...

Najua unajiuliza nifanye nini ili nigundue kusudi langu?
Nami sina blabla nyingi, bali nipo hapa kukusihi, urudi kwenye chanzo chako, yaani mrudie Mungu wako!

Yes, boss Rudi kwa Mungu wako Kwani yeye ndiye anajua kwanini alikuumba, anajua kipaji chako, anajua uwezo wako na anajua kabisa kipawa kilichopo ndani Yako..

Mpenzi msomaji unatakiwa kujua kwamba Mungu pekee ndiye ajuaye kwanini alikuumba! 

Ukipata muda kasome yeremia 1:5, neno la BWANA linasema;
'Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa". 

Kumbe yeremia huenda alijiona kwamba yeye ni mtu wa kawaida tu, ni kama vile mimi na wewe tunavyojiona leo hii..

Lakini cha ajabu Mungu akasema  nimekuweka kuwa nabii wa kimataifa!
Mungu anasema na wewe siku ya leo kwamba amekufanya uwe mtu mkuu!

Kama utakuwa unaweza kuhusianisha matukio utakuwa ushagundua kwamba, Mungu alimuumba yeremia ili aje awe nabii wa kimataifa...

Na, kama Mungu alimuumba yeremia kwa kusudi kuu kama hilo, inamaanisha kwamba hata wewe alikuumba kwa kusudi kubwa sana, kwani yeye hana upendeleo bali humkrimia kila mtu kwa kadri ya mapenzi yake!

Ndugu kuanzia saa hii jiunganishe na Mungu wako!

Huenda ulikuwa umetumainia njia zako na akili zako, pamoja na mifumo ya dunia hii lakini havijakusaidia kitu!

Leo nipo hapa kukusihi urudi kwenye chanzo chako!

Yes, rudi kwenye chanzo chako kwa kuanza kumhoji Mungu alikuumba uje utumike katika eneo gani na ukiwa kama nani?

Kila saa anza kumhoji Mungu wako kuwa ninaweza nikafanya nini hapa duniani?

Vilevile unatakiwa kumhoji Mungu wako juu ya ule uwezo aloweka ndani Yako, utakaokusaidia uweze kuliishi kusudi la kuumbwa kwako!

Haya yote utayajua endapo utaanza kumhoji Mungu wako, na usipomhoji kamwe huwezi ukapata majibu! Sahau kabisa..

Ndugu usimpuuze Mungu, bali mpe Mungu nafasi kwenye maisha yako! 

Kamwe usikae mbali naye kwani yeye ndiye anayekujua wewe vizuri kuliko hata wewe mwenyewe unavyojijjua...

Zaburi 139, Neno la BWANA linasema,
"Ee BWANA, umenichunguza na kunijua. 
Wewe wajua kuketi kwangu na kuondoka kwangu; 
Umelifahamu wazo langu tokea mbali"

Mistari hii inatufundisha kitu kikubwa sana, kwamba kuna yule anayetujua pamoja na kufahamu mawazo yetu tokea mbali..

Na, Kama mwenyezi Mungu ndiye anayekujua wewe zaidi kuliko hata wewe unavyojijjua kwanini usijiunganishe kwake ili upate kujijua?

Wakati uliokubalika ndiyo sasa, jikabidhi mzima kwa Mungu wako...
Ndugu unatakiwa utafute kusudi la kuumbwa kwako!

Kwa ujumla unatakiwa ujue kwamba, kama aliyetengeneza kisu alivyotambua kusudi la kutengeneza kisu (matumizi yake), vivyo hivyo na Mungu naye ameweka kusudi fulani maisha Mwako! 
Hii inamaanisha kwamba, Mungu pekee ndiye anayefahamu kusudi la kukuumba!

Hivyo basi huna budi kumtafuta Mungu, kwa juhudi zako zote na bidii zako zote kwani yeye katu hatadiriki kukutafuta wewe!

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; mwandishi, mwalimu, muelimishaji katika eneo la maendeleo Binafsi life coach and consultant!

Unaweza kuwasiliana nami kupitia Whatsapp no +255744284329
 

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...