Kutoka 100% Hadi 0%Jinsi Ya Kuanza Upya Tena…
Hivi unafahamu kwamba karibu kila binadamu katika kuishi kwake huwa anafika hatua fulani na kuona ni bora kuanza upya kuliko kuendelea kuishi kimazoea, huku akiwa hana cha maana anachokipata kutokana na mwenendo wake wa kuishi?
Huenda hata wewe hapo ukawa uliweka matarajio makubwa sana kuhusu maisha yako, kwamba ulitarajia uje uishi maisha mazuri yenye furaha, Amani pamoja na mafanikio, lakini umejikuta muda unazidi kwenda mbele na hakuna chochote kile cha maana kinachotokea maishani mwako…
Nafahamu ni jinsi gani hali hii inakuumiza, kwani mbali na kufanya juhudi kubwa sana pamoja na kujitoa kwako kwa asilimia zote, mwisho wake umejikuta unaishia kuambulia patupu…
Huenda ulikuwa na matarajio murua kabisa kuhusu mahusiano yako cha ajabu umejikuta upo kwenye mahusiano ambayo hata hujui yanahusiana na nini…
Huenda ulikuwa na matarajio mazuri sana kuhusu kipato unachotaka kutengeneza kwa mwezi, lakini mwisho wa siku unaishia kuambulia patupu…
Huenda ulikuwa una matarajio makubwa sana kuhusu uwekezaji lakini hakuna cha maana kinachoendelea…
Huenda ulikuwa na matarajio makubwa kuhusu mali utakazomiliki, lakini hakuna chochote unachokimiliki zaidi ya kumiliki shida pamoja na kumilikiwa…
Huenda ulikuwa unautaka mwisho mzuri wa maisha yako, yaani maisha yako yawe yenye furaha, Amani na mafanikio lakini umeishia kuambulia huzuni karaha na mateso…
Yes, huwa inatokea kwamba unakuta mavuno ni kidogo lakini juhudi unazozifanya pamoja na mipango uliyoiweka ni mikubwa sana...
Kwamba umefanya baadhi ya mambo na umefikia asilimia mia lakini hakuna tumaini lolote unaloliona juu ya ufanyaji wa mambo hayo, kweli inaumiza sana, lakini kwa usalama wa maisha yako ni muhimu ukaanza upya tena…
Huenda mpaka umefika hapo umefanya juhudi nyingi sana, na umeona kama hakuna haja ya kuendelea tena kupambana.
Kwamba juhudi zako na matokeo hazina na uwiano sawa, ilihali katika hali ya kawaida juhudi na matokeo zinatakiwa ziwe na uwiano sawa. (Input and output must balance)
Kama umefika hatua hii basi ninakusihi ujiulize maswali yafuatayo:
Ninafanya nini kwa wakati huu? ...
Je ni kwa namna gani nitafanya kwa utofauti endapo nitapata wasaa mwingine tena wa kufanya jambo hili? ..
Unatakiwa kujua kwamba endapo utakuwa unafanya kitu kwa namna ileile uliyozoea kufanya mara zote hutopata matokeo tofauti na yale ambayo huwa unayapata siku zote…
Sikatai kwamba kuanza upya ni swala jepesi bali ni suala zito kwani, kwani tokea utotoni hadi utu uzima wako umefanya juhudi kubwa sana, huku ukiwa unapitishwa kwenye mifumo tofauti tofauti.
Na, mategemeo yako yakiwa ni kupata mabadiliko maishani mwako lakini hakuna chochote kile kinachoendelea…
Huenda kuna mfumo uliingizwa na umeenda nao hadi umefika asilimia mia lakini mwisho wa siku hakuna matumaini yoyote yale.
Kwamba hakuna chochote cha maana unachokipata zaidi ya kuteseka tu…
Tuchukulie labda mfumo wa elimu, kwamba umetumia zaidi ya miaka 18 katika kujifunza hadi kuhitimu, lakini mwisho wa siku umeishia kukutana na tatizo la ukosefu wa ajira…
Kwamba matarajio yako yalikuwa ni kupata ajira, sasa basi umeenda na mfumo mzima ukitarajia ajira lakini mwisho wa siku hakuna chochote kinachoendelea, najua inauma lakini huna budi kuanza upya, kwani ukiamua uache hivyohivyo hakuna chochote kile kitakachobadilika zaidi ya kuteseka zaidi na zaidi...
Sasa hapo jaribu kuhusisha na masuala mengine mengi ambayo huenda umeshayafanya kwa muda mrefu na umeenda nayo mbali sana lakini, hakuna chochote cha maana kinachoendelea kwayo zaidi ya kupoteza dira na matumaini yako...
Natambua inakuuma kwa sababu umewekeza juhudi zako kwa muda mrefu, lakini bado umeishia kuvuna upepo, yaani ulipanda mbegu njema lakini umeishia kuvuna upepo! Pole sana!
Lakini nina habari njema kwako wewe mpendwa wangu..
Habari yenyewe ninayotaka nikujuze ni kwamba, wakati uliokubalika ndiyo sasa! Kwamba huu ndiyo wakati wa kuanza upya…
Unatakiwa kujua kwamba, kila binadamu ana sehemu kuu mbili za maisha yake, yaani sehemu aliyoiishi na sehemu ambaya bado hajaiishi.
Kutokana na ukweli huo ndiyo maana leo hii niko mbele zako kukusihi uanze upya!
Kwanini uanze upya? Unatakiwa uanze upya kwa sababu huenda katika kuishi kwako umeishia kuishi sehemu duni tu ya maisha yako, bali ile sehemu ya maisha yako iliyojaa utele na mafanikio bado hujaanza kuiishi, IKIWA hiyo ndiyo sehemu halisi ya maisha yako.
Ndugu ni muhimu ukaanza upya ili ubadili maisha yako, kwani pasipo kufanya hivyo hakuna atakayefanya hivyo kwa ajili yako…
Na, ndiyo maana hata mwanasayansi Isaack Newton alikuja na kanuni ya inertia inayosema kwamba, “vitu vilivyotulia vitabaki katika hali ya utulivu mpaka pale itakapotokea fosi kutoka nje itakayovisukuma, ikiwa vitu vilivyo katika mwendo vitabaki katika hali ya mwendo mpaka pale vitakaposimamishwa”.
Hii inamaanisha kwamba hata maisha yako yatabaki kama yalivyo kama hutoamua kuyabadili, na ndiyo maana niko hapa kukusihi uanze upya…
Ndiyo bosi, inatakiwa uanze upya kwa sababu mifumo iliyokutengeneza haijakuletea upya wowote ule maishani mwako…
Hivyo basi wewe hapo ndiyo una wajibu wa kuanza upya, na endapo hutafanya hivyo, maisha yako yatabaki kama yalivyo kama kanuni ya inertia inavyosema…
Najua unajiuliza naanzaje upya? usijali fanya yafuatayo:
1. Tumia Kanuni Ya Kichocheo Na Matokeo
Kwa muda mrefu nimekuwa gizani kutokana na kutokujua kanuni hii.
Lakini mara baada ya kujua kanuni hii nuru kubwa iliangaza maisha yangu! Na maisha yangu yalibadilika siku hiyohiyo.
Kanuni ya kichocheo na matokeo inasema kwamba “kwa kila kinachotokea maishani mwako kuna kichocheo chake maalumu”.
Na, ndiyo maana huwezi ukapata matokeo ambayo hayana kisababishi kilichopelekea kutokea kwake.
Hii inamaanisha kwamba hata hali unazopitia katika maisha yako ni matokeo ambayo yana visababishi vyake maalumu vilivyopelekea kutokea kwake.
Na, kama unapitia hivyo kutokana na vichocheo mbalimbali basi unaweza ukabadili upya maisha yako kwa kutafuta vichocheo vipya vitavyochochea mabadiliko ya matokeo maishani mwako...
Je utatumiaje kanuni hii? Ni rahisi sana my friend... unachopaswa kufanya ni kuchagua matokeo unayoyataka.
Mara baada ya kuchagua matokeo unayoyataka, utatakiwa uchague vichocheo vitakavyopelekea matokeo hayo!
Ukiweza kufanya hivyo utakuwa umepiga hatua kwa kiasi chake!
Kwa mfano kama unataka kufanikiwa kifedha unaweza ukaamua kutafuta vichocheo vitakavyopelekea mafanikio hayo.
Unachopaswa kujua ni kwamba mafanikio hayaji kwa kuchagua matokeo unayoyataka tu, bali yatakuja kutegemeana na vichocheo utakavyovichagua ili vikuletee matokeo hayo!
Kwa mfano unaweza kuchagua kufanikiwa kifedha kama matokeo unayoyataka, mara baada ya kufanya hivyo ukaorodhesha: kutafuta ujuzi wa kutengeneza pesa, kutafuta ujuzi wa kufanya pesa yangu ijizalishe, kutafuta ujuzi unaohusu bajeti pamoja na kujiongezea ujuzi wa kudhibiti pesa zangu zisipotee...
Hii inamaanisha kwamba ni lazima nitafanikiwa kifedha kwa sababu nimeorodhesha vichocheo vitakavyopelekea mafanikio hayo!
Ahsante Sana kwa kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya...
Kesho nitaendelea na mbinu ya pili ya kuanza upya!
Somo hili lipo kwa makala, kwahiyo ukihitaji makala nzima njoo inbox!
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; mwalimu, mwandishi, muelimishaji katika eneo la maendeleo Binafsi, life coach and consultant!
Unaweza kuwasiliana nami kupitia Whatsapp +255744284329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com
Comments
Post a Comment