Kwani Tatizo Lako Ni Nini…?
Hivi Unafahamu Kuwa Asilimia Kubwa Ya Watu Duniani Kote Huishia Kulaumu Kuhusu Matatizo Wanayokumbana Nayo Pasipo Kuchukua Hatua Stahiki Dhidi Ya Matatizo Hayo?
Suala Hili Ndilo Limechangia Kwa Kiasi Kubwa Dunia Iwe Ni Sehemu Ya Kukutana Na Matatizo Ya Kila Aina.
Hii Ni Kwa Sababu Watu Waliopo Wanakumbana Na Matatizo, Halafu Hawachukui Hatua Yoyote Ile Katika Kuyakabili.
Kutokana Na Hilo Matatizo Hayo Yanakuwa Yanarithishwa Kizazi Hadi Kizazi...
Pia, Unatakiwa Kujua Kwamba Huwezi Ukapata Matokeo Tofauti, Kama Utaendelea Kufanya Mambo Yaleyale Ambayo Umezoea Kufanya Siku Zote.
Hii Inamaanisha Kama Umekuwa Ni Mtu Wa Kulaumu Tu Kuhusu Matatizo, Endapo Hutobadili Njia Nyingine Ya Kuyakabili Matatizo Zaidi Ya Kulaumu, Huwezi Ukapata Matokeo Tofauti, Bali Matatizo Yako Yatabaki Palepale...
Hata Hivyo Ni Muhimu Ukafahamu Kwamba Hakuna Kiwango Cha Lawama Ambacho Hutatua Tatizo, Laumu Utakavyoweza, Ukiweza Tukana Hata Kutukana, Lakini Nipo Hapa Kukufahimisha Kuwa Hakuna Chochote Kile Kitakachobadilika Kwenye Matatizo Yako.
Yaani, Matatizo Yako Yatabaki Kama Yalivyo, Hata Kama Utapandisha Hasira Na Lawama Zako Zifike Asilimia Mia Moja.
Tatizo Ni Nini Labda? Tatizo Ni Kitu Chochote Kile Ambacho Huibuka Kama Kikwazo, Kwamba Huweza Kuathiri Utokeaji Au Ufanyikaji Wa Jambo Fulani Au Kutatiza Jambo Hilo Lisitokee Kabisa.
Au, Tatizo Ni Ile Hali Iliyo Kinyume Na Matarajio. Kwa Mfano Ulitarajia Kupata Furaha Maishani Mwako Halafu Ukajikuta Ukikumbana Na Huzuni Nyingi.
Hii Inamaanisha Huzuni Ni Tatizo Kwako Kwani Matarajio Yako Yalikuwa Ni Furaha…
Hivyo Basi Huzuni Ni Hali Iliyo Kinyume Na Matarajio Yako.
Kwamba, Badala Ya Kukutana Na Furaha (Matarajio Yako) Umejikuta Ukikutana Na Huzuni Tu (Tatizo)…
Yapo Mambo Mengi Ambayo Wanadamu Hukumbana Nayo, Wakidhani Kuwa Ni Matatizo Ilihali Mambo Hayo Siyo Matatizo, Bali Tatizo Ni Wao Wenyewe Kwamba Hawana Uelewa Wowote Juu Ya Mambo Hayo Pamoja Na Kuwa Na Mitizamo Hasi Juu Ya Mambo Hayo.
Na, Ndiyo Maana Ishawahi Kusemwa Kwamba Tatizo Siyo Tatizo Bali Namna Unavyoliona Tatizo Hilo Ndiyo Tatizo Lenyewe, Kwamba Unaliona Tatizo Kutegemeana Na Wewe Ulivyo Na Siyo Kwamba Tatizo Hilo Liko Hivyo…
Ukiona Unakumbana Na Shida Au Changamoto Fulani Ambazo Hazikuzuii Usifanye Jambo Fulani Hayo Siyo Matatizo Bali Ni Maisha Tu…
Yes Boss, Ni Sehemu Ya Maisha Tu Kwani, Hakuna Mtu Ambaye Huwa Hakumbani Na Tatizo, Adha Au Changamoto Fulani Bali Kila Mtu Hukumbana Nazo.
Kwamba Hivi Ni Vitu Unavyotakiwa Upitie Ili Mradi Uko Hai. Na Kama Wewe Hutaki Ukutane Na Matatizo Ni Nani Unayemtaka Akutane Nayo? Ndugu Matatizo Yapo Ili Kukoleza Ladha Maisha Yetu, Yes Yapo Ili Kuyapa Maisha Ladha…
Fahamu Ukweli Kuhusu Matatizo..
1. Matatizo Hayakwepeki
Maisha Yetu, Ni Kama Shule Hivyo Matatizo Ni Kama Mitihani Kwamba, Matatizo Yapo Kukuvusha Na Kukupeleka Ng’ambo Nyingine Endapo Utayatatua...
Hivyo Basi Unatakiwa Kujua Kuwa Ukiwa Hai Kukutana Na Tatizo Ni Hali Ya Kawaida, Na Matatizo Hutukumba Ili Yatudhihidrishie Uwezo, Thamani, Ukomavu Wetu Na Ukuu Wetu.
Vilevile Matatizo Yapo Ili Kudhihirisha Ukuu Wa Mungu Wetu, Kwamba Kwa Macho Yako Uliona Hili Halitatatuliwa Ila Yeye Katenda Na Kaliondoa Kabisa, Kwanini Yeye Ni Mungu Wa Wazekenayo Na Si Mungu Wa Yasiyowezekana…
2. Matatizo Yote Hutatulika.
Hakuna Tatizo Ambalo Huwa Halitatuliki, Kwamba Kutokuona Njia Ya Kutatua Ya Kutatua Tatizo Hilo Haimaanishi Kwamba Tatizo Hilo Halitatuliki. Kila Tatizo Hutatulika…
Na, Ukiona Hakuna Njia Ya Kutatua Tatizo, Maana Yake Hapo Hakuna Tatizo Kwani Matatizo Yote Hutatulika…
3. Matatizo Ni Fursa.
Kila Tatizo Ni Mbegu Iliyopandwa Kwa Ajili Ya Fursa Zako. Matatizo Hudhiridhisha Thamani Yako Na Uwezo Wako.
Kwa Mfano Kutokana Na Ukosefu Wa Elimu Ya Kujitambua Kama Tatizo Nimeanza Kutatua Na Ninalipwa, Na Thamani Yangu Inazidi Kukua Kila Leo..
Hii Inamaanisha Kutokana Na Uwepo Wa Matatizo Ya Watu Mimi Nimepata Fursa Ya Kutengeneza Kipato Pamoja Na Kujitengenezea Thamani Zaidi Na Zaidi..
Fahamu Kuhusu Aina Za Matatizo.
Kuna Aina Tatu Za Matatizo, Kama Zifuatazo:
1. Tatizo Lililopo Akilini.
Ni Lile Tatizo Ambalo Bado Halijawa Halisi Lakini Kifkra Unaliona Kuwa Litakuja Kutokea…
Kwa Mfano Unaweza Ukawa Unaona Kuna Hali Ngumu Inakuja Mbele Yako, Ila Kwa Wakati Huo Hauna Hali Yoyote Iliyo Ngumu…
Matatizo Haya Huja Kutokea Kweli Kwani Kanuni Ya Msawazo Wa Akili Inasema Kwamba, “Kile Unachokipata Kwenye Maisha Ni Uhalisia Wa Kile Unachokitengeneza Akilini”
Jinsi Ya Kulikabili Tatizo Hili Ni Kufanya Mind Reprograming Kwa Kuanza Kuona Hali Nzuri Inakuja Badala Ya Kuona Hali Nzuri.
Kumbuka Kile Kanuni Ya Msawazo Wa Akili Inasema..
2. Tatizo Linaloonesha Dalili Za Kutokea Kwake…
Kama Walivyopata Kusema Wahenga Kwamba “Dalili Ya Mvua Ni Mawingu”, Basi Hapa Kuna Ishara Kadhaa Unaziona Kabisa Kuhusu Kile Kitakachotokea Kama Tatizo Siku Zijazo.
Kama Ni Bishara Utakuta Mauzo Yanaporomoka Kila Leo Na Kama Ni Mahusiano Utakuta Mwenzi Wako Haeleweki, Mpaka Unashindwa Kutambua Upo Kwenye Mahusiano Yanayohusiana Na Nini...
Mbinu Kubwa Ya Kulikabili Tatizo Hili Ni Kuanza Kutafuta Suluhu, Pamoja Na Kuziba Mianya Yote Ambayo Inaweza Ikapelekea Kutokea Kwake.
Kumbuka Wahenga Walisema “Usipoziba Ufa Utajenga Ukuta”
3. Tatizo Halisi.
Hapa Ndipo Sasa Kile Ulichoona Akilini, Pamoja Na Kile Kilichoonesha Dalili Kinageuka Na Kuwa Uhalisia Kama Hatua Hazikuchukuliwa.
Hapa Ndipo Pale Kama Ni Ndoa Mke Atadai Talaka Na Kama Ni Biashara Itakufa Kabisa…
Sasa Haya Ni Matatizo Ambayo Yanahitaji Umakini Wako Mkubwa Sana, Kwamba Usipochukua Hatua Sahihi Utapata Matokeoa Mabaya Zaidi..
Mbali Na Hilo Tatizo Likiwa Katika Hatua Hii Unashauriwa Kutuliza Serikali Ya Kichwa Chako Vizuri Ili Uweze Kukabili Matatizo Hayo...
Unahitaji Kuwa Na Ujasiri Mkubwa Sana Na Roho Ngumu Ili Uweze Kukabili Matatizo Haya, Ukiwa Na Roho Nyepesi Hutoweza Kuyakabili..
Na Endapo Hautayakabili Matatizo Yako Hakuna Atakayeyakabili...
Ahsante Sana Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya!
Kesho Nitakusogezea Somo Lihusulo Jinsi Ya Kutatua Matatizo Hatua Kwa Hatua...
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e;
Mwalimu, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!
Unaweza kuwasiliana nami kupitia Whatsapp no +255744284329
Comments
Post a Comment