Utabadili Maisha Yako Siku Utakayojua Wewe Ni Nani...
Hivi unafahamu kwamba zaidi ya asilimia 80 ya watu wengi hapa duniani, hawana uelewa wa kutosha kuhusu wao wenyewe kiasi kwamba hawajui wafanye nini au wajifanyie nini?
Tatizo hili limekuwa ni sugu sana, kiasi kwamba tumekuwa na watu wazima (hewa) ambao hawana mchango wowote ule katika kubadili maisha yao na hata kuibadili jamii yetu!
Hali hii imepelekea maisha yetu Yazidi kudumaa na kudidimia zaidi kadri siku zinavyozidi kwenda mbele...
Hata hivyo, wadau walisema kwamba, kile usichokijua ndicho kitakachokuangamiza siku moja.
Hii inamaanisha kwamba usipojijua wewe ni nani, basi huko kutokujijua ndicho kitakuwa chanzo cha maangamizi yako!
Mbali na hilo Neno la Mungu linasema "Watu Wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa"
Kinachomaanishwa hapa ni kwamba, kama hutakuwa na maarifa ya kukutosha, basi ukosefu wa maarifa hayo ndicho kitakuwa chanzo cha maangamizi Yako!
Tupo kwenye dunia ambayo ina kizazi kilichojaa ukaidi mwingi sana!
Ukaidi wa kutokutaka kujifunza wakati hakina maarifa!
Ukaidi wa kutokutaka kupokea mabadiliko wakati dunia tuliyonayo inabadilika kila iitwapo leo!
Ukaidi wa kutokutaka kubadili mitizamo yao, ili hali kila siku mambo yanabadilika!
Ukaidi wa kutokutaka kusikiliza sauti zao za ndani na kuamua kufuata mifumo ya dunia hii!
Ukaidi wa kutokutaka kumsikiliza Mungu na kuamua kufuata njia zao na mawazo yao wenyewe yaliyo na ukomo...
Waswahili waliwahi kusema kwamba, "mtoto mkaidi hafaidi mpaka siku ya Eid"
Hii inamaanisha kwamba unapokaidi kutokujifunza ili ujijue, ilihali huna maarifa ya kutosha kuhusu wewe mwenyewe na maisha yako, maana yake hutayafaidi maisha yako mazuri uliyoumbiwa na Mungu wako ili uje uyaishi!
Mpenzi msomaji unatakiwa kujua kwamba utaanza kuishi maisha yako halisi siku Utakayojijua Wewe Ni Nani!
Na kama, bado hujajijua wewe ni nani maana yake, bado hujaanza kuishi maisha yako halisi!
Simaanishi wewe ni nani, kwamba unitajie jina au uniambie mimi ni mwanaume au mwanamke, lahasha...
Hapana, namaanisha kwamba unitajie sababu iliyokufanya uumbwe pamoja na kunitajia kwa ubayana thamani Yako na utu wako!
Unatakiwa kujua kwamba endapo utaweza kujijua katika maeneo hayo, utapata mwanga na ukishapata mwanga masna yake utafanyika kuwa nuru!
Na ukishakuwa nuru maana yake utakuwa mwangaza wa maisha yako!
Hii inamaanisha utaweza kuishi yale maisha halisi uliyoumbiwa uje uyaishi!
Unatakiwa kujua kwamba, sababu kubwa ambayo imetufanya wengi tusiishi maisha yetu halisi ni kwa sababu maarifa tuliyonayo kuhusu sisi yameshindwa kututambulisha sisi ni akina nani!
Je vipi maarifa uliyonayo unaona yametosha kukutambulisha wewe ni nani?
Kama jibu ni ndiyo, je wewe ni nani?
Na kama jibu ni hapana unaweza ukafanya nini ili uweze kujijua?
Mpenzi msomaji kujijua wewe ni nani, ni Jambo jepesi sana!
Lakini pia linaweza kuwa jambo gumu sana!
Unatakiwa kujua kwamba kile Unachokijua Ndicho Kitapima umbali utakaoenda, hii inamaanisha kwamba endapo utajijua wewe ni nani utaenda mbali sana kimaisha, lakini endapo utajijua kidogo hakuna hatua utakayopiga!
Vilevile unatakiwa kufahamu kwamba, huwezi ukaenda Mbali zaidi ya pale ulipoishia kujijua...
Hata hivyo kiwango chako cha kujijua ni kama kibali kitakachokuruhusu uishi maisha yenye hadhi fulani...
Hii inamaanisha kwamba, endapo utajijua zaidi utaweza kuishi maisha yenye ukuu, furaha na mafanikio, ilihali usipojijua hutaishi maisha yenye ukuu, amani na mafanikio...
Mbali na hilo na ifahamike kwamba, usipofanya juhudi ili ujijue wewe ni nani, hakuna atakayekuja kufanya hilo kwa ajili Yako!
Mpenzi msomaji kuna vitabu vingi sana ambavyo huangaza maarifa mbalimbali kuhusu eneo hili la kujijua ( personal development books)
Imagine kuna kitabu unakisoma, halafu unajikuta kinakubadili kabisa!
Yaani kitabu kinakupambanua wewe vizuri mno, kiasi kwamba ukisoma unatoka gizani na kuwa nuruni!
Hii inamaanisha kwamba, ukitaka kujijua vizuri Wewe Ni Nani huna budi kujifunza kila leo pamoja na kusoma vitatu mbalimbali!
Habari njema kuhusu wewe ni kwamba, wewe ni mtu mkuu sana, unayeweza, mwenye nguvu, mwenye mamlaka makubwa sana hapa duniani na unastahili uishi maisha yenye furaha, amani na mafanikio makubwa!
Lakini umeshindwa kufikia hatua hii kwa vile umeshindwa kujijua wewe ni nani!
Mpenzi msomaji huna budi kurudi kwenye chanzo chako!
Yes mrudie Mungu wako Kwani yeye anakujua vizuri wewe ni nani, kuliko hata wewe unavyojijjua!
Hii inamaanisha kwamba, ukijiunganisha kwake maana yake utajijua wewe ni nani!
Na ukishajijua wewe ni nani utaweza kujisimamia, kujiongoza na kujitawala!
Ukipata muda kasome, Zaburi 139:1-2
Neno la BWANA linasema, "Ee BWANA, umenichunguza na kunijua, Wewe wajua kuketi kwangu na kuondoka kwangu
Umelifahamu wazo langu tokea mbali"
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; mwandishi, mwalimu, muelimishaji katika eneo la maendeleo Binafsi, life coach and consultant!
Unaweza kuwasiliana nami kupitia Whatsapp no +255744284329.
Comments
Post a Comment