Jinsi Ya Kupata Matokeo Unayoyataka, mbinu ya 4&5
4. Jiweke Huru Kutoka Kwenye Vikwazo...
Kwa chochote kile utakachoazimia kukifanya lazima kuna vikwazo huibuka!
Kwa mantiki hiyo usipojiweka huru kutoka kwenye vikwazo hivyo hutapata matokeo unayoyataka!
Rafiki, unatakiwa uvikabili vikwazo vyote ambavyo vitakufanya ushindwe kupata matokeo yale unayoyataka!
Hata hivyo kuna baadhi ya vikwazo vingine huwa vipo nafsini mwako kwa hiyo huna budi kuanza nafsi yako kwanza!
Kwa maana moja ya sababu ambazo hutatiza ndoto za wengi ni ile hali ya mtu kujiona hawezi na hastahili! (Self limiting beliefs)
Rafiki hutakiwi kujiona, huwezi, hustahili, wewe ni duni, wewe ni dhaifu na unatokea kwenye familia ya kimaskini.
Endapo utajiona hivyo, ni dhahiri kabisa hutaweza kupata matokeo yale unayoyataka!
Kwa maana hutopata hamasa na motisha ya kufanya juhudi ili upate kile unachokitaka!
Mbali na hilo Kanuni Ya Vikwazo inasema; “kwa chochote kile utakachoazimia kukifanya lazima kuna vikwazo vitaibuka”.
Hata hivyo mbali na kuibuka kwa vikwazo hivyo haimaanishi kwamba hutapata matokeo unayoyataka!
Bali utayapata matokeo unayoyataka endapo hutaruhusu vikwazo hivyo vikusimamishe.
Ndugu hutakiwi kuninukuu vibaya, sina maana kwamba vikwazo huibuka, kukwaza lahasha!
Ifahamike kwamba, vikwazo huibuka ili vikupe mbinu mbadala zitakazokusaidia ili upate kile unachokitaka.
Kuna watu huwa wanashindwa kupata matokeo wanayoyataka siyo kwa sababu hawawezi kuyapata, bali ni kwa sababu wamejifunga wenyewe kwenye gereza la vikwazo kwa kujiona: hawastahili, hawana uwezo, hawana akili za kutosha, wanatokea familia za kimaskini, hawana ujuzi wa kutosha, kwa sababu wao ni weusi pamoja na visingizio vingine ambavyo hujiwekea.
Ndugu unatakiwa kujua kwamba ili uweze kupata matokeo yale unayoyataka ni lazima ujiweke huru (ujitoe kwenye kila kikwazo), kuanzia akilini mwako, kwa maana kile unachokipata maishani mwako ni uakisi wa kile unachokiona akilini mwako!
Friend, unatakiwa kujua kwamba hakuna kitu huleta raha kama ule uhuru utakakaoamua kujipa mwenyewe akilini mwako, kwa kuruhusu kila kitu kipite kisha ukarelax!
Then ukajitamkia kwa imani kubwa kwamba, "nayaweza yote katika yeye anitiaye nguvu"
Hapo utakuwa umepasua na kuvunja vikwazo vyote, baada ya hapo tegemea kupata matokeo unayoyataka!
Hata hivyo ninachotaka ufahamu hapa ni hiki kitu; "duniani hakuna vikwazo halisi zaidi ya vikwazo unavyojiwekea mwenyewe kupitia mtindo wako wa kufikiri"...
Yes, boss kutokana na hilo ndiposa ukatokea huu usemi maarufu usemao "maisha ya binadamu ni matokeo ya Fikra zake mwenyewe"
Na ndiyo maana hata mithali 23:7 inasema: "maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo"
Habari njema ni kwamba, ukishajiweka huru, utajipa mamlaka, ukishajipa mamlaka utapata nguvu za kupambana, ukishapata nguvu za kupambana hakuna kitakachokusimamisha, na kama hakutakuwa na kitakachokusimamisha maana yake utayapata yale matokeo unayoyataka!
And I'll see you at the top!
5. Ufikie Mwisho Mwema Unaoutaka Akilini Mwako Kwanza...
Kile unachokiona akilini ndicho unachokipata maishani mwako!
Huwezi ukakivuta/ukakipata kitu ambacho akilini mwako bado hujakiwaza au hujakiona!
Hata hivyo kwa mujibu wa tafiti nyingi za kisaikolojia zilizofanyika zimeonesha kwamba, hakuna kitu chenye nguvu kama picha kwenye mfumo wa ufanyaji kazi wa ubongo wa binadamu, hasa linapokuja suala la uchakataji ili matokeo fulani yatokee!
Hii ni sawa na kusema ubongo wako huchakata picha kwa haraka sana ili kuyafanya yale yaliyoonwa yaje yatokee.
Kwa hivi ili uweze kupata matokeo unayoyataka ni lazima kiakili uufikie mwisho wa matokeo hayo (uyaone kama uhalisia kabisa)!
Na, ndiyo maana kuna usemi maarufu usemao, “yule unayemuona ndiye utakayekuwa” kutokana na usemi huo tunaweza kusema kwamba, “kile unachokiona ndicho utakachokipata”
Je, akilini mwako kuna picha gani juu ya matokeo ya kile unachokitaka?
Huenda unatamani matokeo yenye mwisho mwema halafu akilini mwako unaona matokeo mabaya, nipo hapa kukufahamisha kwamba hicho unachokiona ndicho utakachokipata!
Friend, unatakiwa uwe na picha kamili juu ya matokeo unayoyataka, kwani ukishauona mwisho utaupata utayari wa kuufikia mwisho huo!
Na, ndiyo maana kanuni ya msawazo wa akilini inasema kwamba “kile unachokipata maishani mwako ni uakisi wa kile unachokitengeneza akilini mwako kupitia picha mbalimbali unazozitengeneza mwenyewe”
Hivyo basi ili uweze kupata matokeo unayoyataka, kifikra unatakiwa uyafikie matokeo hayo!
Kwa mfano kama unatafuta kazi nzuri jione tayari upo ofisini na unafanya kazi hiyo, kinachomaanishwa hapa ni kwamba (kwa chochote kile unachokitaka, kifikra uone tayari unamiliki kitu hicho)...
Friend kuna umuhimu mkubwa sana wa kutengeneza picha kamili ya matokeo unayoyataka!
Kuanzia saa hii anza kuuona mwisho mzuri wa matokeo unayoyata! Kumbuka kile unachokiona ndicho utakachokipata!
Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya!
Somo Lihusulo Jinsi Ya Kupata Matokeo Unayoyataka Litaendelea Tena Kwa Siku Ya Kesho!
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Mwl, Mwandishi Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!
Unaweza kuwasiliana nami kupitia Whatsapp no +25673184329 au tembelea blog yangu kwa kuandika, ekingunge.blogspot.com
Comments
Post a Comment