Jinsi Ya Kupata Matokeo Unayoyataka. Mbinu Ya 6,&7
6. Jua Gharama Zitakazohitajika Pamoja Na Kuwa Tayari Kulipa Gharama
Kwa kila matokeo mazuri na ya maana utakayoyataka ni lazima kuna gharama utatakiwa kulipa kwanza!
Rafiki, huwezi kupata matokeo unayoyataka pasipo kujua gharama zitakazohitajika ili uweze kupata matokeo hayo!
Hii ni sawa na kusema, ili uweze kupata matokeo yoyote yale yaliyo mazuri ni lazima kuna gharama unatakiwa uwe tayari kuzilipa.
Na ifahamike kwamba, kujua matokeo unayoyataka siyo kigezo cha wewe kuyapata bali ni lazima ukubali kulipa gharama zitakazohitajika ili upate matokeo hayo!
Hivyo basi unachopaswa kufanya hapa ni kuchagua matokeo unayoyataka, baada ya hapo jua gharama zitakazohitajika, na ukishazijua gharama hizo kuwa tayari kuzilipa ili uweze kupata matokeo unayoyataka.
Kumbuka tupo kwenye ule ulimwengu ambao kitu unachoweza kukipata bure ni salamu tu, cha ajabu ni kwamba watu wenye siku hizi hawasalimii sijui uungwana unapotelea wapii?
Hata hivyo unatakiwa kujua kwamba gharama zitakuwa kama kichocheo halafu kile utakachokipata mara baada ya kulipa gharama zinazotakiwa, ndiyo matokeo yenyewe.
Ndugu kipengele cha gharama hakikwepeki ndiyo maana ni muhimu ukatambua baadhi ya gharama utakazopaswa kuzilipa.
Mfano wa gharama hizo ni pamoja na: gharama ya fedha, gharama ya muda (kuchelewa kulala na kuamka mapema), gharama ya kujitoa sadaka, gharama ya kuwa wewe pekee, gharama ya kihisia pamoja na gharama ya uvumilivu!
Kwa mfano kama ninataka matokeo ya kuongeza mauzo kwenye biashara yangu maana yake ni lazima nijue gharama zitakazonisaidia ili nipate matokeo hayo!
Kutokana na hilo ninaweza kuongeza ujuzi wa mauzo na usokoaji, ambapo kuna gharama nitapaswa kuzilipa ili niweze kupata ujuzi huo, matokeo yake nitapata ujuzi utakaonisaidia niweze kupata matokeo ninayotaka (kuongeza mauzo kwenye biashara)
Kwa hiyo ili uweze kupata matokeo unayoyataka ni muhimu kujua gharama utakazopaswa kuzilipa ili uweze kupata matokeo hayo!
Yaani jua unachokitaka, Halafu kuwa tayari kulipa gharama!
Mchezo unakuwa umeisha kiulaini yaani kama kunywa maji vile!
6. Fanya Jambo Fulani Kila Siku
Kadri siku zinavyozidi kwenda mbele ndivyo unavyotakiwa uwe unapiga hatua ya kusonga mbele ili kuyafikia matokeo ya kile unachokitaka!
Kwani hakuna matokeo ambayo hayapatikani pasipo kipindi cha muda fulani kupita!
Yes boss, kuna kipindi cha muda lazima kipite ili uweze kupata matokeo unayoyataka!
Kutokana na hilo huna budi kufanya jambo Fulani juu ya matokeo unayoyataka kila siku iendayo kwa Mungu.
Kwa mfano kama kuwa mwimbaji ndiyo matokeo unayoyataka, maana yake kila siku unaweza ukaamua kutenga hata masaa mawili utakayoyatumia ili uweze kufanya jambo juu ya matokeo hayo unayoyataka...
Hii ni sawa na kusema, unaweza ukatumia sehemu ya muda huo kutunga nyimbo, kutafuta maarifa mbalimbali kuhusu utungaji pamoja kufanya mazoezi ya uimbaji.
Endapo utafanya hivyo kila siku lazima utapata yale matokeo unayoyataka, unatakiwa ufanye kila siku kwa sababu kujaribu kwa vitendo ndiko hutufanya tuwe bora.
Jaribu kufikiri kila siku ukawa unafanya jambo fulani juu ya matokeo unayoyataka, utakuwa mbali kiasi gani baada ya siku 365 (mwaka mmoja) kupita?
Ama hakika utakuwa mbali sana! Na hapo ni lazima upate matokeo unayoyataka!
Hivyo basi kila siku kunapokucha hakikisha unafanya jambo Fulani litakalokuwa linakusogeza kwenye yale matokeo unayoyataka!
Kwa minajiri hiyo, ni lazima utapata matokeo unayoyataka!
Himisho: hakuna matokeo mazuri ambayo hujitengeneza yenyewe.
Unatakiwa kujua kwamba matokeo mazuri ni lazima yatengenezwe ikiwa matokeo mabaya huja tu pasipo hata kutengenezwa.
Hii ni sawa na kusema kushindwa kupanga ni sawa na kupanga kushindwa!
Tuchukulie kufaulu na kufeli, kwamba ili ufaulu lazima uweke mkakati utakaopelekea kufaulu kwako, ilihali kufeli kutakuja tu pasipo kuweka mkakati wowote ule!
Ndugu unatakiwa ujue unachokitaka kwanza ndipo sasa ukipate, kumbuka usipojua unachokitaka yale usiyoyataka ndiyo yatawala maisha yako!
Ndimi Emmanuel Samuel King’ung’e, Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!
Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No +255673184329 Au Tembele Blog Yangu Kwa Kuandika ekingunge.blogspot.com
Comments
Post a Comment