Tatizo Siyo Kilichotokea Tatizo Ni Kile Unachokiamini... ni

Hivi unafahamu kwamba zaidi ya asillimia 80 ya watu wanaamini zaidi katika imani potofu, kuliko imani thabiti hali ambayo hupelekea anguko lao? 
Unatakiwa kujua kwamba imani ni kama mbegu, ambayo ikipandwa humea, ikishamea hukomaaa, ikishakomaa huzaa matunda ya aina yake, ikishazaa matunda basi matunda hayo huchumwa…

Mlolongo huo unaonesha ni kwa namna gani unapoamini katika jambo Fulani ndivyo unavyokuja kulivuna jambo hilo kutegemeana na ile imani uliyoipanda kuhusu jambo hilo…
Mpenzi msomaji unatakiwa kujua kwamba kuamini ni kupokea kuwa jambo Fulani ni kweli hata kama jambo hilo halipo hivyo…
Kutokana na hilo ni dhana potofu kuamini katika imani potofu kwani kile utakachokiamini kuwa kipo vile kitakuja kutokea kama vile wewe mwenyewe ulivyokiamini...

Na, ndiyo maana hata kanuni ya kuamini inasema, “chochote utakachokiamini kuhusu wewe na dunia yako kitafanyika kwako kama uaminivyo”
Unatakiwa kujua kwamba kanuni hii inafanya kazi kwenye imani thabiti au imani potofu. 

Na ifahamike kwamba msisitizo mkubwa umewekwa kwa kile unachokiamini. 
Hivyo basihaijalishi utakachokiamini kitakuwa ni kizuri au kibaya, bali hicho ndicho utakachokipokea kwani umeamini hivyo… 

Kwani ishawahi kusemwa kwamba, "nawe utapokea kwa kadri ya uaminivyo".
Hata hivyo unatakiwa kujua kwamba yule anayeamini anaweza na yule ambaye anaamini kuwa hawezi wote wako sahihi, kwani kile unachokiamini ndicho chenye mashiko zaidi…

Kwamba ukiamini jambo Fulani linawezekana nalo litawezekana, pia, ukiamini jambo Fulani haliwezekani nalo halitawezekana…
Kuwezekana na kutokuwezakana ni suala la kuamini tu. 
Hata hivyo unatakiwa kujua kwamba imani haijawahi kumsaliti mtu. Tangu lini ushawahi kusikia mtu amesalitiwa na imani yake?
 Mpenzi unatakiwa kuweka akilini kwamba Imani haijawahi kumsaliti muamini wake. kwamba kwa kile utakachokiamini utakipokea kama vile wewe mwenyewe ulivyokiamini!

Unatakiwa kujua kwamba kuwezekana au kutokuwezekana siyo kitu halisi, bali ile Imani uliyoiweka ndiyo hufanya kuwezekana au kutokuwezekana kiwe kitu halisi…

Kutokana na hilo, ndipo watu hugeuza kuweza au kutowezekana kuwe halisi...
Na ndiyo maana unaweza ukaona mtu anaamini anaweza kufanya jambo Fulani huku mwingine akiwa anaamini kuwa hawezi kufanya jambo hilo! 

Hata hivyo uwepo wa suala hili ndiyo umepelekea niamini kwamba tunaishi kwenye dunia moja tofauti kwani kila mtu anaiona na kuiamini kwa namna yake!

Hali hii imenifanya nijenge falsafa inayodai kwamba dunia ni wewe ulivyo, hii inamaanisha dunia itaakisi masuala kadhaa kuhusu maisha yako kutegemeana na mfumo wako wa kuamini ulivyo! 
Mpenzi msomaji unatakiwa kujua kwamba suala la kuamini lipo mikononi mwako kwamba unaweza kuchagua kuamini katika imani thabiti au imani potofu…
Hata hivyo ni heri sana ukafahamu kwamba kuamini katika uhaba huvuta uhaba, ikiwa kuamini katika utele huvuta utele…

Kutokana na ukweli huo, huna budi kujua kwamba hata hali zote unazopitia katika maisha yako umezivuta mwenyewe kutokana na mfumo wako wa kuamini…
Huenda uliamini zaidi katika Imani potofu kitu ambacho kimekufanya uvute matukio hasi maishani mwako…
Ni dhana potofu kuamini uliumbwa uje uteseke…
Ni dhana potofu kuamini uliumbwa uje uishie kuwa maskini…
Ni dhana potofu kuamini huwezi…
Ni dhana potofu kuamini hutokuwa na maisha mazuri…
Ni dhana potofu kuamini kwamba huwezi ukapata mke/mume wa chaguo lako…
Ni dhana potofu kuamini hutopata kazi nzuri…
Ni dhana potofu kuamini utaishia kuteseka maisha yako yote…
Ni dhana potofu kuamini bado u mdogo…
Ni dhana potofu kuamini kuna mtu atakuja kuwajibika kwenye maisha yako…
Ni dhana potofu kuamini kwamba huwezi ukaongeza pato lako…
Ni dhana potofu kuamini kwamba mafanikio yanatokana na bahati…
Ni dhana potofu kuamini kwamba matajiri hutumia njia ovu kupata mali zao…
Ni dhana potofu kuamini katika uhaba na ukomo…
Ni dhana potofu kuamini kitu Fulani kitakuletea madhara…
Ni dhana potofu kuamini mambo yatakaa sawa yenyewe…
Ni dhana potofu kuamini wewe ni mnyonge…
Ni dhana potofu kuamini kwamba huna bahati…
Ni dhana potofu kuamini wewe ni fungu la kukosa…
Ni dhana potofu kuamini una mikosi…

Ahsante sana kwa kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya!
Somo Lihusulo Tatizo Siyo Kilichotokea Tatizo Ni Kile Unachokiamini, Litaendelea Kwa Siku Ya Kesho!

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e, Mwl, Mwandishi Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant! 

Unaweza kuwasiliana nami kupitia Whatsapp no 0744284329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...