Tatizo Siyo Kilichotokea Tatizo Ni Kile Unachokiamini...
Mpenzi, unatakiwa kujua kwamba imani potofu ndiyo hupelekea upate matokeo hasi, kwa maana imani yako haiwezi kukusaliti wewe muamini wake!
Hivyo basi endapo utaamini katika dhana potofu matokeo yake yatakuwa ni kupotea...
Kwani nawe utapokea kwa kadri ya uaminivyo!
Na ifahamike kwamba, ni kupitia kuamini katika imani potofu ndiko kumekuwa kukiangusha jitahada zako pamoja na juhudi zako, kwani hata ukifanya juhudi huoni kama zitakulea matunda kwa kuwa umeamini kwamba wewe huwezi na si chochote kile...
Hii inamaanisha kwamba ni vigumu sana kupata hamasa ya kufanya jambo fulani, kwa sababu hata ukifanya imani yako inakuona wewe ni fungu la kukosa, na hakuna kitu cha maana unachoweza kukifanya au kukipata...
Hata hivyo kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kisaikolojia kuwahi kufanyika, zimeonesha kwamba mwanadamu huteseka zaidi kifikra kuliko uhalisia.
Unatakiwa kujua kwamba, unapofikiri kuwa jambo Fulani lipo hivi, maana yake unaanza kutengeneza imani kuhusu jambo hilo kwenye mfumo wako wa ubongo.
Kutokana na hilo, mwishowe utajikuta unaamini kwamba jambo hilo lipo hivyo hata kama jambo hilo haliko hivyo kabisa!
Na endapo utatengeneza fikra potofu kuhusu jambo hilo na ukaziamini, maana yake utakuwa umetengeneza imani potofu ambapo mwisho wa siku utapata matokeo kutokana na kuamini kwako!
Na, ndiyo maana hata wahenga walisema kwamba “utavuna ulichopanda”.
Hii inamaanisha kwamba atakayevuna ni yule aliyepanda tu.
Na, haijalishi alipanda nini, lakini sharti la kuvuna liko palepale!
Kwa mfano kama mpanzi huyo alipanda fikra hasi, na, akaziamini fkira hizo mwisho wa siku atakuja kuvuna matukio hasi katika maisha yake...
Kumbuka umeanza kupanda fikra fulani, ukaziamini mwisho wa siku utakuja kuvuna!
Sasa, aliyekuaminisha kwamba wewe huwezi ni nani?
Sasa, aliyekufanya uamini kwamba mahusiano sahihi hayapo ni nani?
Sasa, aliyekufanya uamini kwamba ulizaliwa uje uteseke ni nani?
Sasa, aliyekuaminisha kwamba hustahili ni nani?
Sasa, aliyekuaminisha kwamba huwezi kubadili maisha yako ni nani?
Sasa, aliyekuaminisha kuwa maisha yenyewe hayana maana ni nani?
Ni nani huyo aliyekuaminisha hayo yote, na je, ana uthibitisho upi juu ya ukweli wa mambo hayo?
Kwanza yeye ni nani mpaka aseme hayo yote kuhusu wewe? Je yeye ni Mungu kwamba anakujua zaidi kuliko hata wewe mwenyewe unavyojijua?
Friend ukiamini hivyo una tofauti gani na muuaji anayejiua mwenyewe?
Huoni kabisa kwamba, kuamini hivyo ni kujikatili pamoja na kujimaliza kabisa? Why kill your self my friend?
Kwanini usijionee huruma my friend? Hivi unafikiri kama wewe mwenyewe usipojionea huruma ni nani atakayekuonea huruma?
My friend unateseka sana si kwa sababu unatakiwa uteseke ila unateseka kwa sababu umeamini katika dhana potofu...
Sasa utatokaje hapo ulipo kama hutobadili mfumo wako wa kuamini katika imani potofu?
Unatakiwa kujua kwamba ni kanuni ya ulimwengu mzima kwamba maji hutiririka kwa kufuata mkondo, kadhalika na maisha yako yatatiririka kutegemea na mfumo wako wa kuamini…
Hii inamaanisha kile kitu ambacho unakiwaza na kukiamini ndicho utakachokipokea…
My friend huenda uliaminishwa kwamba: Huwezi!, Hustahili! Utashindwa Tu! Hutopata Nafasi! Wewe Ni Mkosaji! Una Mikosi! Hakuna Atakayejali kuhusu wewe! Mambo Yanaharibika Kila Siku Afadhari Ya Jana! Maisha Hayana Jema! Huwezi Kushinda! Mapenzi Ni Kwa Ndege Tu! Utafisirika! Huwezi Kufanikiwa Kwa Lolote Wewe Hapa Duniani Ni Msindikazaji Tu! Mifumo Siyo Rafiki! Utaishia Pabaya! Utaishia kuwa maskini tu! Utaishia Kuteseka Tu! N.k
Leo nipo hapa kukufahamisha kwamba hayo yote siyo kweli kabisa kuhusu wewe!
Unachopaswa kufanya ni kukataa kabisa!
Kwanini ukatae? Unatakiwa uyakatae kwa sababu Mungu alishakupa mamlaka na alishakupa utawala juu ya dunia hii...
Je utaendelea kutawaliwa mpaka lini na imani potofu?
Hapana... imetosha sasa.
Kuanzia leo hii anza kuamini kwamba wewe ni mtawala...
Unatakiwa kujua kwamba uliumbwa uje uishi maisha yenye furaha, Amani na mafanikio, lakini kwa kuwa umeamini katika ukomo ndiyo maana mateso, dhiki, na taabu hazikomi kwako.
Kwamba kupitia kuamini huko, ndiko kumekufanya uwe unavuta matukio hasi katika maisha yako, na ndiyo maana matukio hasi hayakomi maishani mwako!
Enyi watu wangu! Hata lini mtaachana na imani potofu?
Hata lini mtaanza kujiwazia mema ili myalete maishani mwenu?
Ndugu, inatosha sasa hebu jitoe kifungoni kwa kuamini katika imani thabiti.
Kwani ni kupitia kuamini katika imani thabiti ndiko hukupepeka kule iliko kweli ya maisha yako!
Friend, huhitaji kingine zaidi ya kubadilisha mfumo wako wa kuamini!
Unatakiwa kujua kwamba hakuna ambaye huzaliwa hawezi au hastahili bali kuamini kwake ndiko humfanya aone hawezi au hastahili…
My friend wewe unaweza, unastahili na unaweza kuwa mtu mkuu sana kuwahi kutokea hapa duniani…
Unahitaji tu kutengeneza imani chanya juu yako!
Somo Lihusulo Tatizo Siyo Kilichotokea Tatizo Ni Kile Unachokiamini Litaendelea Tena Kwa Siku Ya Kesho!
Ahsante sana kuwa mwanafamilia wa masomo haya!
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!
Unaweza kuwasiliana nami kupitia Whatsapp no +255744284329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com
Comments
Post a Comment