Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika
Katika mfumo wetu wa sasa wa elimu, mwanafunzi anafundishwa kusoma ili afaulu mtihani. Mtihani unapimwa kwa kukariri na kujibu maswali yaliyoandaliwa na mtu mwingine. Hakuna anayemuuliza mwanafunzi: "Kwa nini upo hai?" au "Umetumwa kufanya nini katika dunia hii?" Hii ni hatari. Kwa sababu tunazalisha wanafunzi wa alama, si wanafunzi wa maono. Tunalea waajiriwa wa mifumo isiyo na huruma badala ya kulea waongozaji wa jamii zenye uhai. Tuna mashule, tuna vyuo, tuna mitihani... lakini hatuna somo la kusudi. Na hapa ndipo tulipoanguka. Mtoto anakua bila kujua anasoma ili awe nani au atumike kufanya nini. Matokeo yake? Anajitahidi apate kazi yoyote ilimradi alipwe, hata kama kazi hiyo inaharibu mazingira, inahujumu jamii au inampoteza yeye mwenyewe. “Mwanadamu asiyejua kusudi lake ni sawa na meli isiyo na dira – itazunguka tu baharini hadi itakapogonga miamba.” Vijana wetu wanafundishwa kutafuta kazi, si kutafuta athari chanya katika dunia. Hili ni kosa la...
Comments
Post a Comment